Kati ya Toyota Raum na Toyota Ractis ninunue ipi?

switch Off

Member
Oct 30, 2019
48
186
Wakuu Habari zenu.

Kijana wenu natarajia kununua gari mwishoni mwa mwezi huu. Magari niliyo yapendekeza mpaka sasa ni mawili tu:
- Toyota RAUM
- Toyota RACTIS

Sijawahi kumiliki gari, hii ndio itakuwa mara ya kwanza. Naombeni msaada wenu wa mawazo kwa mnao yafahamu magari vizuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ractis na raum zinatumia engine moja( 1NZ) ingawa kuna Ractis ina matoleo mawili ya engine yaani 1NZ na 2SZ....pia Kwa upande wa body imara Toyota raum iko juu zaidi kuliko Ractis na hata Kwenye spare parts raum iko bei poa zaidi ya Ractis.

Tukija Kwenye upande wa comfortability hasa space ya ndani Ractis ina nafasi ya kutosha kuanzia siti zake za mbele na nyuma Ila kama unataka kumiliki Ractis zaidi ya miaka 5 itakuwa imechoka Sana na utashindwa kuuza Kutokana na body yake tofauti na raum unaweza ukaishi nayo Hadi wajukuu wakaitumia,hivyo angalia mwenyewe moyo wako unapenda nini
 
raum mkuu toyota ractis huwa zinasumbua sana gear box hasa kwenye mfumo wa gia

karibu sana jerry empire tukupatie gari ya ndoto yako kwa gharama nafuu na zenye ubora tupo ilala dar es salaam
0623953036
0659756647

Sent using Jamii Forums mobile app
Ractis,Porte,Passo haya ni Vimeo Ila Kwa muonekano wengi wanaingia mkenge kuyanunua..
Hata Kwenye kuuza lazima utaabike zaidi ya miezi 6 ndipo ufanye biashara tofauti na mnyama raum hii gari ni zaidi ya Ractis mara 50
 
Ractis na raum zinatumia engine moja( 1NZ) ingawa kuna Ractis ina matoleo mawili ya engine yaani 1NZ na 2SZ....pia Kwa upande wa body imara Toyota raum iko juu zaidi kuliko Ractis na hata Kwenye spare parts raum iko bei poa zaidi ya Ractis.

Tukija Kwenye upande wa comfortability hasa space ya ndani Ractis ina nafasi ya kutosha kuanzia siti zake za mbele na nyuma Ila kama unataka kumiliki Ractis zaidi ya miaka 5 itakuwa imechoka Sana na utashindwa kuuza Kutokana na body yake tofauti na raum unaweza ukaishi nayo Hadi wajukuu wakaitumia,hivyo angalia mwenyewe moyo wako unapenda nini

Naongezea kuwa spea zake Raum hazina taabu na ni bei rahisi kuliko Ractis pia mafundi wapo kwani Raum vitu vingi ni vya Corola, na ni gari inafaa kwa safari na kutembelea mjini
 
Ractis na raum zinatumia engine moja( 1NZ) ingawa kuna Ractis ina matoleo mawili ya engine yaani 1NZ na 2SZ....pia Kwa upande wa body imara Toyota raum iko juu zaidi kuliko Ractis na hata Kwenye spare parts raum iko bei poa zaidi ya Ractis.

Tukija Kwenye upande wa comfortability hasa space ya ndani Ractis ina nafasi ya kutosha kuanzia siti zake za mbele na nyuma Ila kama unataka kumiliki Ractis zaidi ya miaka 5 itakuwa imechoka Sana na utashindwa kuuza Kutokana na body yake tofauti na raum unaweza ukaishi nayo Hadi wajukuu wakaitumia,hivyo angalia mwenyewe moyo wako unapenda nini
Hapo kwenye body umedanganya mkuu, gari ni matunzo tu na si vinginevyo, na hakuna tofauti ya material ya body Kati ya raum na ractis zote sawa tu
 
Matunzo ni kitu cha Kwanza Ila Kwa upande wa body raum ni ngumu na sehemu kubwa ya body yake ni bati gumu tofauti na Ractis
 
Hizo gari zote ni nzuri ila inategemea wewe utaipenda ipi..

Ractis mara nyingi huwa na CC 1290 to 1300,ila Raum huwa na Cc 1480 japo zipo chache zenye cc 1300.Hivyo consumption ya mafuta Ractis iko vizuri zaidi ya Raum.

Comfortability zote ziko Bomba kabisa sioni inayomzidi mwenzake.

Raum ina automatic door ambao ni Mwepesi sana kuharibika kama ukivutwa vibaya.

Zote ni ngumu na zinastahimili mazingira mabovu ya barabara zetu.

Ractis ni Push to Start ila Raum unakomaa na funguo..

Raum Spare zake zinapatikana kiurahisi Sana na ukiwa dereva mzuri ni ngumu kuharibika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom