Kati Ya Zitto Kabwe na Mbatia Nani anafanya kazi ya Kikwete? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kati Ya Zitto Kabwe na Mbatia Nani anafanya kazi ya Kikwete?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwamakula, Jul 28, 2012.

 1. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Zitto Kabwe alikuwa Upande Wa Mhando Tanesco na Kusema Maswi amekiuka Kanununi Za Manunuzi Kama Lowasa na hapa Maswi angeangushwa .

  Mbatia (Mteule wa Rais Kikwete)alilazimika Kuungana na Kafulila ambaye hana kadi ya Chama Chocote na Kusema Mhando kapanga mkataba Kitandani jambo ambalo litasababisha Mhando kutupwa Tanesco . Je Watu hawa wawili wanafanya kazi ya nani??? au Utawala unayumba ???  Ni Jambo la Ajabu Mbatia aliyependekeza Kafulila afukuzwe Bungeni kwa kumunyang'anya kati ya NCCR leo amekaa naye katika Vita hii??? Je , Vita hii anapigana kwa maslahi ya nani???

  [FONT=&amp] NCCR – MAGEUZI [/FONT]
  [FONT=&amp]National Convention for Construction and Reform – Mageuzi[/FONT]

  [FONT=&amp]Kumb Na. NCCR-M/MM/BJMT/10/21 [/FONT][FONT=&amp] 17 January, 2012[/FONT]
  [FONT=&amp]Mhe.Nee S. Makinda (mb)[/FONT]
  [FONT=&amp]Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,[/FONT]

  [FONT=&amp]Ofisi ya Bunge,[/FONT]
  [FONT=&amp]S.L.P 9133,[/FONT]
  [FONT=&amp]DAR ES SALAAM.[/FONT]
  [FONT=&amp]Mheshimiwa Spika, Salaam.[/FONT]

  [FONT=&amp]YAH: TASWIRA DHALILI YA CHAMA CHA NATIONAL CONVENTION FOR CONSTRUCTION AND REFORM – MAGEUZI KWA OFISI YA BUNGE.

  [/FONT]

  [FONT=&amp]Tafadhali husika na somo hapo juu.Chama chetu cha National Convention for Construction and reform – mageuzi (NCCR-Mageuzi) ni miongoni mwa vyama vya siasa vinavyotambulika hapa nchini na chenye usajili wa kudumu kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa, sura ya 258 ilivyoruhusiwa mwaka 2002.[/FONT] [FONT=&amp]Aidha unantaambua kwamba chama chetu kilishiriki uchaguzi mkuu wa Urais, Wabunge,Wajumbe wa baraza la Wawakilishi na Madiwani wa Mwaka 2010 ambapo tulifanikiwa kupata viti vya wabunge wane katika bunge Tukufu. [/FONT]

  [FONT=&amp]Mheshimiwa Spika, unatambua pia kwamba mnamo tarehe 21/12/2011, chama chetu kilikuandikia na kukufahamisha kuhusu hatua za kinidhamu alizochukuliwa aliyekuwa mmoja wa wanachama wake ndugu David Zacharia Kafulila na ambaye kwa tiketi ya chama hiki alichaguliwa kuwa mbunge jimbo la Kigoma Kusini. Barua yetu yenye Kumb. NA NCCR-M/MM/BJMT/10/20 iliyoandikwa na kukabidhiwa kwako kupitia kwa Katibu Mkuu wetu wa chama Ndugu Samuel AM. Ruhuza ya tarehe 21/12/2011 ikikufahamisha hatua hizo, na nina uhakika unayo ofisi kwako. Ni tegemeo letu kuwa hadi sasa ofisi yako ilitakiwa kuwa imeshachukua hatua zinazostahili kuhusiana na nafasi ya Mbunge ambaye amevuliwa uanachama wake na chama cha sias anachokiwakilisha Bungeni.[/FONT]

  [FONT=&amp]Tofauti na matarajio yetu, nasikitika kueleza kwamba ofisi yako imeamua kutoyatilia maanani matakwa ya kisheria yanayohusiana na nafasi ya Mbunge anayeacha au kuvuliwa uanachama na chama chake. Badala yake, ofisi yako imeendelea kumtambua ndugu David Zacharia Kafulila na kumpa fursa na nafuu zote za Mbunge bila kujali hatua za chama ambazo zilichukuliwa.[/FONT]

