Kati ya Songea na Singida ni mkoa upi mzuri kwa mtu anaetaka kuishi na kujishuhurisha na ufugaji na kilimo? | Page 5 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kati ya Songea na Singida ni mkoa upi mzuri kwa mtu anaetaka kuishi na kujishuhurisha na ufugaji na kilimo?

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Kajole, Mar 30, 2018.

 1. Kajole

  Kajole JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2018
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 764
  Trophy Points: 280
  Habari wakuu?. Hope tunajiandaa vema na sikukuu ya pasaka pia hongereni kwa mapumziko mareeeefu!.

  OK nirudi kwenye kitu kilichonileta hapa kwenu nyie wadau na wataalam wa fani mbalimbali mliopo humu ndo maana hakuna kinachoshindikana ndani ya Jamiiforums. Naombeeni kujuzwa kati ya songea na Singida ni mkoa upi mzuri kwa mtu anaetaka kuishi na kujishuhurisha na UFUGAJI na KILIMO!?.

  Hapa tutaangalia na gharama za maisha na huduma za kijamii pia.
  KUMBUKA nipo tayar kuishi hata kijijini sana ili mradi nifanikishe lengo langu la kutoka kiuchumi kupitia ufugaji hasa wa UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI .

  Asanteni sana na poleni kwa kuwatoa kwenye mada zetu za siasa
   
 2. Rene Jr.

  Rene Jr. JF-Expert Member

  #81
  Apr 3, 2018
  Joined: Jan 31, 2014
  Messages: 3,327
  Likes Received: 922
  Trophy Points: 280
  Duh, wewe unalima/unafuga?
  Dar kuna wafugaji wa kuku wa kienyeji, Morogoro, Dodoma kote wapo lakini bado kuku wa Singida anauza sana tu. Broiler wanafugwa sana Dar lakini tunaingiza mpaka kutoka South Africa. Acheni uoga, popote unapoweza kuppata ardhi bei nzuri na uzalishaji gharama chini wewe fanya kazi acha kuogopa.
   
 3. j

  julius milla JF-Expert Member

  #82
  Apr 4, 2018
  Joined: Sep 8, 2017
  Messages: 636
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 80
  Songea ni bora.
   
 4. L

  La Vista14 JF-Expert Member

  #83
  Apr 12, 2018
  Joined: Apr 9, 2017
  Messages: 688
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 80
  Nenda Ruvuma kijana hautojutia kmwe.

  Ardhi cheap.
  Maisha rahis.
  Maji na mvua za uhakika.
  Watu wamelala bado.
  Kilimo ni uhakika.


  Nilishawah ishi kule na singida pia... ila ruvuma ndio the best.
   
 5. donacianm

  donacianm Member

  #84
  Apr 12, 2018
  Joined: Sep 20, 2016
  Messages: 97
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 25
  Singida kuzuri tuwasiliane
   
 6. xav bero

  xav bero JF-Expert Member

  #85
  Apr 12, 2018
  Joined: Nov 24, 2016
  Messages: 4,884
  Likes Received: 6,316
  Trophy Points: 280
  Ukitaka kulima nenda Songea,huku wana mkataba na mvua,haijawah acha kunyesha haswa kilimo cha mahindi,ila ukitaka ufugaj nenda singida,utanunua kuku hata buku mbili,utawekeza ufugaj wako wa mwaka mmoja au miwili then utajuja kutupa mrejesho,,,mikoa hyo imegawanyika sio kwamba singida huwez kulima ila zaid utalima alizeti na songea mahindi ndo nyumban kwao.. Siku songea wataacha kulima miaka miwil mfululizo nahakika dar wataendelea kula chips mayai kila siku..
   
 7. PatriceLumumba

  PatriceLumumba JF-Expert Member

  #86
  Apr 12, 2018
  Joined: Mar 9, 2016
  Messages: 399
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 80
  HABARI,
  "Kajole,
  Natumaini pasaka ilipita vema kwako na kwa wapendwa wote nadahni sijachelewa kukutoa ushauri wangu juu ya swali lako,
  Mimi nadhani singida ni mahala sahihi sana kwa vigezo kadhaa nitakavyo vitaa.
  1.Kwakilimo na ufugaji ni eneo karibu na masoko makubwa kama mkoa wa dar na arusha hata nairobi.
  2.Usafiri ni rahisi kwani kuna njia kuu magari mengi hupita yakiwa hayana mzigo kwenda kwenye masoko.
  3.Ni eneo linalofaa kwa kilimo ha umwagiliaji

  Nitaongeza mengine baadae tafadhali.

  LUMUMBA
   
 8. kalagabaho

  kalagabaho JF-Expert Member

  #87
  Apr 13, 2018
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,649
  Likes Received: 2,605
  Trophy Points: 280
  Kama umechukua ushauri huu basi sio mzima wewe
   
 9. G'taxi

  G'taxi JF-Expert Member

  #88
  Apr 13, 2018
  Joined: Sep 15, 2013
  Messages: 3,187
  Likes Received: 2,600
  Trophy Points: 280
  Unamdanganya wazi wazi..Mara imebarikiwa na nini?sisi wa Mwanza hapa tunaijua Mara mwanzo mwisho na ndiyo tunaihudumia pakubwa kimahitaji.yaani Mara ikawe mkoa uliobarikiwa kwa kipi.sana sana ungemwambia aje hapa Mwanza,aende Bukoba,aende Manyara au hata huko kaskazini kote.maeneo anayoweza kufuga na kulima pia.najua Mara inawafugaji lakini si kwa kumshauli kwamba Mara ndiyo zaidi ya Singida.bado hapo hapo Singida anaweza kutusua maisha kwa kilimo biashara.sema wewe utakua mjita au mkurya ama akabila ya mkoa wa Mara ndiyo maana unaweza dhani kwenu ni zaidi tu kuliko Singida

  JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
   
 10. jombezi

  jombezi Member

  #89
  Apr 15, 2018
  Joined: Jun 30, 2017
  Messages: 24
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 5
  Mkuu uko timamu sana kichwani,hongera
   
 11. A

  Ayatolaalikhaminey Member

  #90
  Apr 19, 2018
  Joined: Apr 16, 2018
  Messages: 20
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 15
  Kwa Singida utategemea kilimo cha mvua sana sana,ila utalima Alizeti hiyo ni simple sana,Nenda Singida Vijijini has kule pembeni kabisa karibu na Wilaya ya Hanang (mf.Kijiji kimoja kinaitwa Ngamu saa mbili hadi Singida town) ardhi iko na rutuba. Utaanza kukaa kijiweni kuna umeme utakodisha nyumba elf 15-30 kuna umeme,na huduma zingine za kijamii zipo.

  Utakodisha sijui ni eka ngapi lakini ni vizuri ukaanza na eka 10-20. Bei yake ni rafiki kuanzia kukodisha hadi kulima
  Mfano wa mchanganuo wa eka 10 katika alizeti.
  Kukodisha ni elf 50-100 inategemeana na majira na anayekodisha ana changamoto kiasi gani ,Tufanye wastan elf 80/eka
  so
  Kukodisha
  Tsh 8,0000 x eka 10=800,000. Kukodisha ,bei iko very flexible itategemeana na wewe.
  Tsh 40,000x 10=400,000 hapa ni Kulima kwa ajjili ya kuweka mbegu/Kupanda.hiyo ni bei ya trekta ya ng'ombe ni elf 30.
  Tsh 5,000 x 10=50,000 hiyo ni mbegu ya kienyeji nyeupe( sisi tunaita serena) inatoa ukiamua kukamua mafuta.
  Tsh 30,000x10=300,000 hii ni palizi kumbuka alizeti ina palizi moja tu.
  Tsh 5,000x10=50,000 hapa ni kukata kwa ajili ya kupiga piga
  Tsh 20,000x1= 20,000 kukusanya toka shambani hadi sehem utakayo pigapiga.(sisi tunaita kupura) kwa eka zote.
  Tsh 20,000x1 =20,000 kupiga(Kupura) na kupepeta-kwanza hapa we fanya hiyo kazi ni rahisi sana.
  Tsh 5,000x1 =5,000 Uzi wa kushonea pamoja na Sindano
  Tsh 600x 120(idadi ya gunia) =72,000 hii ni mifuko ya kuhifadhia.Japo ukipata safari ya Arusha utapata kwa tsh 300.
  Tsh tufanye 50000 kodisha sehem ya kuhifadhia,japo unaweza kuhifadhi bure au ukaweka hapo nje ka nyumba ina geti.
  Jumla kuu =(1,767,000) au

  Eka moja inatoa kati ya gunia 10-15. Lets make 12/eka=120 Kuuza hadi kufikia December bei yake ni hadi elf 75.Lakini we uza kwa mwezi wa 9 ili ujiandae kukodisha tena bei ni kati ya elf 50-55 .Uza kwa elf 50

  Mauzo
  Idadi bei@ Jumla kuu
  120x 50,000 =6,000,000
  Mauzo-Gharama = Faida
  6,000,000 - 1,767,000 =4,233,000

  Sasa rudi tena shambani kafanye eka 30.Mavuno yake ukakamue mafuta,utauza mafuta,mashudu,na mafuta ghafi-ingawa hayana bei sana haya crude oil.

  Pia kuna watu wanauza mimea ikiwa shambani,amepanda amepalilia afu mnafanya tathimini unanunua,Wakulima wengine wanauza gunia kwa elf 25 ikiwa shambani akivuna anakulipa(Sisi tunaita tunatoa advance)


  Mengine unaweza kulima vitunguu ila ukishakuwa mwenyeji hapa ndio patamu zaidi,japo risk ni kubwa sana,ila ukifanikiwa baasi,Utalima mahindi pia.

  Risks zake zaweza kuwa,ni mda mrefu tangu umepanda hadi kuvuna, Kukodishiwa eka 1 watu wawili-Hapa dawa yake ni mfanye kwa maandishi,Wadada wazuri na watajitaidi kwa kila namna akumiliki ata kwa kutumia miundo mbinu-Ila itakuwa ni uzembe wako,Mvua kuchelewa n.k

  Ufugaji wa kuku ,tutafuga chotara,kwa vile wanakuwa haraka,pia watu wa huku hawapendi wa kisasa wanaamini huwa wanakuzwa kwa dawa,wanaume wakila wanaota matiti.

  Mchanganuo wake tutafanya siku tukionana kijijini.
   
 12. zacha

  zacha JF-Expert Member

  #91
  Apr 19, 2018
  Joined: Feb 28, 2009
  Messages: 687
  Likes Received: 382
  Trophy Points: 80
  Nimekuelewa sana mkuu...!

  Changamoto zipi zilizopo maeneo haya ambazo tunaweza zigeuza kuwa fursa?

  Technolojia ya kiafrika ikoje maeneo haya hasa kwa mgeni ambaye hafahamiki kwa wenyeji?

  Vitu gani vya kujiepusha navyo hasa ukifika kijijini hapo?!
   
 13. zacha

  zacha JF-Expert Member

  #92
  Apr 19, 2018
  Joined: Feb 28, 2009
  Messages: 687
  Likes Received: 382
  Trophy Points: 80
  Na haya mafuriko atafugaje mkuu?!
   
 14. A

  Ayatolaalikhaminey Member

  #93
  Apr 19, 2018
  Joined: Apr 16, 2018
  Messages: 20
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 15
  Mf. hapo kumechangamka sana,watumishi wa serikali wamekuwa wengi,watu wengi pia wamekopa benki lakini huduma za kifedha ni hafifu mara nyingi hadi Uende town-We unaweza ukawa NMB wakala,Ukaweka na mpesa,tigo pesa pia utawasaidia sana. Pia wengi wanafyatua tofali za block kwa mkono we unaweza ukaweka ile ya kufyatua kwa umeme,ukaongeza na pavement zile za kuweka chini-watakufrahia,Kingine ni mbegu za mahindi -we fanya kitu kimoja leta mbegu nadhani ni kilo 8 kwa eka 1,unawakopesha akivuna anakupa gunia 1 kwa kila eka 1-hutajuta lakini muandikishane,frusa zipo nyingi.

  Teknolojia ya kiafrika ipo ila hawanaga mda kaaabisa na mtu mgeni,wanapenda wageni wanaamini kwa mtu mgeni hasa wa kimaendeleo akija ndio mji unakua,vinginevyo we ukawatibue tu.Pia ujitaidi kuwa mtu wa watu be simple.Shiriki katika matukio ya kijamii hasa changamoto,kwenye sherehe sio lazima ukienda ukae hadi iishe we pitia onekana kidogo sepa zako.

  Vitu vya kuangalia,huku kijijini watu wote ni ndugu kwa hiyo usigombane na mtu bila sababu za msingi hata kama we unajua sheria huko utawashinda ila watakushughulikia tu,pia issue zote za kimahusiano hapo kijijini usiingie kwa haraka zitakuletea shida.Usiwe mlevi sana kama unakunywa just piga ile ya kukata kiu unawasha bodaboda unaenda kuangalia mashamba yako,pia fasheni zisizo na afya mf.unavaa macheni makubwa,mara nywele umeweka sijui nini zimekuwa nyekundu,hapo wataona huyu atatuharibia vijana tu,jaribu kufanana nao japo kwa mbali.

  Welcome kijijini aisee.
   
 15. xav bero

  xav bero JF-Expert Member

  #94
  Apr 19, 2018
  Joined: Nov 24, 2016
  Messages: 4,884
  Likes Received: 6,316
  Trophy Points: 280
  Asiulize swali kwa mchanganuo huu tena
   
 16. Chiwa

  Chiwa JF-Expert Member

  #95
  Apr 19, 2018
  Joined: Apr 17, 2008
  Messages: 1,882
  Likes Received: 1,236
  Trophy Points: 280
  ningekushauri uanzie singida kwa kuwa ni karibu na pia kuna soko jipya la kukulinaongezeka litakalotokana na mji mkuu wa kiutendaji wa serikali kuamia dodoma hivyo kutakuwa na ongezeko la wateja wa kuku na hasa ukizingatia watu wa dar wengi wanapenda eti kukimbia nyama nyekundu. lakini pia singida nayenyewe inakuwa, kama ilivyongezeka mkoa wa Pwani kwa kibaha na chalinze ndivyo mji wa singida utakavyoongezeka kwa ajili ya dodoma.
  changaomoto iliyokuwepo ni kwamba eneo hili halina mvua nyingi kama songea lakini mazao yake yanadhamani sana kuliko songea kwa kuwa kilimo cha huku hakitumii sana mbolea za viwandani. pia faida nyingine mkoa huu kuna wakazi wengi wanajishughulisha ufugaji wa kuku maeneo kama sanjaranda ni mazuri kwako kuna virgin land mbayo haijaguswa sehemu kubwa kwa kilimo na pia kuna wafugaji wazuri wa kuku pia kilimo kinawezekana.
  songea sikujui sana lakini uhakika wa mvua na kuendesha kilimo kunaweza kuwa rahisi zaidi japo changamoto la soko ni jambo lingine mahindi yao sio mazuri sana kwa kuwa wakulima wengi wanatumia mbolea ya viwandani na ndo maana debe la mahindi songea linaweza shuka mpaka 2500/- lakini singida na dodoma litaishia 8000/-. kama dini haikuzuii songea ni kuzuri kwa ufugaji wa nguruwe kwa kuwa uhakika wa maji na chakula ni mkubwa sana.
   
 17. Hornet

  Hornet JF-Expert Member

  #96
  Apr 19, 2018
  Joined: Apr 29, 2013
  Messages: 12,705
  Likes Received: 8,186
  Trophy Points: 280
  Nimekaa singida
  Ppp0p,,p,cUkiingia ike
   
 18. MAPUMA MIYOGA

  MAPUMA MIYOGA JF-Expert Member

  #97
  Apr 19, 2018
  Joined: Jan 30, 2013
  Messages: 3,235
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  Karibu Singida mkuu, achana na habari za Gono sijui na nini na nini ni za wale walioshindwa. Naishi Iramba na nalima mazao yanatoka vema kabisa.
  Hakuna shida ya kuwaza utafikishaje mazao sokoni kwani usafiri ni 24/7 iwe masika iwe kiangazi.
   
 19. stephot

  stephot JF-Expert Member

  #98
  Apr 19, 2018
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 5,974
  Likes Received: 3,686
  Trophy Points: 280
  Singida..
   
 20. MAPUMA MIYOGA

  MAPUMA MIYOGA JF-Expert Member

  #99
  Apr 19, 2018
  Joined: Jan 30, 2013
  Messages: 3,235
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  UKO VIZURI MKUU, MI NIKO KINAMPANDA- IRAMBA, NILIANZA MWAKA JANA. HIVI SASA NAELEKEA KUVUNA. JAPO NILIANZA NA ENEO DOGO NA NINATEGEMEA KUONGEZA WIGO MWAKA HUU NA KUENDELEA POLE POLE.
   
 21. miminimkulimaakachekasana

  miminimkulimaakachekasana JF-Expert Member

  #100
  Jul 11, 2018
  Joined: May 29, 2017
  Messages: 458
  Likes Received: 668
  Trophy Points: 180
  DAH MKUU ULIPATA ENEO KWA SHILINGI NGAPI
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...