Kati ya Wanafunzi 7,805 waliofukuzwa UDOM, ni 382 tu ndio wenye sifa

Kansigo

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
2,670
2,000
Waziri wa Elimu nchini Tanzania, Prof. Joyce Lazaro Ndalichako atoa msimamo wa Serikali juu ya wanafunzi waliofukuzwa chuo kikuu cha Dodoma, leo jijini Dar es Salaam, ambapo amesema kuwa kati ya wanafunzi zaidi ya elfu saba waliokuwa wamedahiliwa na kuanza Chuo Kikuu Dodoma ni wanafunzi 382 tu ndio wenye sifa ya kurudi chuoni.

=========================​

Prof.-Ndalichako.jpg


Serikali imetangaza orodha ya wanafunzi ambao watarejea kuendelea na masomo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) baada ya uchambuzi kumalizika na kupatikana idadi ya wanafunzi ambao wana sifa za kuendelea na masomo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako alisema kuwa kwa kipindi chote walikuwa wakifanya uchambuzi ili kuona ni wanafunzi gani walikuwa na sifa za kusoma kozi hiyo maalum ambayo ilianzishwa kutokana na tatizo la walimu wa Sayansi.

Alisema kuwa programu hiyo ilikuwa inahitaji walimu ambao watakwenda kufundisha shule za sekondari lakini kulikuwa na wanafunzi 1,210 ambao walikuwa wanachukua stashahada ya ualimu wa shule za msingi ambao ni kinyume na malengo na 6,595 wakichukua stashahada ya kufundisha shule za sekondari.

“Baada ya hatua ya kuwaondoa wanafunzi chuoni kuchukuliwa, serikali ilifanya uchambuzi wa wanafunzi hao kwa lengo la kujiridhisha na sifa zao. Sifa zilizotakiwa ni ufaulu wa daraja la 1 hadi daraja la 3 na krediti mbili au zaidi katika masomo ya Sayansi na Hisabati,

“Lakini baada ya uchambuzi kufanyika kati ya wanafunzi wanaosomea ualimu wa sekondari 6,595 ni wanafunzi 382 pekee ndiyo wana sifa za kuendelea na masomo yao, 134 ni mwaka wa kwanza na 248 ni mwaka wa pili,” alisema Prof. Ndalichako.

Aidha alisema kuwa wengine 4,586 wa mwaka wa kwanza wa programu maalum wa stashahada ya ualimu wa sekondari waliokidhi vigezo vya ufaulu watahamishiwa katika vyuo vya ualimu vya serikali ambavyo ni Morogoro, Butimba, Mpwapwa, Songea na Tukuyu kuendelea na masomo na wanafunzi 1,337 wa mwaka wa pili watahamishiwa vyuo vya Korogwe na Kasulu ili kumalizia masomo yao.

Pia alisema kuwa serikali itaendelea kuwapatia mikopo wanafunzi watakaoendelea kusoma UDOM na watarejea chuoni mwezi Oktoba mwaka huu, huku wale wa vyuo vya ualimu watakuwa wakilipiwa ada ya 600,000 kwa mwaka ambayo ndiyo ada ya vyuo hivyo na wataripoti chuoni mwezi Septemba.

Kwa upande wa wanafunzi wa kufundisha elimu ya shule ya msingi, Prof. Ndalichako alisema wanafunzi 29 wa mwaka wa pili ambao wana cheti cha daraja A la ualimu watahamishiwa Chuo cha Ualimu Kasulu ili wamalize masomo yao ila tu kwa gharama zao huku wengine 1,181 akiwataka waombe nafasi katika vyuo vingine katika masomo ambayo wana sifa zinazolingana nao.

Aidha katika hatua nyingine, Prof. Ndalichako alisema kuwa migomo iliyokuwa ikitokea chuoni UDOM kwa walimu kugoma kuwafundisha wanafunzi hao yawezekana ilikuwa ikichangiwa na wanafunzi hao kwani uwezo wa chuo cha UDOM ilikuwa ni kupokea wanafunzi 1,180 lakini wakapokea wanafunzi 7,805.

“Walimu kwao mzigo ulikuwa ni mzito wewe utafanya nini?, kwahiyo tukubali kuwa wingi wa wanafunzi ulichangia kutokea mgomo sababu walimu wameajiriwa kufundisha na wengine wa digrii sasa kupokea wanafunzi 7,805 na ilitakiwa 1,180 walikuwa wengi,” alisema Prof. Ndalichako.
 

