Kati ya Toyota Brevis na IST ipi inaweza kuishi miaka mingi?

Yaani chuma kiko vzr mkuu,kwa reliability iko fresh kabisa ila kua makini wasikushikishe 1JZ-FSE/2JZ-FSE hizo zenye 'D4' maana kuna watu zimewashinda kuzitunza/kimeo wanawasukumia watu wengine kwa bei chee.

Kama ni 1J-GE/2JZ-GE hio fresh tu, ingawa kwa mazingira yetu ya kawaida hio 1JZ-GE cc 2500(ai 250) inatosha kabisa kwa safari/mambio/misele.

Na kua makini sa hivi wajomba wenye brevis cc 3000 hua wanatoa ile label kule nyuma(Ai 300) na kupachika (Ai 250) ili kumdanganya mnunuaji kwamba ni CC 2500.
Card inabaki vipi? Kile kibati cha ndani ya bonnet kwenye body?
 
Hio TX si ni diesel engine mkuu 1KD bila shaka, kuipata 160kph kwa diesel ni shughuli pevu kidogo. Mchanganyo wake sio kama wa Petrol maana ukiipa pedeli ni ndani ya sekunde kadhaa tu unakuwa umegusa 100! Ukikomalia chini unafuta kisahani ndani ya dakika 3 tu.
Mwanzo wa kijazi hadi mwisho wa kijazi huwa namaliza 180.. na pakiwa pazuri natembeaga na hiyo 180 hadi mataa ya kivulini..
 
Unazungumziaje Crown na Brevis
Crown sijawahi kuiendesha, ila, engine yake inaonekana kuwa na pulling zaidi mwanzoni , ila engine ya Brevis ina stamina kubwa zaidi ya kumaintain speed za juu, hivyo after a few seconds, ile crown ambayo ilitangulia kutokana na pulling yake kubwa huwa inapotezwa kirahisi sana
 
Crown sijawahi kuiendesha, ila, engine yake inaonekana kuwa na pulling zaidi mwanzoni , ila engine ya Brevis ina stamina kubwa zaidi ya kumaintain speed za juu, hivyo after a few seconds, ile crown ambayo ilitangulia kutokana na pulling yake kubwa huwa inapotezwa kirahisi sana
Brevis wanazisifia sana wapiga route ndefuu.. nzuri ipi zaidi kati ya ai250 au ai300.. Crown inachanganya faster sana. Kwenye hapa na hapa rahisi kukuacha.. inamaliza 180 haraka, unabaki hauna kazi tena
 
Unamshauri anunue sare ya shule? Seriously?

Kwani anaenda kutafta maks wapi jombaa ? Ni gari inavumilia haswa, kwenye servise vipuri ni vingi na Bei ni nafuu;- , Ni ushauri tu lkn. Zipo nyingi anaweza cheki ingine like subaru forester, Vanguard, Xtrail n.k

Ulaji wa wese / Mafuta hutegemeana na Ukubwa wa gari(CC)

Kama nifogo ajaribu kutafuta ya kipekee duniani.
 
Back
Top Bottom