Kati ya Songea na Singida ni mkoa upi mzuri kwa mtu anaetaka kuishi na kujishuhurisha na ufugaji na kilimo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kati ya Songea na Singida ni mkoa upi mzuri kwa mtu anaetaka kuishi na kujishuhurisha na ufugaji na kilimo?

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Kajole, Mar 30, 2018.

 1. Kajole

  Kajole JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2018
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Habari wakuu?. Hope tunajiandaa vema na sikukuu ya pasaka pia hongereni kwa mapumziko mareeeefu!.

  OK nirudi kwenye kitu kilichonileta hapa kwenu nyie wadau na wataalam wa fani mbalimbali mliopo humu ndo maana hakuna kinachoshindikana ndani ya Jamiiforums. Naombeeni kujuzwa kati ya songea na Singida ni mkoa upi mzuri kwa mtu anaetaka kuishi na kujishuhurisha na UFUGAJI na KILIMO!?.

  Hapa tutaangalia na gharama za maisha na huduma za kijamii pia.
  KUMBUKA nipo tayar kuishi hata kijijini sana ili mradi nifanikishe lengo langu la kutoka kiuchumi kupitia ufugaji hasa wa UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI .

  Asanteni sana na poleni kwa kuwatoa kwenye mada zetu za siasa
   
 2. Mwifwa

  Mwifwa JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2018
  Joined: Apr 3, 2017
  Messages: 25,348
  Likes Received: 64,554
  Trophy Points: 280
  Anzia hapa kwanza.

  Jee mvua katika hiyo mikoa ikoje, utofauti wake uko vipi?
   
 3. MLA PANYA SWANGA

  MLA PANYA SWANGA JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2018
  Joined: Jul 31, 2015
  Messages: 2,992
  Likes Received: 3,011
  Trophy Points: 280
  Lazima ujue aina ya mazao unayotaka kuwekeza na pia ujue aina ya mifugo pia.
  Hali ya hewa mfano ukame.
  Hali ya chakula kwa ujumla,usiende kufanya uwekezaji mikoa ambayo gharama za chakula ziko juu sahau kutoka.
  Usafiri na usafirishaji gharama zake.
  Masoko kwa ujumla.
  Japo mikoa yote sijaishi naona ungeenda ruvuma huko kuna previlage.
   
 4. GENTAMYCINE

  GENTAMYCINE JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2018
  Joined: Jul 13, 2013
  Messages: 27,704
  Likes Received: 31,872
  Trophy Points: 280
  Sijui niseme bahati mbaya au nzuri Mkuu kwani Mikoa yote hiyo ' tajwa ' ni ya ' Watani ' zangu wakubwa sana Wangoni na Wanyiramba / Wanyaturu. Kujibu tu swali lako si Ruvuma wala Singida ambako labda unaweza ukatoka Kimaisha. Sana sana huko Ruvuma utatoka tu na zawadi za ' Hirizi ' nyingi na huko Singida unaweza ukatoka tu ni Zawadi za ' Gono ' na ' Kaswende '. Usipoteze muda wako kwenda ' Kuwekeza ' huko tafadhali ila kama kweli unataka ' Kuwekeza ' na kutoka haraka Kimaisha nenda Mikoa ya Mtwara na Mara tu ambako huko kuna ' Fursa ' nyingi na ' Utajiri ' Mkuu. Halafu usisahau hiyo Mikoa Mtwara na Mara ndiyo Mikoa pekee iliyobarikiwa mno hapa Tanzania.

  Nasisitiza tena Kwako Mkuu usipoteze muda wako kwenda ama Ruvuma au Singida. Karibu Mtwara na Mara utajirike.
   
 5. Kajole

  Kajole JF-Expert Member

  #5
  Mar 30, 2018
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Asante sana mkuu,umenipa kitu kipya hivyo kama hutojar naomba unisaidie haya kwa mkoa wa Mtwara!
  1. Wilaya ipi nzur kwa UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI. Unaweza kushaur hata kijiji kipi nianzie kwenda kuangalia
  2. Kijiji hicho hali ya usafir mpaka mjin ipoje?

  Asante
   
 6. mkulu senkondo

  mkulu senkondo JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2018
  Joined: Feb 19, 2017
  Messages: 701
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 180
  Nenda singida kwenye ile wilaya ya Dr Mwigulu...huko unaweza kufuga kuku wa kienyeji na kama ni mpenzi wa watoto wazuri basi huko ndio kwenyewe! Mengineyo subiri wadau waongezee,, watarudi muda si mrefu kwani nafikiri wameenda kunywa chai.
   
 7. Kajole

  Kajole JF-Expert Member

  #7
  Mar 30, 2018
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Asante sana mkuu!. Watoto wazur hapana boss nazisaka kwanza pesa
   
 8. mkulu senkondo

  mkulu senkondo JF-Expert Member

  #8
  Mar 30, 2018
  Joined: Feb 19, 2017
  Messages: 701
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 180
  OK ni vizuri pia...
   