  [TABLE="align: left"]
  [TR]
  [TD][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][/TD]
  [TD] [TABLE]
  [TR]
  [TD]
  HEAD QUARTERS
  P.O.BOX 72474, DAR ES SALAAM, TANZANIA​
  Phone/Fax:+255-022-2862238/website:www.nccrmageuzi.or.tz/Email:info@nccrmageuzi.or.tz
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]


  [FONT=&amp]

  All correspondence should be addressed to the Secretary General[/FONT]


  [FONT=&amp]Mheshimiwa Spika, kana kwamba hayo hayatoshi, nikiwa mbele yako na katika hafla ya kuaga mwili wa marehemu Regia Mtema (Mb), aliyeaga dunia kwa ajali ya gari tarehe 14/01/2012 na mwili wake kuagwa leo tarehe 17/01/2012 katika ukumbi wa Karimjee. Ofisi yako imefanya kitendo cha kutudhalilisha, kutunyanyasa, kutufedhehesha,kutuonea na kejeli kwa maamuzi halali ya Halmashuri Kuu ya Taifa ya Chama chetu, licha ya kwamba umetoa tamko na msimamo wako binafsi na wa ofisi yako kwamba, Watanznia tuwe na moyo wa upendo na ushirikiano na kuacha itikadi zetu za vyama na tofauti zetu ndogo ndogo ili tujenge taifa moja lenye umoja na Upendo. Hii ilikuwa ni kauli nzito na inayoonesha msimamo wa ofisi yako wa kutenda kazi zake bila kujali itikadi za watu wala tofauti zao.
  [/FONT]
  [FONT=&amp]Wakati huo huo, nimesikitika pia kuona ofisi yako ikitenda kinyume na kauli yako nzito kama ilivyoelezwa hapo juu kwa kutangaza majina ya wabunge watakaowasilisha vyama katika mmsafara wa maziko huko Ifakara mkoani Morogoro, katika namna ambayo ilitukejeli, kutudhalilisha na kushusha heshima ya chama chetu cha kijamii. Hii imetokana na kauli ya mwendeshaji wa hafla hiyo kutoka katika ofisi yako alipoueleza umma wa watanzania kwamba mwakilishi wa chama cha NCCR – Mageuzi katika maziko atakuwa ndugu David Zacharia Kafulia. Kauli hii imetolewa mbele yangu nikiwa Mwenyekiti wa Taifa, Msimamizi Mkuu wa Maslaihi ya Chama na msemaji mkuu wa chama cha NCCR – Mageuzi na bila kujali athari za kisiasa na kiitikadi ambazo kwa sasa zipo kufuatia hatua za kumvua uanachama ndugu David Zacharia Kafulia katika chama chetu.[/FONT]

  [FONT=&amp]Mheshimiwa Spika, nasikitika pia kuiarifu ofisi yako kwamba kwa kumtangaza ndugu David Zacharia Kafulia kuwa mwakilishi wa NCCR – Mageuzi katika msafara wa maziko ni kukiuka kanuni na misingi ya haki. Ni dhahiri kwamba chama chetu hakijakuandikia barua ya kumtambulisha ndugu David Zacharia Kafulia kuwa mwakilishi wetu katika hafla hiyo, mbali na kwamba tunao wabunge wengine. Naamini kwamba hekima ya ofisi yako ingelitafakari athari za kitendo hicho cha chama chetu. Ni kitendo ambacho kinatupa ujumbe kwamba ofisi yako imetumika kukidhoofisha chama chetu, kwanza kwa kutoweka bayana masuala ya msingi yanayotokana na hatua za kinidhamu tulizozichukua na sasa kuanza kumnadi hadharani ndugu David Zacharia Kafulia kuwa mwanachama wetu ilhali ofisi yako inafahamu kuwa siyo kweli. Hizi fedheha ambazo ofisi yako inaanza kuzijenga na kuwataka watanzania wamtambue hivyo na kumjengea utukufu ndugu David Zacharia Kafulia kuwa yeye yuko juu ya chama. Hakika kwa kitendo hicho, haki haijatendeka, hekima haikutumika na busara zinakataa kukubaliana na jambo hilo.

