aleesha
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 776
- 1,121
Je wazanzibari wananufaika na fursa za bara Au wabara wananufaika na fursa za Wazanzibari?
Kipindi hiki nimeona wabara wakilalamikia sana Wazanzibari mpaka kufikia hatua wanatamani katiba ya Zanzibar ibadilishwe ambayo imekuweko miaka na miaka.
Kwa mfano suala la umiliki wa Ardhi watanganyika hili naona limewachoma sana ambalo suala hili halikuanza jana na juzi.
Kwa upande mwengine asilimia kubwa ya Wazanzibari wanalilia na kulalamika juu ya uhuru wa nchi yao ambayo ni Zanzibar ambapo wanahisi kama nchi imekosa uhuru wake na utambulisho wake kupitia koti la muungano. Kiufupi Wazanzibari wanahitaji mamlaka kamili ya nchi yao.
Kwa upande wa pili wa ndugu zetu wa kitanganyika asilimia kubwa malalamiko yao ni kutaka kuiona Zanzibar ikizidi kudidimia na kuzidi kuwa duni!
Mfano mdogo hapa majuzi tu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar walinufaika na mikopo ambayo ni haki yao ya kikatiba, angalia mitandaoni jinsi Watanganyika walivopiga kelele na kulalamika, na kuanza kumdhikahi Raisi Mama Samia Suluhu Hassan.
Mfano mwengine ni suala la Petrol na Diesel bei kua chini kuliko Tanganyika angalia jinsi gani ndugu zetu povu lilivowatoka hadi kuanzisha mijadala mbali mbali mitandaoni na kwenye vituo vya habari, wasilolijua ni kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefidia lile gap la kupanda kwa bei kwa kulipia kama sijakosea tsh 200 kwa lita.
Kutokana na malalamiko kuwa mengi haswa awamu hii nilitaka kupata majibu kutoka kwenu wanajukwaa hivi ni nani anaenufaika zaidi kati ya Tanganyika na Zanzibar?