Kati ya Rais Magufuli na Rais Museveni nani anaweza kupata tuzo ya Rais bora Afrika Mashariki?

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
6,697
9,048
Najaribu kufikiria kama Marais wa nchi hizi 2 Tanzania na Uganda wakipambanishwa kwenye mchuano wa kupata yupi Rais bora katika Afrika Mashariki nani ataibuka kidedea?

Nimepata wazo hili baada ya kulinganisha Utawala wa hawa Marais 2 jinsi wanavozitawala nchi zao kwa mkono wa chuma. Nimengalia utendaji wao wa kazi katika kuwashughulikia wapinzani wao hasa wale wenye kidomodomo na kimbelembele ambao wanatishia tawala zao.

Hivi majuzi Uganda imeginga kwenye vichwa va habari kutokana na sakata la M-7 kumzushia nguli wa Muziki Bobi Wine madai ya Uhaini ati akitaka kumwua M-7 kwa kuurushia mawe msafara wa Rais M-7.Bobi alikamatwa na kushushiwa kipigo cha mbwa mwizi huku akisingiziwa kumiliki bunduki aina ya AK-47 na moja kwa moja kupelekwa Mahakama ya Kijeshi.

Baada ya tuki hilo kuna kelele zimepigwa toka kila pembe ya dunia kuwa Boni Wine ameonewa na Wanausalama wa M-7 hivo aachiwe mara moja. Bada ya kelele hizi M-7 akaanza kubabaika na kuhangaika kwani hakutegemea kuwa hali ingelikuwwa hivo.Ilimlazimu M-7 kwenda kumona Bobi Wine kwenye mahabusu ya Kijeshi na akaongea naye na baaadaye Haraka haraka Mahakama ya Kijeshi ikaamua kumwachia Huru kuwa hana kesi ya kujibu lakini mara akadakwa na Mapolisi na kuswekwa ndani tena. Kelele zikaenelea kupigwa na maandamano kila kona. Hatimaye Mahakama ya Uganda imemwachia Bobi Wine kwa dhamana.....Tayari askari waliompiga Bobi Wine na Wabunge wengine wanasakwa ili wakamatwe na kushtakiwa. Lakini pia Spika wa Bunge la Uganda amemwandikia M-7 akitaka awaeleze Waganda nini kinachoendelea nchini dhidi ya Wabunge wa Upinzani na tayari Bunge limesitishwa kwa iHuo ni ushindi mkubwa sana kwa Waganda..!!,

Tukio la Bobi Wine halina tofauti na lile la Tundu Lissu(MB) aliposhambuliwa kwa risasi 38 mchana kweupe kwenye Viwanja vya Bunge lakini Mungu ni mkubwa TL bado yuko hai. Lakini tukio la TL lilivoshughulikiwa na Mamlaka za Tanzania mpaka leo hii bado limeacha maswali lukuki kwamba mpaka leo hakuna aliyekamatwa kuhusiana na shambulio la TL na mpaka leo hii Bunge na Serkali wamekataa kumpa huduma za matibabu kwa sababu za kitoto kabisa. Lakini kama hiyo haitoshi bado hakuna Mtanzania aliye andamana kulaani na kupinga uonevu huo kwa Tundu Lissu.

Wakati wote Lissu akiugulia maumivu na mateso ya risasi 38 Rais pendwa wa CCM hakuwahi kwenda kumwona TLsi Dodoma, Nairobi wala Ubelgiji. Je kwa hulka hizi 2 za viongozi hawa 2 nani ana uafdhali kidogo anweza angalao akafikiriwa kupewa tuzo kwa kutawala kidiktata na unafuu kidogo?Ni M-7 au Magu?
 
Hakuna hata mmoja.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwa maana hiyo Wote ni madikteta waliokubuhu. Ingawa M-7 kidogo anaka huruma kwa mbaaali kuliko Jiwe. Maana Jiwe bhana yaelekea hana huruma hata chembe.......Juzi tu nilikuwa naangalia msiba wa Marehemu Mama wa Mhe. Sugu sikuona twitt ya Jiwe wala salamu za rambirambi kupitia kwa Msigwa!! JPM kakauka kama vile Sugu kafiwa na.....tu?. Nikakumbuka JPM alivyofiwa na Dadake jinsi alivyolialia na kulalamika kwa kuondokewa na dadake....!!!Lakini kwa vile Sugu ni mpinzani na kafiwa na mama yake acha aendelee KAPATA TAABU SANA......!!.
 
Back
Top Bottom