Kati ya wamiliki wa Tv Channels na wamiliki wa ving'amuzi, nani anayemlipa mwenzake?

Majan

JF-Expert Member
Jul 2, 2015
1,255
1,783
Habari wakuu,

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, hicho kitu kinanitatiza kwa kweli.

Je, ni mmiliki wa Tv channel ndo anaemlipa mmiliki wa Kinga'muzi ili channel yake ionekane kwene king'amuzi husika au ni Mmiliki wa King'amuzi ndiye anaemlipa Mmiliki wa Tv channel ili nae aweze kuuza king'amuzi chake?
 
Mbona huulizi kuhusu sattelite zinazofanya upate hizo picha..
Duh Apo mkuu unaweza ukaelewesha tu 2pate kujua mana kwauelewa wangu minajua Sattelite hulipii nifree niwewe tu nakifaa chako chakukuwezesha kunasa ayo mawimbi yasattelite mfn dishi au GPS
 
TV channels ndio wanalipa ada kwa wenye ving'amuzi.

I'm not sure sana...ila Startimes ni kama dola 3500 kwa mwezi ili TV channel yako irushwe.
Okee basi kumbe waving'amuzi wanalamba Huku nahuku mana kama Tv Chaneels ndo wanalipa alafu nasisi tena tunawalipa kwa kununua vifurushi..
 
Ni makubaliano yenu mtu wa kingamuzi anamlipa mwenye TV kurusha channel yake maana anatengeneza faida
Mwenye TV ndio analipwa Na wenye decoda coz Mwenye TV tayari anavindi vyake binafsi so kwasababu ya Kuweka wigo wa watazamaji unaweza pia kuwapatia nafasi kwa makubariano ya malipo wenye Decoda
 
Mwenye kingamuzi ndiye anaelipa mwenye tv kulingana na ukubwa wa watazamaji wa tv wenyewe
 
Kwa mujibu wa anayejiita Nabii Suguye, anachanhisha watu pesa kwa ajili ya ya kulipia matangazo ya channel yake. Ni dhahiri kuwa mwenye TV channel ndo analipa wenye ving'amuzi.
 
Ni makubaliano yenu mtu wa kingamuzi anamlipa mwenye TV kurusha channel yake maana anatengeneza faida
Ivi nifaida zipi nyingine anazozitengeneza mwene king'amuzi
Mana minaona kama mwenye Tv channel ndo anatengeneza faida nyingi kupitia matangazo, mwene king'amuzi naona faida yake nipale tunaponunua vifurushi tu.
 
Mmiliki wa Kingamuzi ndo anaemlipa Mmiliki wa Tv channel we hujiulizi Kwanini vin'gamuzi vingi vya bongo havina channel kama supersport,HBO,Fox, n.k hiyo nikutokana na gharama kuwa juu ili kurusha hizo channel..sema kwa hapa bongo nahisi wanafanyiana fea tu...
 
Mwenye Ving'amuzi ndio anaemlipa mwenye Tv Station sababu yeye Mwenye Ving'amuzi anaviuza hivyo Ving'amuzi anapata hela.
Mmiliki wa TV Station analazimika kurusha vipindi viuri ili Station yake ipendwe then Mwenye Ving'amuzi amfuate
 
Okee basi kumbe waving'amuzi wanalamba Huku nahuku mana kama Tv Chaneels ndo wanalipa alafu nasisi tena tunawalipa kwa kununua vifurushi..
Iko hivi,

Hawa wamiliki wa ving'amuzi wananunua haki zote za kurusha matangazo ya TV. TV channels wao wanazalisha na kutengeneza vipindi. Sasa TV channels lazima wauze wanachozalisha. Na ndio wanauza kwa wenye ving'amuzi maana ndio wenye haki ya kurusha matangazo.
 
Mm ninavyojua kwamba decoder ndio wanao walipa wenye tv channel, ila hapa inategemeana na ukubwa wa hicho kituo, leo hii malipo ya Mnet huwezi fananisha na malipo ya Ktv, ndio maaana kuna kitu kinachoitwa bundle.
Na vilevile haya malipo hutegemeana, kwa mfano mtu anaweza anzisha television yake, labda atataka iruke hewani kwa freee hata km bundle limekwisha basi hana mgao wowote kutoka kwa decoder, mm ninavyoelewa tyuuuu
 
TV channels ndio wanalipa ada kwa wenye ving'amuzi.

I'm not sure sana...ila Startimes ni kama dola 3500 kwa mwezi ili TV channel yako irushwe.
Upo kinyume,wenye ving'amuzi ndio wanawalipa wamiliki wa tv station kuonyesha content zao,hao wenye ving'amuzi wanatuuzia sisi,japo wengine wanapewa bure na tv station kwa makubaliano flan flani
 
Upo kinyume,wenye ving'amuzi ndio wanawalipa wamiliki wa tv station kuonyesha content zao,hao wenye ving'amuzi wanatuuzia sisi,japo wengine wanapewa bure na tv station kwa makubaliano flan flani
TV station atarusha vipi content zake wakati hana transmission rights? Ndio maana ya kutoka analogy kwenda digital.

Zamani kila TV station ilikuwa na minara yake ya transmission, sasa hivi TV station wanafanya production tu, transmission wanafanya wa ving'amuzi.
 
Back
Top Bottom