  Mtu ambaye amevuliwa uanachama kwa kufukuzwa na chama husika hawezi leo hii akaonekana ndiye mtu pekee aliyeteuliwa kukiwakilisha chama hicho, tena katika hafla ya kitaifa.[/FONT] [FONT=&amp]Ingelikuwa ndugu David Zacharia Kafulia alipovuliwa uanachama wake tayari ameshahamia chama kingine je?, ofisi yako ingeendelea kumtambua kuwa mwanachama na mwakilishi wa NCCR – Mageuzi? Hii ni sawa na kiongozi wa dini kubadili imani yake na kuendelea kuongoza ibada za dini alikotoka. Ni dhahiri jamii haitamuelewa kiongozi huyo wa dini na pia waumini wenzake katika dini alikotoka hawatakuwa na imani naye tena ya kuwangoza katika ibada zao.[/FONT]


  [FONT=&amp]Ibara ya 71(1)(a) na (f) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 imeweka bayana kwamba Mbunge ataacha kuwa Mbunge na kiti chake kubaki wazi endapo sifa alizokuwa nazo wakati wa kuchaguliwa zitabadilika na kumfanya akose sifa hizo za kuwa Mbunge. Sifa hizo ni kuacha kuwa mwanachama wa cham cha siasa. Aidha, sifa za kuchaguliwa zimetamkwa katika ibara ya 67(1)(b) kuwa ili mtu awe Mbunge ni lazima awe na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa[/FONT] [FONT=&amp]Katika kumbukumvbu za Bunge lako tukufu, mnamo mwaka 2003, Chama cha United Democratic Party (UDP) kiwafukuza uanachama wabunge wake wawili ambao ni ndugu Danny Makanga pamoja na ndugu Erasto Tumbo. Matokeo yake, ofisi yako ilitambua hatua hizo na kuwaondolea ubunge wao kwa mujibu wa Katiba. Uchaguzi mdogo uliitishwa kuhusiana na majimbo waliyokuw wakitokea.[/FONT]

  [FONT=&amp]Mheshimiwa Spika, inasikitisha na inafedhehesha sana kwamba ofisi yako haijatutendea haki. Pamoja na kuwapo shauri katika Mahakama Kuu ya Tanzania kuhusu uamuzi wa Halmashauri kuu ya Taifa ya[/FONT] [FONT=&amp]NCCR – Mageuzi, bado hakuna amri yoyote ile inayokuzuia wewe kutekeleza majukumu yako kama mhimili mmojawapo wa dola.[/FONT]

  [FONT=&amp]Ni dhahiri kwamba kam ofisi yako ingezingatia kutenda haki katika suala hili, tayari ungelikwishamsimamisha ubunge ndugu David Zacharia Kafulila na kushirikisha taasisi za umma zinazohusika katika kusimamia na kuitisha uchaguzi wa jimbo Kigoma Kusini. Kuendelea kukaa na kutofanyia kazi suala hili muhimu Kitaifa, ofisis yako imesababisha mgogoro mkubw katika chama chetu na kuendelea kupandikiza chuki, fitina na majungu miongoni mwa wanachama, wapigakura na Watanzania kwa ujumla.[/FONT]

  [FONT=&amp]Mheshimiwa Spika kwa baruq hii, ni imani yangu kuwa ofisi yako itachukua hatua zinazostahili ili kulinda maslahi ya Chama cha NCCR – Mageuzi na kutoendelea kufedheheshwa na kudhalilishwa mbele ya Watanzania kama ilivyotokea leo.[/FONT]

  [FONT=&amp]Pamoja na salamu za Democrasia na Maendeleo.[/FONT]

  [FONT=&amp]Ndimi mtumishi mtiifu,[/FONT]  [FONT=&amp]…………………………..[/FONT]
  [FONT=&amp]James Francis Mbatia[/FONT]
  [FONT=&amp]MWENYEKITI WA TAIFA.[/FONT]


  [FONT=&amp]Nakala:[/FONT][FONT=&amp] Mhe. Mizengo K.P Pinda (Mb)[/FONT]
  [FONT=&amp] Waziri Mkuu wa JAMHURI YA Muungano wa Tanzania[/FONT]
  [FONT=&amp] Na Kiongozi wa shughuli za Serikali Bungeni,[/FONT]
  [FONT=&amp] S.L.P. 3021,[/FONT]
  [FONT=&amp] DAR ES SALAAM.[/FONT]
   
 2. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  [h=2]Zitto Kabwe na Jakaya Kikwete ni kitu Kimoja kuna nini TANESCO ????[/h]
  [​IMG]


   
 3. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  [h=2]Zitto na baadhi ya wabunge wa CCM wadaiwa kuhongwa na menejimenti ya TANESCO[/h]


  [​IMG]
   
 4. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #4
  Jul 28, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Ee bwana ee izi skandal za zitto na mbatia zimetuchosha..waache wazikane.
   
