Kati ya wanasiasa 10 wa kizazi cha leo, ni wangapi wanaoweza kuweka mbele maslahi ya wananchi na ya Taifa kwa ujumla kuliko yao binafsi?

Hakuna narudia hakuna Mwanasiasa yeyote wa aina ya Nyerere kwny upande wa kutoabudu Tumbo
 
Naomba tufanye tathimini isiyo rasimi kupitia mtandao huu wa JamiiForums juu ya namna gani wananchi wanawachukulia wanasiasa wa kizazi cha leo kuwalinganisha na wale wa kiza cha Mwalimu Nyerere, mtu alieacha kazi ya ualimu na kwenda kupigania uhuru wa Taifa hili kazi ambayo kama sikosei, haikuwa na masilahi manono kama ya kuwa mwalimu kwa wakati huo.

Swali:Kati ya wanasiasa kumi tulionao leo hii, ni wanasiasa wangapi walau tunaweza kuwalinganisha na wanasiasa wa kizazi cha mwalimu?

Kwa maneno mengin, ni wanasiasa wangapi kati ya wanasiasa kumi wa leo hii walio tayari kuweka mbele masilahi ya wananchi naTaifa kwa ujumla kuliko masilahi yao binafsi?
Chadema, Bavicha na Bawacha
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom