Kati ya Songea na Singida ni mkoa upi mzuri kwa mtu anaetaka kuishi na kujishuhurisha na ufugaji na kilimo?

Kajole

JF-Expert Member
Apr 12, 2011
1,667
1,642
Habari wakuu?. Hope tunajiandaa vema na sikukuu ya pasaka pia hongereni kwa mapumziko mareeeefu!.

OK nirudi kwenye kitu kilichonileta hapa kwenu nyie wadau na wataalam wa fani mbalimbali mliopo humu ndo maana hakuna kinachoshindikana ndani ya Jamiiforums. Naombeeni kujuzwa kati ya songea na Singida ni mkoa upi mzuri kwa mtu anaetaka kuishi na kujishuhurisha na UFUGAJI na KILIMO!?.

Hapa tutaangalia na gharama za maisha na huduma za kijamii pia.
KUMBUKA nipo tayar kuishi hata kijijini sana ili mradi nifanikishe lengo langu la kutoka kiuchumi kupitia ufugaji hasa wa UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI .

Asanteni sana na poleni kwa kuwatoa kwenye mada zetu za siasa
 
Lazima ujue aina ya mazao unayotaka kuwekeza na pia ujue aina ya mifugo pia.
Hali ya hewa mfano ukame.
Hali ya chakula kwa ujumla,usiende kufanya uwekezaji mikoa ambayo gharama za chakula ziko juu sahau kutoka.
Usafiri na usafirishaji gharama zake.
Masoko kwa ujumla.
Japo mikoa yote sijaishi naona ungeenda ruvuma huko kuna previlage.
 
Habari wakuu?. Hope tunajiandaa vema na sikukuu ya pasaka pia hongereni kwa mapumziko mareeeefu!.
OK nirudi kwenye kitu kilichonileta hapa kwenu nyie wadau na wataalam wa fani mbalimbali mliopo humu ndo maana hakuna kinachoshindikana ndani ya Jamiiforums. Naombeeni kujuzwa kati ya songea na Singida ni mkoa upi mzuri kwa mtu anaetaka kuishi na kujishuhurisha na UFUGAJI na KILIMO!?.
Hapa tutaangalia na gharama za maisha na huduma za kijamii pia.
KUMBUKA nipo tayar kuishi hata kijijini sana ili mradi nifanikishe lengo langu la kutoka kiuchumi kupitia ufugaji hasa wa UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI .

Asanteni sana na poleni kwa kuwatoa kwenye mada zetu za siasa

Sijui niseme bahati mbaya au nzuri Mkuu kwani Mikoa yote hiyo ' tajwa ' ni ya ' Watani ' zangu wakubwa sana Wangoni na Wanyiramba / Wanyaturu. Kujibu tu swali lako si Ruvuma wala Singida ambako labda unaweza ukatoka Kimaisha. Sana sana huko Ruvuma utatoka tu na zawadi za ' Hirizi ' nyingi na huko Singida unaweza ukatoka tu ni Zawadi za ' Gono ' na ' Kaswende '. Usipoteze muda wako kwenda ' Kuwekeza ' huko tafadhali ila kama kweli unataka ' Kuwekeza ' na kutoka haraka Kimaisha nenda Mikoa ya Mtwara na Mara tu ambako huko kuna ' Fursa ' nyingi na ' Utajiri ' Mkuu. Halafu usisahau hiyo Mikoa Mtwara na Mara ndiyo Mikoa pekee iliyobarikiwa mno hapa Tanzania.

Nasisitiza tena Kwako Mkuu usipoteze muda wako kwenda ama Ruvuma au Singida. Karibu Mtwara na Mara utajirike.
 
Asante sana mkuu,umenipa kitu kipya hivyo kama hutojar naomba unisaidie haya kwa mkoa wa Mtwara!
1. Wilaya ipi nzur kwa UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI. Unaweza kushaur hata kijiji kipi nianzie kwenda kuangalia
2. Kijiji hicho hali ya usafir mpaka mjin ipoje?

Asante
 
  • Thanks
Reactions: rr3
Nenda Singida kwenye ile wilaya ya Dr Mwigulu...huko unaweza kufuga kuku wa kienyeji na kama ni mpenzi wa watoto wazuri basi huko ndio kwenyewe! Mengineyo subiri wadau waongezee, watarudi muda si mrefu kwani nafikiri wameenda kunywa chai.
 