 5. m

  mwabakuki JF-Expert Member

  #5
  Jul 28, 2012
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 268
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  upuuzi mtupu....nani kakwambia kosa upimwa kwa ukubwa wake...kosa ni kosa na kila mtu atabeba mzigo wake...tambua hakuna kosa nusu..hatuwezi kuwa tunatafuta mwizi wa viatu wewe ukatwambia ulichukuavnyuzi za viatu ila viatu hukuiba alafu ukadhani utasalimika...kinachopimwa ktk makoea au jinai ni dhamira na ukubwa wa kosa wala udogo wake....tafadhali tunakuadharisha usitetee upuuzi hatuna muda kupoteza hapa...wewe kwani umekuwa microphone ya zitto mwache aje mwenyewe akanushe au athibitishe makosa yake hapa...kama kulinganisha makosa yake na wenzie aje hapa aseme mwenyewe
   
 6. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #6
  Jul 28, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,480
  Likes Received: 788
  Trophy Points: 280
  Sijakuelewa unataka nini
   
 7. kbosho

  kbosho JF-Expert Member

  #7
  Jul 28, 2012
  Joined: Jun 4, 2012
  Messages: 12,505
  Likes Received: 3,314
  Trophy Points: 280
  wote ni mashushushu! Bt zitto hs a fraud leadr
   
 8. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #8
  Jul 28, 2012
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Anayetetea Maslahi ya nchi katika hili, ndiye anayefanya kazi ya wananchi bila kujali anatoka chama gani.
  Hilo suala la Mbatia na Kafulila ni mambo ya misigishano ya kisiasa ambayo wanaweza wakayaweka tu pembeni na wakaamua kufanya kazi ya wananchi kwa pamoja. Kama Mbatia na Mdee waliweza kuelewana yakaisha kwa maslahi ya wana-kawe, nadhani ilitosha kueleza Mbatia kama anavyosema mara kadhaa, meza ya mazungumzo ni dawa ya misigishano ya kisiasa.
   
 9. Manyi

  Manyi JF-Expert Member

  #9
  Jul 28, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 3,256
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hueleweki bana, na habari yako ndeefu kama gazeti la Mzalendo!
   
 10. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #10
  Jul 29, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  [h=2]Wabunge wa CHADEMA Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kuhojiwa[/h]
  Habari za ndani ya uongozi wa juu wa Chadema nilizopata hivi punde zinasema Wabunge wa Chadema waliomo katika kamati ya Nishati na Madini inayovunjwa wataitwa mbele ya vikao vya juu vya chama hicho kujitetea kwa tuhuma za rushwa na ikithibitika walihusika wataombwa wenyewe wajiuzulu ubunge. Wakikataa watafukuzwa uanachama mara moja bila kujali nyadhifa zao katika chama.

  Naupongeza uongozi wa CDM iwapo watachukua hatua hii -- na itakuwa fundisho kwa kile chama cha rushwa ambacho kulindana kwao ndiyo utamadauni wao bila kujali athari kwa wananchi masikini.
   
 11. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #11
  Jul 29, 2012
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Safi sana, ila wanaotuhumiwa si wale tu waliokuwa katika kamati iliyovunjwa, tuhuma zingine zinaelekezwa kamati ya mashirika ya umma.
  Aidha, vikao vya juu vya chadema kabla ya kuwaita waheshimiwa hawa, navyo vikusanye ushahidi dhidi yao ili viweze kuwahoji dhidi ya ushahidi huo. Bila hivyo kuwahoji kutakosa mashiko, maana 'mwizi' kama kawaida yake, ni hodari wa utetezi.
   
 12. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #12
  Jul 30, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Admin upuuzi kam huu ni kuondoa ,sijui mtoa mada anaajenda ghani .ok tumfururahishe kwa kusema wote ni mashushu are u happy!! Ni miongoni mwa kampeni za kumtafuta mwenyekiti wa kamati ya bunge ya mashirika ya imma ,zito anaondoka kesho baada ya kikao cha kamati ya bunge ya maadili
   
Loading...