Kati ya Songea na Singida ni mkoa upi mzuri kwa mtu anaetaka kuishi na kujishuhurisha na ufugaji na kilimo? | Page 4 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kati ya Songea na Singida ni mkoa upi mzuri kwa mtu anaetaka kuishi na kujishuhurisha na ufugaji na kilimo?

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Kajole, Mar 30, 2018.

 1. Kajole

  Kajole JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2018
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 766
  Trophy Points: 280
  Habari wakuu?. Hope tunajiandaa vema na sikukuu ya pasaka pia hongereni kwa mapumziko mareeeefu!.

  OK nirudi kwenye kitu kilichonileta hapa kwenu nyie wadau na wataalam wa fani mbalimbali mliopo humu ndo maana hakuna kinachoshindikana ndani ya Jamiiforums. Naombeeni kujuzwa kati ya songea na Singida ni mkoa upi mzuri kwa mtu anaetaka kuishi na kujishuhurisha na UFUGAJI na KILIMO!?.

  Hapa tutaangalia na gharama za maisha na huduma za kijamii pia.
  KUMBUKA nipo tayar kuishi hata kijijini sana ili mradi nifanikishe lengo langu la kutoka kiuchumi kupitia ufugaji hasa wa UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI .

  Asanteni sana na poleni kwa kuwatoa kwenye mada zetu za siasa
   
 2. msumeno

  msumeno JF-Expert Member

  #61
  Apr 3, 2018
  Joined: Aug 3, 2009
  Messages: 2,842
  Likes Received: 936
  Trophy Points: 280
  Mkuu Kilimo Singida hapana, mvua za kule shida, while Songea inaweza kua nzuri kwa vyote though ni mbali na soko ( DAR) ila kama mshabiki wa Yanga Singida sio pazuri sana ( last point ni jok)
   
 3. dumejm

  dumejm JF-Expert Member

  #62
  Apr 3, 2018
  Joined: Feb 18, 2016
  Messages: 512
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 60
  duuuh unapotosha watu boss... Hivi mtwara kuna nini
   
 4. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #63
  Apr 3, 2018
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 9,424
  Likes Received: 2,934
  Trophy Points: 280
  Ruvuma mbona panafikika kiurahisi kila siku Fuso zinapishana usiku na barabara ni nzuri kabisa tena nadhani wao kwa upande wa miundombinu walianza kitambo kuw na lami hivyo hata issue ya usafirishaji wa bidhaa wapo vizuri (FUSO kila siku usiku zinapishana)
   
 5. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #64
  Apr 3, 2018
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 9,424
  Likes Received: 2,934
  Trophy Points: 280
  Njoo na alizeti kama upo Singida mkuu najua utapata lifta
   
 6. Rene Jr.

  Rene Jr. JF-Expert Member

  #65
  Apr 3, 2018
  Joined: Jan 31, 2014
  Messages: 3,327
  Likes Received: 922
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu nilichogundua humu watu wengi wanaongea kwa kutumia uzoefu wa kwenye keyboard. Ukimuuliza kwanini unashauri akafugie Singida sjuwi atakujibu kule wafugaji wa kuku wa kienyeji ni wengi, then wakiwa wengi wewe ina faida gani kwako?!
   
 7. R

  Roy kimei JF-Expert Member

  #66
  Apr 3, 2018
  Joined: Aug 10, 2017
  Messages: 297
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 60
  Singida ni jangwa, hakunafursa yoyote, am nimesahaukitu Ukitaka kuliwazwa kisawasa nenda singida. wanawake wa kisingida apana mchezo Tanga inasubiria.
   
 8. stephanoadolph

  stephanoadolph Member

  #67
  Apr 3, 2018
  Joined: Jun 22, 2016
  Messages: 83
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 25
  mkuu kwenye mtwara naunga mkono hasa ukizingatia una taka kufuga kuku..mkoa wa mtwara wilaya ya masasi biashara ya kuku wa kienyeji na mayai yake ni dili sana mkuu.kuna kipindi kuku anafika 30 elfu mmoja..mayai ya kienyeji ni buku moja yakishuka sana ni 700
   
 9. avogadro

  avogadro JF-Expert Member

  #68
  Apr 3, 2018
  Joined: Apr 30, 2013
  Messages: 2,518
  Likes Received: 2,231
  Trophy Points: 280
  usiongee kishabiki ukawapotosha watu wasiojua jografia ya MUSOMA. Kwanza upatikanaji wa ardhi utaipata wapi? ardhi kule kama Kilimanjaro na Kagera ambapo inamilikiwa kiukoo kuuza ni marufuku. La pili kuna usalama gani? utalima gunia mbili tu za maindi MKURYA (baba zako wadogo) wanakuja usiku kukucharanga na mapanga mwili mzima au kukutifuatifua na bunduki wanabeba kila kitu mpaka panya. Musoma hapafaiiiiii!!! kwa uwekezaji wenyeji wa kule wakifanikiwa kuiba mgodini huko hawawekezi kwao wanakwenda kujenga Mwanza sembuse mgeni!!! ma woya!!!!???
   
 10. impongo

  impongo JF-Expert Member

  #69
  Apr 3, 2018
  Joined: Feb 18, 2015
  Messages: 4,097
  Likes Received: 2,158
  Trophy Points: 280
  Singida kwa ufugaji na kilimo ni afadhari maana kuna uhakika wa kuuza unachokizalisha usafiri ni wa uhakika tofauti na Ruvuma ambako mtu anavuna gunia 50 za mahindi na anaendelea kuwa masikini asiyejiweza.
   
 11. impongo

  impongo JF-Expert Member

  #70
  Apr 3, 2018
  Joined: Feb 18, 2015
  Messages: 4,097
  Likes Received: 2,158
  Trophy Points: 280
  Singida ni pazuri na kuna usafiri wa uhakika nenda manyoni au itigi kuna fursa nyingi kilimo cha Alzeti, choroko, Ufuta Dengu mahindi Ngano Soya niwewe kuamua.
   
 12. impongo

  impongo JF-Expert Member

  #71
  Apr 3, 2018
  Joined: Feb 18, 2015
  Messages: 4,097
  Likes Received: 2,158
  Trophy Points: 280
  Hata ufugaji wa kuku kwa singida hauna shaka kuku wanakua vyema
   
 13. impongo

  impongo JF-Expert Member

  #72
  Apr 3, 2018
  Joined: Feb 18, 2015
  Messages: 4,097
  Likes Received: 2,158
  Trophy Points: 280
  Bora hata Mtwara huko Msoma hakufai kabisa mijamaa mikatili sana
   
 14. Rene Jr.

  Rene Jr. JF-Expert Member

  #73
  Apr 3, 2018
  Joined: Jan 31, 2014
  Messages: 3,327
  Likes Received: 922
  Trophy Points: 280

  Hahahahaa, safi mkuu. Mara ya kwanza kabisa kwenda mkoa wa ruvuma aliniita jamaa yangu mmoja Mkinga (very successfull) wa kutokea njombe kwa sababu ya kazi moja maalum, nilipofika nikakutana na wazee wengine wawili ambao nafahamiana nao vizuri sana kupitia kwa mzee wangu, wote waliwahi kufanya kazi na mzee wangu huko serikalini na walikuwa kama family friends (angalizo; sijawahi kufanya kazi serikalini, wala kazi ya kuajiriwa popote), hao wote siyo kwao mkuo huo...lakini wamezamia. Kukatisha story ni kwamba, baada ya kumaliza tu project ile ilonipeleka nilijikuta nina ekari zaidi ya miambili za mashamba, yule jamaa akawa ananitania "tayaaari", kila mara ananiambia "tayariii", nikikutana na wazee wangu nao "tayaariii". Nikuibie siri, sehem yoyote ambayo watu wamelala fofofo kuna oportunities nyingi sana kwa wajanja, sehem zooote zenye migogoro wajanja ndiyo hupatia pesa. Ingia kariakoo, wakinga wooote wamechukua mitaji huko unakosema watu wasiende. Haya ni mawazo tu mkuu, huenda yasikufae sana wewe waofisini, lakini washambani kama mimi yatamfaa.
   
 15. Thad

  Thad JF-Expert Member

  #74
  Apr 3, 2018
  Joined: Mar 14, 2017
  Messages: 6,441
  Likes Received: 13,409
  Trophy Points: 280
  Sio lazima uzalishie sokoni, anaweza akazalishia Singida akauza Zanzibar.
  Nakuunga mkono kwa hoja ya kufugia Ruvuma kwa sababu ya upatikanaji wa chakula cha mifugo yake.
   
 16. ChoiceVariable

  ChoiceVariable JF-Expert Member

  #75
  Apr 3, 2018
  Joined: May 23, 2017
  Messages: 1,500
  Likes Received: 960
  Trophy Points: 280
  Mwambie ahamie kama ni dili
   
 17. ChoiceVariable

  ChoiceVariable JF-Expert Member

  #76
  Apr 3, 2018
  Joined: May 23, 2017
  Messages: 1,500
  Likes Received: 960
  Trophy Points: 280
  Uhakika wa soko la mazao kati ya dar na songea wapi ni uhakika?
  Mkulima au mfugaji wa morogoro au singida wakienda kuuza zao aina moja nani atakuwa kwenye disadvantage zaidi?
   
 18. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #77
  Apr 3, 2018
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 7,953
  Likes Received: 4,090
  Trophy Points: 280
  Utatuwekea hapa matokeo yake mkuu na sisi tujisomee!
   
 19. Musa Ezekiel

  Musa Ezekiel New Member

  #78
  Apr 3, 2018
  Joined: Jul 19, 2015
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Songea
   
 20. DR. MWAKABANJE

  DR. MWAKABANJE JF-Expert Member

  #79
  Apr 3, 2018
  Joined: Nov 7, 2012
  Messages: 1,739
  Likes Received: 2,463
  Trophy Points: 280
  Watu wengi wanajibu kwa kuisikia hiyo mikoa lakini si kwa kufanya utafiti wa ulichokiuliza!

  Jibu langu, ingia Ruvuma: sababu
  Mvua za kutosha
  Ardhi ya kutosha bei karibu na bure.
  Chakula cha mifugo kama Pumba na mashudu bei chini, hivi sasa pumba unapata kwa 1000tshs debe.
  Maji yanapatikana kwa urahisi
  Usafiri upo wa ndani na nje ya mkoa hivi sasa barabara ya kuunganisha mtwara ipo tayari hivyo uhakika wa soko kwani mtwara na hata Lindi zinategea chakula toka Ruvuma..changamoto zingine ni kawaida.
   
 21. darubin

  darubin JF-Expert Member

  #80
  Apr 3, 2018
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,084
  Likes Received: 694
  Trophy Points: 280
  watu wengi hapa wanashauri kiushabiki na kila mmoja anavutia kwao, wa singida atakuambia njoo huku na wa ruvuma vilevile. fanya analysisi tu vizuri mkuu,mi naamini si Ruvuma wala singida popote unatoboa ila dhamira yako ndio itakayokuongoza. Tanzania hii popote utakapoenda kuna matajiri wanaoheshimika na kuna majumba mazuri tu.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...