Nenda singida kwenye ile wilaya ya Dr Mwigulu...huko unaweza kufuga kuku wa kienyeji na kama ni mpenzi wa watoto wazuri basi huko ndio kwenyewe! Mengineyo subiri wadau waongezee,, watarudi muda si mrefu kwani nafikiri wameenda kunywa chai.
Asante sana mkuu!. Watoto wazuri hapana boss nazisaka kwanza pesa
 
Sijui niseme bahati mbaya au nzuri Mkuu kwani Mikoa yote hiyo ' tajwa ' ni ya ' Watani ' zangu wakubwa sana Wangoni na Wanyiramba / Wanyaturu. Kujibu tu swali lako si Ruvuma wala Singida ambako labda unaweza ukatoka Kimaisha. Sana sana huko Ruvuma utatoka tu na zawadi za ' Hirizi ' nyingi na huko Singida unaweza ukatoka tu ni Zawadi za ' Gono ' na ' Kaswende '. Usipoteze muda wako kwenda ' Kuwekeza ' huko tafadhali ila kama kweli unataka ' Kuwekeza ' na kutoka haraka Kimaisha nenda Mikoa ya Mtwara na Mara tu ambako huko kuna ' Fursa ' nyingi na ' Utajiri ' Mkuu. Halafu usisahau hiyo Mikoa Mtwara na Mara ndiyo Mikoa pekee iliyobarikiwa mno hapa Tanzania.

Nasisitiza tena Kwako Mkuu usipoteze muda wako kwenda ama Ruvuma au Singida. Karibu Mtwara na Mara utajirike.
Singida unaogopa wanawake, Ruvuma unaogopa wachawi!!!....hizo zote siyo changamoto za kumkimbiza mtu sehem, ni kuonesha namna gani ulivyo weak. Btw mimi nalima Ruvuma, nalima Mbeya, nanext week naenda kuangalia shamba Mgao na Nanhyanga. We endelea kuogopa hirizi
 
Habari wakuu?. Hope tunajiandaa vema na sikukuu ya pasaka pia hongereni kwa mapumziko mareeeefu!.
OK nirudi kwenye kitu kilichonileta hapa kwenu nyie wadau na wataalam wa fani mbalimbali mliopo humu ndo maana hakuna kinachoshindikana ndani ya Jamiiforums. Naombeeni kujuzwa kati ya songea na Singida ni mkoa upi mzuri kwa mtu anaetaka kuishi na kujishuhurisha na UFUGAJI na KILIMO!?.
Hapa tutaangalia na gharama za maisha na huduma za kijamii pia.
KUMBUKA nipo tayar kuishi hata kijijini sana ili mradi nifanikishe lengo langu la kutoka kiuchumi kupitia ufugaji hasa wa UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI .

Asanteni sana na poleni kwa kuwatoa kwenye mada zetu za siasa
Naishi Singida karibu sana kama una lengo la kufuga kuku aisee huku ndio penyewe njoo pm nikupe full data za Singida
 
Singida unaogopa wanawake, Ruvuma unaogopa wachawi!!!....hizo zote siyo changamoto za kumkimbiza mtu sehem, ni kuonesha namna gani ulivyo weak. Btw mimi nalima Ruvuma, nalima Mbeya, nanext week naenda kuangalia shamba Mgao na Nanhyanga. We endelea kuogopa hirizi
Mkuu hebu sema kitu kuhusu Ruvuma!. Naanza wapi na iwe kijijini mkuu
 
Singida kuna kuku wengi wa kienyeji halafu bei rahisi lakini kati ya mkoa wa Singida na Ruvuma kwa kuishi na kufanya shughuli za kilimo ni bora uende Songea. Singida ni kukame sana kuliko Ruvuma.
 
Mkuu hebu sema kitu kuhusu Ruvuma!. Naanza wapi na iwe kijijini mkuu

Sasa hivi barabara zimefunguka uelekeo wote, vijiji vyote ukiwa unatokea barabara ya njombe viko accessible, wilaya ya namtumbo pia barabara ya uelekeo wa mtwara ni lami tupu, koote huko ardhi ina rutba na mvua za kutosha, na wenyeji hawana maneno ukitua popote ulizia ofisi ya mtendaji nenda kajitambulishe eleza lengo lako utasaidiwa bila shida, ardhi ipo ya kutosha.

Kwa vile unaenda vijijini basi ni vizuri kuchukua barua ya utambulisho kutoka huko utokako, na kama ulkuwa mwajiriwa ukaacha kazi beba vitambulisho vyako. Ruvuma zao kuu wanalolima ni mahindi, pia wanalima maharage, kahawa, korosho, karanga, mihogo nk, kifupi ardhi ni inakubali mazao kibao, niwewe tu.

Na kwavile wewe unataka kwenda kuishi hukohuko nakushauri tafuta vijiji ambavyo haviko mbali sana na mji, Maeneo kama Mlilayoyo, Mtangimbole, Shuleyatanga, jirani na barabara kuu na pia huduma za umeme na zingine za kijamii, unaweza kujikuta unafuga samaki pia ambao wanahitajika sana Songea. Kiikubwa tafuta kijiji uhame kwanza mkuu, ukipata hata ekari 10 za jirani kijijini we lipa jenga kajumba kako zungushia uzio anza mambo.
 
Sasa hivi barabara zimefunguka uelekeo wote, vijiji vyote ukiwa unatokea barabara ya njombe viko accessible, wilaya ya namtumbo pia barabara ya uelekeo wa mtwara ni lami tupu, koote huko ardhi ina rutba na mvua za kutosha, na wenyeji hawana maneno ukitua popote ulizia ofisi ya mtendaji nenda kajitambulishe eleza lengo lako utasaidiwa bila shida, ardhi ipo ya kutosha. Kwa vile unaenda vijijini basi ni vizuri kuchukua barua ya utambulisho kutoka huko utokako, na kama ulkuwa mwajiriwa ukaacha kazi beba vitambulisho vyako. Ruvuma zao kuu wanalolima ni mahindi, pia wanalima maharage, kahawa, korosho, karanga, mihogo nk, kifupi ardhi ni inakubali mazao kibao, niwewe tu. Na kwavile wewe unataka kwenda kuishi hukohuko nakushauri tafuta vijiji ambavyo haviko mbali sana na mji, Maeneo kama Mlilayoyo, Mtangimbole, Shuleyatanga, jirani na barabara kuu na pia huduma za umeme na zingine za kijamii, unaweza kujikuta unafuga samaki pia ambao wanahitajika sana Songea. Kiikubwa tafuta kijiji uhame kwanza mkuu, ukipata hata ekari 10 za jirani kijijini we lipa jenga kajumba kako zungushia uzio anza mambo.
Nakuja inbox mkuu kukupa namba yangu tuzungumze zaidi.
 
Asante sana mkuu,umenipa kitu kipya hivyo kama hutojar naomba unisaidie haya kwa mkoa wa Mtwara!
1. Wilaya ipi nzur kwa UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI. Unaweza kushaur hata kijiji kipi nianzie kwenda kuangalia
2. Kijiji hicho hali ya usafir mpaka mjin ipoje?

Asante

Samgwea ' niliwahi kwenda mwaka 1988 kama siyo 1989. Mkoa ambao nimeenda na naenda sana ni wa Mara ( Musoma ) ambako ndiko ' Mshua ' wangu ( Dingi ) anatokea. Na naenda sana Mara ( Musoma ) kwasababu ya Samaki wengi na naogopa kwenda Mtwara kwakuwa Panya ni wengi halafu wametukuka.

Narudia tena kukuomba usipoteze kabisa muda wako kwenda sijui Ruvuma au Singida huko hakuna Kitu halafu Watu wa huko ni ' Washamba / Mambwigira ' sana.ahani Mkuu nimezaliwa Dar japo huko Mtwara ni Nyumbani kwa upande wa ' Bidashi ' wangu ( Mum ) pamoja na Lindi ila sijawahi ' Kukanyaga ' kabisa Mtwara isipokuwa Lindi hasa ' Nachin
 
Samahani Mkuu nimezaliwa Dar japo huko Mtwara ni Nyumbani kwa upande wa ' Bidashi ' wangu ( Mum ) pamoja na Lindi ila sijawahi ' Kukanyaga ' kabisa Mtwara isipokuwa Lindi hasa ' Nachingwea ' niliwahi kwenda mwaka 1988 kama siyo 1989. Mkoa ambao nimeenda na naenda sana ni wa Mara ( Musoma ) ambako ndiko ' Mshua ' wangu ( Dingi ) anatokea. Na naenda sana Mara ( Musoma ) kwasababu ya Samaki wengi na naogopa kwenda Mtwara kwakuwa Panya ni wengi halafu wametukuka. Narudia tena kukuomba usipoteze kabisa muda wako kwenda sijui Ruvuma au Singida huko hakuna Kitu halafu Watu wa huko ni ' Washamba / Mambwigira ' sana.
Asante sana mkuu, nachukua ushauri wako.
 
Back
Top Bottom