Kati ya Tandika, Buguruni na Mwananyamala ipi inaongoza kwa kuwa na Masela wa Kutukuka?

Kitunda wanapokaa Wakurya hivi hao Masela wapo kweli?

Ila Kigogo ni nuksi kuna mtu wa kuitwa Mzazi Keiwanga anapiga ngumi balaa, yeye ni mzee kudili na Boxer.

Ukienda Mwananyamala kuna Rama tall nae alitikisa kijiji.

Ukienda Temeke kuna jamaa anaitwa Tom Kidali huyo ni tembo / mbabe wa levo nyingine, bila Doka ( Difenda ) humkamati.

Anyway hivi Damme wa Sinza yuko wapi siku hizi? Muda mrefu hajaingia kwenye anga zetu.
 
Kigogo kuna chafu kibao yaani kule mtoto wa miaka 13 anakushikia panga mchana kweupe vitoto wanakuchukulia dogoli .

Ndio singeli ilipotokea na makundi ya wahuni kibao kaa mbali na kigogo ase kuna vichwa vigumu hatari

Usela wa panya road ndio ulianzia kigogo ukatapakaa sehemu zingine
Embu rudia tena,Singeli ilianzia wapi?

Sent from my Vodafone Smart Tab 3G using JamiiForums mobile app
 
Kitunda wanapokaa Wakurya hivi hao Masela wapo kweli?

Ila Kigogo ni nuksi kuna mtu wa kuitwa Mzazi Keiwanga anapiga ngumi balaa, yeye ni mzee kudili na Boxer.

Ukienda Mwananyamala kuna Rama tall nae alitikisa kijiji.

Ukienda Temeke kuna jamaa anaitwa Tom Kidali huyo ni tembo / mbabe wa levo nyingine, bila Doka ( Difenda ) humkamati.

Anyway hivi Damme wa Sinza yuko wapi siku hizi? Muda mrefu hajaingia kwenye anga zetu.
yupo kajichokea mtu wa mizinga ya bia tu mitaani na club
 
Buguruni 'uswahili' ni nembo tu, ila kumepevuka sana kimaendeleo. Ule ubungulutu wa zamani utatoweka mazima hivi punde, sema miaka 5.
Ni wabuguruni pia?coz umenena kitu ninachokiona kwa sasa ndani ya buguruni yetu,
 
Mkuu usidanganyike, dar ni temeke na tandika yake kwingineko ni ushuani tu. tafuta chumba tmk mtaa wa lang'ata, njaro, mango, double kebin, maputo, kaburi moja, sh/kilakala utapata vyote. loba nje nje, kubakwa na kubaka ni kawaida tu.bange inauzwa sokoni. naamini baada ya mwaka mmoja utaamini kuwa kweli sasa upo dar. Angalizo kwenye maeneo hayo usimwamini jirani, ndugu wa kuzaliwa, sungusungu wala mjumbe, hata baadhi ya wazee kwenye maeneo hayo ni vibaka wastaafu. ukikosa nenda mwananyamala.
Lang'ata na njaro kumetulia sasa hivi,masela walikuwa zamani
 
Napenda sana kuishi maeneo ambayo kuna Masela wengi wa Kutukuka ili nikaishi nao kutoka hapa ninapoishi sasa ambapo kuna Mabishoo na Wanabana pua Watupu ambao Kwangu Mimi naona hawana faida Kwangu zaidi tu ya kila mara kupiga stori za akina Marioo na za akina Diamond na Kiba.

Nimedokezwa na Mtu kuwa ukitaka kufanikiwa haraka sana kimaisha basi jaribu angalau tu kukaa maeneo yenye Masela ( Wahuni / Watoto wa Mjini ) kwani hawa Watu ukiondoa tu hizo tabia zao za Kitukutu ila wana akili nyingi za kuyajua maisha na kuona fursa ya kupambana Kimaisha hivyo nimeshawishika kutaka kuishi nao karibu.

Je kati ya Tandika, Buguruni na Mwananyamala ambako ndiko kuna Masela wengi ni wapi kumezidi kuwa wengi ili leo hii hii nikampe Kazi Dalali anitafutie huko Chumba nihamie huko nami nikatiririke na niserereke nao?

Nawasilisha na nitashukuru nikijibiwa.
Umesahau TANDALE ujue nako masela tupo, sio ushuani huku
 
Kuanzia studio kuja mwananyamala ulizia tolu mbabe.. Uliza wapiga debe wa studio wote hadi mwananyamala watakuleta hadi kwangu.
Ila tu kama una nia ya kuja kuishi na masela huku.

Siku hizi hakuna kukaba watu. Fursa ni kuokota makopo
Poa tolu mbabe tutakuja na Noah kukutafuta.
 
Mnanani alikuwa noma,pale kwao walishauza kwa mama kitunguu sasa hivi shwari halafu yule mama alishakufa.nafikiri sasa hivi mikoroshini bado mateja ndiyo wako na vibaka,Mimi
 
Huijui lang'ata wewe, mnanani alihamia mbagala tangu miaka ya 90, lakini dada zake waliendeleza tabia ya kukaba na kuibiana wao kwa wao. kama nyumba yao haijauzwa bado usalama ni mdogo eneo hilo

Mkuu hii kali kwahiyo kumbe hata Dada zake nao walikuwa Watu wa matukio? Sidhani kama Mgeni aliyekuwa akiwatembelea alikuwa akitoka salama bila kulazimishwa kupata hasara au upotevu wa Mali yake kwa Kuibiwa.
 
Mnanani alikuwa noma,pale kwao walishauza kwa mama kitunguu sasa hivi shwari halafu yule mama alishakufa.nafikiri sasa hivi mikoroshini bado mateja ndiyo wako na vibaka,Mimi
Na pale makaburini kuna mtoto anaitwa Robert na kakayake anaitwa Juma wako wapi maana walinyanyasa sana pale kwa maganga?
 
Back
Top Bottom