Kati ya nyimbo hizi upi ungefaa zaidi kuwa wimbo wa taifa?

Ipi inafaa zaidi kuwa nyimbo ya taifa?


  • Total voters
    11

James Martin

JF-Expert Member
Apr 2, 2016
1,206
1,509
Habazi zenu wana Jamii Forums popote pale mlipo. Leo nina swali naombeni maoni yenu. Pia usisahau kupiga kura kuonyesha chaguo lako.

Kati ya nyimbo hizi mbili, 'Mungu Ibariki Tanzania ' na 'Tazama Ramani', ipi ingefaa zaidi kuwa nyimbo ya Taifa?

Mimi binafsi naona kama 'Tazama Ramani' ingefaa zaidi kwasababu kubwa mbili. Kwanza nyimbo hii imetungwa na Mtanzania mwenzetu. Pili, iko tofauti na nyimbo za taifa za South Africa na Zambia. Mapigo ya nyimbo za taifa za nchi hizi mbili yanafanana na ya kwetu ila maneno tu ndio tofauti. Binafsi ningejisikia fahari zaidi kuwa na nyimbo ya taifa ya aina ya pekee bila kuchangia na nchi nyingine na iliyobuniwa na mtu wetu.

Toa maoni yako tafadhali. Halafu naomba msianze kutukanana, huu ni mjadala wa kitaifa mambo ya chama hayana nafasi hapa.

MOD NAOMBA UMFUNGIE KWA MUDA USIOJULIKANA MTU YEYOTE ATAKAYEANZA KUNYOOSHEANA KIDOLE CHA KATI NA ADUI YAKE.
 

Attachments

  • Did_These_Countries_Steal_South_Africa's_National_Anthem?(480p).mp4
    4.3 MB
  • tazama_Ramani_utaona_nchi_nzuri_see_Map_you_will_see_a_beautiful_country_(Tanzania_Patriotic_s...mp4
    17.4 MB
Mungu ibariki Tanzania uendelee kupewa kipaumbele. Unaendana na historia ya nchi, unatunza heshima ya nchi.

Ni ombi la kudumu kwa Mungu, kwamba atuweke kwenye mipango yake kwa binadamu anayewaumba.

Ni wimbo unaosisitizia kuhusu umuhimu wa wote kuwa kitu kimoja, wake kwa waume na watoto.

Tazama ramani ni wimbo wa kuuenzi pia lakini upo kiutalii zaidi kulinganisha na Mungu ibariki Tanzania.
 
Weka na wimbo wa "tazama ramani" tusikie na wenyewe ulivyo ili tuweze ku compare and contrast vizuri mkuu
 
Watafutwe waimba Taarab akiwepo Mzee Yusuph watoe lyrics zenye taarabu na vichambo juu kwa upinzani..itanoga sana kwa uchaguz mwakani
 
Mungu Ibariki unafaa. Ile ni sala, inamtanguliza Mwenyezi Mungu mbele, unaelezea Falsafa zetu kama taifa, n.k.
 
Wimbo wa taifa wa sasa ufupishwe ile part ya Africa iondolewe tubaki na kipande cha nchi yetu.
It's too long na siku hizi dunia iko spidi sana.
 
"TANZANIA TANZANIA nakupenda kwa moyo wote ,nchi yangu Tanzania jina lako ni tamu sana"

Huu ulitakiwa kuwa wimbo wa Taifa...
Kwanza uko kizalendo zaidi pia unaamsha hisia sana yaani unaweza pata mzuka wa kuua mafisadi woote.
 
Back
Top Bottom