Kati ya wanawake na wanaume nani bora katika usimamizi na ufuatiliaji wa shughuli za umma?

Anna Mghwira

R I P
Mar 9, 2012
206
362
KATI YA WANAWAKE NA WANAUME: NANI BORA KATIKA USIMAMIZI NA UFUATILIAJI WA SHUGHULI ZA UMMA?

Inaonekana kama wanawake wana uwezo mkubwa katika majukumu ya usimamizi wakati wanaume wana uwezo mkubwa katika ufuatiliaji. Tujadili.
 
Shikamoo Mama, ulivyoongea ni sawa lakini wakati mwingine inategemea na nafasi,uwezo, afya ya mwili na akili. Unaweza kuwa unasimamia lakini kama una tatizo la afya ya akili utachemka kwa baadhi ya sehemu.
 
mama , wote wanauwezo sawa wa kusimamia na kufuatilia sema inategemea na mazingira ya kazi ..
 
KATI YA WANAWAKE NA WANAUME: NANI BORA KATIKA USIMAMIZI NA UFUATILIAJI WA SHUGHULI ZA UMMA?

Inaonekana kama wanawake wana uwezo mkubwa katika majukumu ya usimamizi wakati wanaume wana uwezo mkubwa katika ufuatiliaji. Tujadili.
Mimi naona wote sawa tu katika usimamizi
 
KATI YA WANAWAKE NA WANAUME: NANI BORA KATIKA USIMAMIZI NA UFUATILIAJI WA SHUGHULI ZA UMMA?

Inaonekana kama wanawake wana uwezo mkubwa katika majukumu ya usimamizi wakati wanaume wana uwezo mkubwa katika ufuatiliaji. Tujadili.

Mama. Heshima yako.
Kwa sasa utapata majibu ukimaliza Field hapa Moshi.

Unamkumbuka mama mwenzako yaliyomkuta kule Shinyanga?
 
Sasa tunahitaji kuuona ubora wako katika usimamizi wa shughuli za maendeleo katika mkoa wa Kilimanjaro. Usituzingue tafadhali.
 
Mama tunataka Demokrasia, Ubunifu, Kutokuonea watu, Utu, Uadilifu, Uzalendo, Unyenyekevu na hekima Katika kuongoza huo mkoa.
Pia usisahau ulipotoka maana miaka mitatu iliyobaki hadi 2020 ni michache!
 
KATI YA WANAWAKE NA WANAUME: NANI BORA KATIKA USIMAMIZI NA UFUATILIAJI WA SHUGHULI ZA UMMA?

Inaonekana kama wanawake wana uwezo mkubwa katika majukumu ya usimamizi wakati wanaume wana uwezo mkubwa katika ufuatiliaji. Tujadili.

Mama, huu mjadala utakucheleweshea utekelezaji wa ilani ukaishia kukosa vyote
 
huu mkoa wetu mara nyingi viongozi wengi wanauchukulia ni wa upinzani.unatuhakikishia vipi hutatubagua kama wenzako waliotangualia mfano tu juzi msiba wa mzee wetu Ndesa walivyofanya figisu na siasa kwenye mambo ya kijamii kisa tu ni mpinzani
 
Kufuatilia na kusimamia!!Kazi ya kusimamia sio ngumu kama kifuatilia!!
MF kuna mradi wa kusambaza maji sehemu flani katika wilaya x kiongozi yampasa kufuatilia hatua he hatua mpaka wananchi wafaidike na huduma ya maji,kusimamia mradi yawezakua na mambo mawili,baada ya shughuli ya ufuatiliaji kufanikiwa Au kabla ya shughuli ya ufuatiliaji kuanza...mtendaji mkuu hapo ni mfuatiliaji na sio msimamizi!!
 
KATI YA WANAWAKE NA WANAUME: NANI BORA KATIKA USIMAMIZI NA UFUATILIAJI WA SHUGHULI ZA UMMA? Inaonekana kama wanawake wana uwezo mkubwa katika majukumu ya usimamizi wakati wanaume wana uwezo mkubwa katika ufuatiliaji. Tujadili.
Haina jinsia, wote poa au bomu..
 
kusimamia na kufuatilia vinakwenda pamoja...ukiwa msimamizi mzuri utafatilia japo unaweza ukawa unafatilia but huwezi kusimamia. Mfano wewe umefatilia ACT lkn umeshindwa kusimamia mnachokiamini kisa cheo cha kiccm
 
Back
Top Bottom