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,241
2,000
Elimu nchini Tanzania Pof.Joyce Lazaro Ndalichako atoa msimamo wa Serikali juu ya wanafunzi waliofukuzwa chuo kikuu cha Dodoma, leo jijini Dar es Salaam, ambapo amesema kuwa kati ya wanafunzi zaidi ya elfu saba waliokuwa wamedahiliwa na kuanza chuo kikuu dodoma ni wanafunzi 382 tu ndio wenye sifa ya kurudi chuoni.
Ndalichako ametoa hili tamko wapi ndugu? au chanzo chako ni kipi?
 

Yodoki II

JF-Expert Member
Oct 17, 2014
5,415
2,000
Hajainisha aina ya sifa walizokosa hao wengne?Basi NACTE iwaelekeze ZAYONI,DATA STAR &KILIMANJARO INSTITUTE na vyuo vingne.
 

pepsin

JF-Expert Member
Apr 23, 2015
3,408
2,000
Basi serikali iliwarubuni watoto wa watu.
Iwajibike.
Yaani watanzania shida kweli,watoto waibiwe na wahindii wa St.Joseph na wrngine warubuniwe na serikali
 

Emma.

JF-Expert Member
Jun 25, 2012
19,905
2,000
Serikali inatakiwa kuwalipia gharama zao zote hao wanafunzi wenye sifa kuendelea na masomo na huyu aliyehusika kusajili wanafunzi wasiokuwa na sifa anatakiwa kuchukuliwa hatua kali pia kulipa gharama za wanafunzi wote ambao aliwasajili bila kuwa hizo sifa.
 

interlacs

JF-Expert Member
Feb 7, 2012
211
250
What do you mean by wenye sifa? sifa zipi?

Tupia sheria iliyopitishwa na bunge na kusainiwa na prezdaa, kumbuka mfumo wa GPA ulikua umeshaanza kufanya kazi.
Pia hao wanafunzi walijipeleka wenyewe?
 

Wong Fei

JF-Expert Member
Apr 13, 2016
4,096
2,000
Nasubiri Tamko kutoka kwa UKAWA
Mkuu kipind serikali yenu inaanzisha hii programme mlikuwa mefumba macho? Au ulikuwa ni mradi wa mtu?
Kuna wakati huwa najiuliza sipati jibu kbsa.
Hawa wanafunzi mliwatahini nyiny wenyew mkopo mkawapa, na ahadi nono mkawahidi. Halafu leo mnasema wachache ndio wanasifa.
Inakuwaje mnajichanganya kiasi hichi?
Jibu tafadhali
(mm sio mshabiki wa chama chochote na haitatokea nikashabikia chama chochote sbb ni unafiki na ni utumwa wa kifikra)
 

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
48,651
2,000
Mkuu kipind serikali yenu inaanzisha hii programme mlikuwa mefumba macho? Au ulikuwa ni mradi wa mtu?
Kuna wakati huwa najiuliza sipati jibu kbsa.
Hawa wanafunzi mliwatahini nyiny wenyew mkopo mkawapa, na ahadi nono mkawahidi. Halafu leo mnasema wachache ndio wanasifa.
Inakuwaje mnajichanganya kiasi hichi?
Jibu tafadhali
(mm sio mshabiki wa chama chochote na haitatokea nikashabikia chama chochote sbb ni unafiki na ni utumwa wa kifikra)
sasa yamefanyika marekebisho 382 watarudi Udom na wengine watakwenda vyuo vya ualimu vya serikali sasa unataka nini tena?
 

interlacs

JF-Expert Member
Feb 7, 2012
211
250
hivi umeandika nini hapa BAWACHA? UMESOMA YALIYO ANDIKWA?

Ujumbe umefika. Rudia kusoma ile post kisha jibu swali. wewe sini msemaji wa wizara sasa jibu swali. mnawaonea watoto bure kisa, umeshika kisu mkononi. Jana tuliambiwa sheria ni nusu meno. Ikae na upande wawanafunzi, upande wenu mumeshakata sasa mgeukie upande wawanafunzi.
Wamepoteza muda wao bure, wameathirika kisaikologia kwa nini mnacheza na maisha ya watu?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom