Kati ya watumishi wa umma, asiyeaminika kuliko wote ni MWALIMU! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kati ya watumishi wa umma, asiyeaminika kuliko wote ni MWALIMU!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sanga malua, Jul 18, 2012.

 1. s

  sanga malua JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa mtumishi wa umma kwa miaka 23 sasa, katika kipindi hiki hasa kuanzia awamu ya tatu mpaka sasa mtumishi wa umma asiye aminika na SERIKALI ni mwalimu.sijui nani katufikisha hapa!!! mwalimu hata aseme nini hataaminika mpaka POLISI,USALAMA WA TAIFA NA PENGINE mtu mwingine kutoka usitawi wa jamii aje athibitishe hilo linalo semwa ndio serikali waamini.ni kitu kibaya na kinacho katisha tamaa kweli. kamwe sitakaa nikubali mtoto wangu awe mwalimu.
  kwa muda mrefu tu walimu wamekuwa wakilalamika kuwa wanafunzi wano letwa miaka hii sekondari wengine hawajui kusoma na kuandika lakini hawakuaminika kuwa wanacho sema walimu ni kweli, kuthibitisha hilo serikali ikawatuma POLISI NA USALAMA WA TAIFA waje wawakague walimu kama wanacho sema ni kweli ndio uamuzi utolewe kuwa anacho sema mwalimu ni kweli na ni kweli tupu.
  zamani kidogo mwaka 1998 mtihani wa kidato cha nne mahali fulani ulivuja na kwa kuwa simu za mkononi ndio zilikuwa zimeanza kushamiri Nchini ule mtihani ulisambaa karibu nchi nzima kwa muda mfupi.bila kutafiti kwa kina chanzo cha kuvuja kwa mtihani ule SERIKALI ikaamua kuwa mitihani itakuwa ikisimamiwa na walimu lakini chini ya usimamizi wa POLISI NA USALAMA WA TAIFA!!! wamesahau kuwa tokea UHURU mpaka mwaka 1998 kwa karibu miaka 34 mitihani haikupata kuvuja ingawa ilikuwa inawekwa kwenye bahasha za khaki tu lakini walimu kwa uaminifu mkubwa waliisimamia ikafanyika kwa usalama mkubwa.1998 uaminifu wa walimu ukatoweka bila kupata kiini cha TATIZO.
  Ushauri wangu kwa serikali ni kuwa linapotokea tatizo fulani likaisibu Nchi kama lilivyo jitokeza katika usimamizi wa elimu dawa siyo kukimbilia kubadili nani wa kumwamini kinachotakiwa ni kufanya utafi wa kweli na wa kina mathalani katika uteuzi wa wasimaizi wakuu wa elimu unazingatia kanuni,sheria na taratibu? wakuu wa shule wote wanateuliwa kufuata vigezo vilivyo kuwa vitumika toka awali?? watunga mitihani je,wanapatikana kwa utaratibu upi?? wakaguzi ni kweli wana sifa za kuwa wakaguzi kweli???
  Mwisho, mbona hawa polisi hata tukisikia wanasaidia kuwavusha waethiopia na wasomali kwa kuwatoza kitu kidogo bado wanaaminiwa?tunasikia madudu mengi kuwahusu lakini hawajawahi kuwaitia walimu wawaangalie!!! UALIMU NILIO UPENDA KWA MOYO WANGU WOTE,AKILI ZANGU ZOTE NA NGUVU ZANGU ZOTE umepoteza hadhi yake kabisa.nani katufikisha hapo??? Ajabu hao wanao kuja kuwasimamia walimu ukimpata miongoni mwao anaye weza kuandika kwa ufasaha kama mimi miongoni mwao njoo nikupe zawadi.LAKINI NDIO WALIOAMINIWA!!!
  Walimu tuamke turudishe hadhi ya mwalimu na ualimu.
   
 2. Adharusi

  Adharusi JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2012
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 10,635
  Likes Received: 3,017
  Trophy Points: 280
  Ngoja nifuatilie nione...!
  "Vox populi,Vox dei"
   
 3. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #3
  Jul 18, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,953
  Likes Received: 1,279
  Trophy Points: 280
  Na walimu hawaiamini serikali. Ngoma droo!
   
 4. Godfrey Electronics

  Godfrey Electronics JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2012
  Joined: Mar 13, 2012
  Messages: 587
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  serikali inajua kuwa hela wanayolipwa walimu ni ndogo hivyo ni rahis kushawishiwa kufanya chochote iwapo kutakuwa na dau mkuu
   
 5. Mandingo

  Mandingo JF-Expert Member

  #5
  Jul 18, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 3,380
  Likes Received: 317
  Trophy Points: 180
  Ule mgomo wenu hivi ume ishia wapi???
   
 6. harakat

  harakat JF-Expert Member

  #6
  Jul 18, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  hapo umenena mi mwenyewe nimechoka sana
  na hii fani maana kazi kweli kweli hapo
   
 7. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #7
  Jul 18, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Kama humuaminiki mbona mnatumiwa kwenye zoezi la SENSA?

  Kama humuaminiki mbona huwa mnatumia kama maafisa wa NEC kwenye uchaguzi mkuu?
   
Loading...