Kati ya watanganyika na wazanzibari, Nani wananufaika zaidi na fursa za upande mwingine?

aleesha

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
776
1,121
Je wazanzibari wananufaika na fursa za bara Au wabara wananufaika na fursa za Wazanzibari?

Kipindi hiki nimeona wabara wakilalamikia sana Wazanzibari mpaka kufikia hatua wanatamani katiba ya Zanzibar ibadilishwe ambayo imekuweko miaka na miaka.

Kwa mfano suala la umiliki wa Ardhi watanganyika hili naona limewachoma sana ambalo suala hili halikuanza jana na juzi.

Kwa upande mwengine asilimia kubwa ya Wazanzibari wanalilia na kulalamika juu ya uhuru wa nchi yao ambayo ni Zanzibar ambapo wanahisi kama nchi imekosa uhuru wake na utambulisho wake kupitia koti la muungano. Kiufupi Wazanzibari wanahitaji mamlaka kamili ya nchi yao.

Kwa upande wa pili wa ndugu zetu wa kitanganyika asilimia kubwa malalamiko yao ni kutaka kuiona Zanzibar ikizidi kudidimia na kuzidi kuwa duni!

Mfano mdogo hapa majuzi tu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar walinufaika na mikopo ambayo ni haki yao ya kikatiba, angalia mitandaoni jinsi Watanganyika walivopiga kelele na kulalamika, na kuanza kumdhikahi Raisi Mama Samia Suluhu Hassan.

Mfano mwengine ni suala la Petrol na Diesel bei kua chini kuliko Tanganyika angalia jinsi gani ndugu zetu povu lilivowatoka hadi kuanzisha mijadala mbali mbali mitandaoni na kwenye vituo vya habari, wasilolijua ni kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefidia lile gap la kupanda kwa bei kwa kulipia kama sijakosea tsh 200 kwa lita.

Kutokana na malalamiko kuwa mengi haswa awamu hii nilitaka kupata majibu kutoka kwenu wanajukwaa hivi ni nani anaenufaika zaidi kati ya Tanganyika na Zanzibar?
 
aleesha huu muungano unanufaisha viongozi Sisi wananchi hatuoni faida ya muungano e.g mimi nikienda unguja ardhi sitapewa lakini mpemba akija bara anaruhusiwa kumiliki ardhi kimsingi wao wananufaika huku Sisi wakitufanya manamba wao
 
Nikiangalia wapemba waliojazana rukwa iringa morogoro wakimiliki maelfu ya ekari ila chogo akienda pemba hata kupangishwa nyumba ya biashara anahangaishwa
Muungano unakuwa ni maigizo ya kisiasa na viongozi kushibisha matumbo
 
Wabara mbanufaima zaidi. Ungekuwepo moaka pale mbele ya Chumbe msingepumua Na Tanganyika ni Darisalama siyo Mwannza wala Kigoma
 
Nikiangalia wapemba waliojazana rukwa iringa morogoro wakimiliki maelfu ya ekari ila chogo akienda pemba hata kupangishwa nyumba ya biashara anahangaishwa
Muungano unakuwa ni maigizo ya kisiasa na viongozi kushibisha matumbo
mimi nahisi wabara ni wanufaika zaidi, TRA ipo mpaka Zanzibar ivi umewahi kusikia ZRB iko bara?
 
aleesha huu muungano unanufaisha viongozi Sisi wananchi hatuoni faida ya muungano e.g mimi nikienda unguja ardhi sitapewa lakini mpemba akija bara anaruhusiwa kumiliki ardhi kimsingi wao wananufaika huku Sisi wakitufanya manamba wao
ukubwa wa Tanzania eneo lote ni 945,087 km² ukilinganisha na Zanzibar ni kama Dowa kwenye nguo nyeupe Zanzibar land area was 2,460 sq.km in 2010 -

Sasa wewe mtu na akili zako utoke Bara ujekuai kumiliki Ardhi ZNZ si kulenta mgogoro usiokuwa na haja.
Hebu tafuteni sababu nyingine yenye mashiko.

Ni lazima zanzibar iweke masharti ya Ardhi utokana na udogo wake.

ZANZIBAR
 
Ama na nani ananufaika na Muungano , nahisi Mamlaka ya Zanzibar kuwa madogo ni Mapungufu makubwa sana na tumepunjwa sana kuliko maslahi ya mtu mmoja mmoja kuishi na kufungua biashara kariakoo.
Bakhresa anailipa Tanzania Mabilioni ya kodi kwa mwaka na Kuzalisha Ajira zaidi ya lakimbili kwa Watanganyika , nahisi Bara wanafaidi Zaidi kama Nchi.
Matajiri wengi waZanzibar wameekeza kwenye biashara Huko bara , na ni walipa kodi na kuzalisha Ajira
Bali Wamachinga na wanyamwezi wengi wanafanya kazi za kibarua na uchuuzi Zanzibar na kupata mapato yasiyolipiwa kodi.
SMZ Hainufaiki sana na wamachinga hawa.
Kwa hiyo utaaona Bara wananufaika Zaidi
Ama zile taasisi za Muungano zinazoliingizia Taifa Mabilioni bado hazijatenda haki kuipa zanzibar Quater yake . Hadi hii leo Account ya Pamoja ya Mapato ya Muungano imeshindikana kufunguliwa pamoja na kuwemo ndani ya Katiba kwa zaidi ma Miongo 4 tokea1984. Kwa maana hiyo Zanzibar haipati gawio lake stahiki
 
Kwa jinsi mabilioni yanavyotiririshwa huko Zenji majibu yapo wazi kabisa.
 
Ama na nani ananufaika na Muungano , nahisi Mamlaka ya Zanzibar kuwa madogo ni Mapungufu makubwa sana na tumepunjwa sana kuliko maslahi ya mtu mmoja mmoja kuishi na kufungua biashara kariakoo.
Bakhresa anailipa Tanzania Mabilioni ya kodi kwa mwaka na Kuzalisha Ajira zaidi ya lakimbili kwa Watanganyika , nahisi Bara wanafaidi Zaidi kama Nchi.
Matajiri wengi waZanzibar wameekeza kwenye biashara Huko bara , na ni walipa kodi na kuzalisha Ajira
Bali Wamachinga na wanyamwezi wengi wanafanya kazi za chi zanzibar na kupata mishahara isiyolipiwa kodi.
SMZ Hainufaiki sana na wamachinga hawa.
Na wale omba omba mabarabarani ni kutoka Tanganyika wale ambao hawana faida kila siku wanamiminika huku
 
Na wale omba omba mabarabarani ni kutoka Tanganyika wale ambao hawana faida kila siku wanamiminika huku
Swadakta, na hii inaipa taswira Zanzibar kuwa nikimbilio la watu wa kiwango cha chini, wanyonge wanaohitaji huduma zaidi kuliko kuzalisha na kulipa kodi.
 
Back
Top Bottom