 9. Rene Jr.

  Rene Jr. JF-Expert Member

  #9
  Mar 30, 2018
  Joined: Jan 31, 2014
  Messages: 3,327
  Likes Received: 922
  Trophy Points: 280
  Singida unaogopa wanawake, Ruvuma unaogopa wachawi!!!....hizo zote siyo changamoto za kumkimbiza mtu sehem, ni kuonesha namna gani ulivyo weak. Btw mimi nalima Ruvuma, nalima Mbeya, nanext week naenda kuangalia shamba Mgao na Nanhyanga. We endelea kuogopa hirizi
   
 10. p

  paschal sabai Member

  #10
  Mar 30, 2018
  Joined: Apr 5, 2017
  Messages: 84
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 25
  Naishi Singida karibu sana kama una lengo la kufuga kuku aisee huku ndo penyewe njoo pm nikupe full data za singida
   
 11. Kajole

  Kajole JF-Expert Member

  #11
  Mar 30, 2018
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Mkuu hebu sema kitu kuhusu Ruvuma!. Naanza wapi na iwe kijijini mkuu
   
 12. M

  Mwakamele 16 JF-Expert Member

  #12
  Mar 30, 2018
  Joined: Aug 26, 2016
  Messages: 1,512
  Likes Received: 1,036
  Trophy Points: 280
  Singida kuna kuku wengi wa kienyeji halafu bei rahisi lakini kati ya mkoa wa Singida na Ruvuma kwa kuishi na kufanya shughuli za kilimo ni bora uende Songea. Singida ni kukame sana kuliko Ruvuma
   
 13. Simple F

  Simple F JF-Expert Member

  #13
  Mar 30, 2018
  Joined: Nov 17, 2016
  Messages: 852
  Likes Received: 812
  Trophy Points: 180
  Ruvuma tatizo usafirishaji gharama zipo juu
   
 14. Rene Jr.

  Rene Jr. JF-Expert Member

  #14
  Mar 30, 2018
  Joined: Jan 31, 2014
  Messages: 3,327
  Likes Received: 922
  Trophy Points: 280
  Sasa hivi barabara zimefunguka uelekeo wote, vijiji vyote ukiwa unatokea barabara ya njombe viko accessible, wilaya ya namtumbo pia barabara ya uelekeo wa mtwara ni lami tupu, koote huko ardhi ina rutba na mvua za kutosha, na wenyeji hawana maneno ukitua popote ulizia ofisi ya mtendaji nenda kajitambulishe eleza lengo lako utasaidiwa bila shida, ardhi ipo ya kutosha. Kwa vile unaenda vijijini basi ni vizuri kuchukua barua ya utambulisho kutoka huko utokako, na kama ulkuwa mwajiriwa ukaacha kazi beba vitambulisho vyako. Ruvuma zao kuu wanalolima ni mahindi, pia wanalima maharage, kahawa, korosho, karanga, mihogo nk, kifupi ardhi ni inakubali mazao kibao, niwewe tu. Na kwavile wewe unataka kwenda kuishi hukohuko nakushauri tafuta vijiji ambavyo haviko mbali sana na mji, Maeneo kama Mlilayoyo, Mtangimbole, Shuleyatanga, jirani na barabara kuu na pia huduma za umeme na zingine za kijamii, unaweza kujikuta unafuga samaki pia ambao wanahitajika sana Songea. Kiikubwa tafuta kijiji uhame kwanza mkuu, ukipata hata ekari 10 za jirani kijijini we lipa jenga kajumba kako zungushia uzio anza mambo.
   
 15. Rene Jr.

  Rene Jr. JF-Expert Member

  #15
  Mar 30, 2018
  Joined: Jan 31, 2014
  Messages: 3,327
  Likes Received: 922
  Trophy Points: 280
  Bei za kusafirisha nini kwenda wapi gharama ni juu ukilinganisha na wapi?
   
 16. Thad

  Thad JF-Expert Member

  #16
  Mar 30, 2018
  Joined: Mar 14, 2017
  Messages: 6,404
  Likes Received: 13,360
  Trophy Points: 280
  Kwa ufugaji wa kuku nenda Singida, kwa kilimo Ruvuma patakufaa zaidi.
   
 17. Kajole

  Kajole JF-Expert Member

  #17
  Mar 30, 2018
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Nakuja inbox mkuu kukupa namba yangu tuzungumze zaid
   
 18. GENTAMYCINE

  GENTAMYCINE JF-Expert Member

  #18
  Mar 30, 2018
  Joined: Jul 13, 2013
  Messages: 27,704
  Likes Received: 31,872
  Trophy Points: 280
  Samahani Mkuu nimezaliwa Dar japo huko Mtwara ni Nyumbani kwa upande wa ' Bidashi ' wangu ( Mum ) pamoja na Lindi ila sijawahi ' Kukanyaga ' kabisa Mtwara isipokuwa Lindi hasa ' Nachingwea ' niliwahi kwenda mwaka 1988 kama siyo 1989. Mkoa ambao nimeenda na naenda sana ni wa Mara ( Musoma ) ambako ndiko ' Mshua ' wangu ( Dingi ) anatokea. Na naenda sana Mara ( Musoma ) kwasababu ya Samaki wengi na naogopa kwenda Mtwara kwakuwa Panya ni wengi halafu wametukuka. Narudia tena kukuomba usipoteze kabisa muda wako kwenda sijui Ruvuma au Singida huko hakuna Kitu halafu Watu wa huko ni ' Washamba / Mambwigira ' sana.
   
 19. Kajole

  Kajole JF-Expert Member

  #19
  Mar 30, 2018
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Asante sana mkuu,nachukua ushaur wako
   
 20. Gyole

  Gyole JF-Expert Member

  #20
  Mar 30, 2018
  Joined: Sep 20, 2013
  Messages: 3,983
  Likes Received: 3,271
  Trophy Points: 280
  Hapohapo ulipo unaweza kufuga kuku
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...