Kati ya watu 100, watu 75 hukutwa na maambukizi ya UKIMWI

Saratani asilimia ngapi? Hebu nyoosha hiyo sentensi wanaopimima baada ya kuumwa magonjwa mengine km TB homa fungus etc. Au wanaopima kwa hiari toka majumbani? Au wajawazito?

Nimenukuu kulingana na taarifa ya habari ilivyosomwa...
 
Kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Hospitali ya Teule nakanusha taarifa hizo kwa kuwa nilikuwepo katika hafla hiyo na kwa bahati nzuri nimerekodi tukio lote anaye take nimtumie an PM. Inaelekea kuwa yule kijana aliyetumwa na Mngazija kuchukua tukio hile amem quote vibaya mhusika

Nawasilisha
 
ni sawa kwani most ya watu wanokwenda kupima majongwa hayo ni baada ya afya zao kutetereka,ni wachache sana wanaokwenda kwa kupima kwa raha zao,ndio hao 25%
 
leo nilienda Angaza kwa lengo la kucheki afya,maelezo niliyopewa ni kuwa wamezuiliwa kutoa huduma na barua wanazo kutoka wizara ya afya kwakuwa vipimo vimegundulika kuwa feki.
 
Kuna makosa ya kimsingi katika kuripoti hiyo taarifa. Kidunia kiwango cha juu cha HIV prevalenve kwa takwimu za 2011 kiko nchi zifuatazo: Botswana (40%), Swaziland(32% na South Africa (24%). Kwa Tanzania vitongoji vilivyowahi kupata alama za juu ni Ilula wilaya ya Kilolo (30%), Makete (40%) na maeneo ya Tunduma na Mlowo Mbeya. Hiyo 75% ya huko Korogwe/ Tanga ni taarifa mpya kabisa kama ipo.
 
kila watu 100 wanaofika hospitalini hapo,watu 75 hukutwa na maambukizi ya virusi vya UKIMWI na baadhi SARATANI.

Sio asilimia 75 wanamaambukizi bali ni idadi ya wanaofika hosp

kwani tunaposema asilimia hamsini ya wanafunzi wamefeli tunafanya vipi? Si huwa tunachukua 200 kati ya mia nne walofanya mtihani na kutafuta asilimia? Tena wamekwambia kabisa 75 kati ya 100 wanaofika hospitali siyo katika wilaya yote. Naomba katiba ijayo tuweke hesabu liwe somo la lazima kwa kila mwanafunzi anayekwenda kidato cha tano!
 
Back
Top Bottom