Kati ya ndugu zako wa damu wote ni yupi unaempenda zaidi?

Fohadi

JF-Expert Member
Jul 24, 2020
770
2,408
Alizaliwa miaka 8 baada yangu. Nikiwa mtoto wa 3 kuzaliwa kati ya watoto 5, huyu yeye ndie kitinda mimba cha Mama Fohadi na ndiye kaka wa mwisho wa familia. Japokuwa nina upendo wa dhati kwa ndugu zangu wa damu wote ila upendo kwa huyu jamaa naona kabisa umepitiliza. Hajui na hakuna anejua ila mimi binafsi ndiye ninaejua.

Nikiwa na miaka 11, yeye alikuwa na miaka 3. Kipindi hicho nilikuwa kila nikitoka shule lazima niende uwanjani kucheza chandimu na watoto wenzangu. Mara nyingi kati ya hizo, nilikuwa nambeba mgongoni naenda nae hadi uwanjani, namkalisha sehemu mimi nacheza mpira nikimaliza tunarudi wote home. Nilikuwa napenda sana kutembea nae popote pale na siku zote nilitamani kumfanya awe proud na sisi wakubwa zake.

Nikiwa kama Kaka mkubwa katika familia nilitamani kumuonesha upendo na raha ya kuwa na kaka mkubwa kwani sikubahatika kuwa na kaka mkubwa. Mimi ndiye mtoto wa kiume wa kwanza katika familia yetu. Kwetu sisi, mtoto wa kwanza na wapili wote ni wakike na sisi tuliobaki (3,4,5) wote ni wakiume huku mimi nikiwa ndiye 'brother kaka'.

Wakati fulani nimemaliza NECTA ya form two, nilikuwa siendi shule hivyo kila siku nilikuwa namsindikiza asubuhi hadi shule kule alikokuwa anasoma chekechea. Sio kwamba asingeweza kufika peke yake hapana, ila nilitamani nimuoneshe kuwa mimi ni mmoja wa kaka zake na anapaswa kujivunia mimi/sisi.

Sikumbuki kama kwenye maisha yangu ya kujitambua nimewahi kumpiga yule dogo. Sikuwahi kumdekeza ila sikuwahi kuwa katili kwake. Pengine kutokana na gap kubwa la umri kati yetu, kadri miaka ilivyokuwa inasonga ndivyo tulivyozidi kuwa sio watu wa story nyingi.

Miaka imekatika, leo dogo amemaliza kidato cha nne na anajitambua. Pamoja na kukua kiumri, ila bado namchukulia kama yule yule niliyekuwa nambeba mgongoni. Kwa wakati huu ndipo nimegundua nampenda sana huyu jamaa kuliko ndugu zangu wengine japo wote nawathamini na kuwapenda. Juzi dogo kanipigia simu akanambia anatamani sana nimpeleke kwa mkapa tukaangalie Derby ya kariakoo. Sikuweza kukataa ila pia kwa sababu zilizo nje ya uwezo wetu (mimi na yeye) hatukuweza kwenda uwanjani na pengine Mungu alitaka hela zetu za viingilio zipone. Hakuna ombi ambalo amewahi kuniomba nikakataa. Ila ile request yake ilinifanya nifikilie zaidi jinsi gani mkubwa anabeba tumaini la wadogo zake when they face imposibilities.

Mara nyingi kila nikimuangalia huwa najiona nipo responsible kwa ajili ya kesho yake. Hajui kina cha upendo wangu kwake kilivyo na sitataka hata siku moja ajue. Ila kiukweli harakati zangu zote za kimaisha ambazo huwa nazifanya kwa kutokata tamaa yeye huwa ni mmoja wa watu wanaonipush kuzidi kupambana zaidi ili siku moja niwe funguo ya dunia yake awe anachotaka.

Hata mimi sijui kwanini nampenda sana, sifahamu labda kwakuwa ni last born nampa upendo ulio jaa huruma ndani yake.. Kitu pekee ninachojua ni kuwa huyu nampenda sana kuliko ndugu zangu wengine. Wale ndugu zangu 3 upendo wangu kwao ni 100% ila huyu ni zaidi ya 100%.

Ninamshukuru Mungu sina ndugu ninaemchukia kati ya ndugu zangu. Wewe unampenda nani zaidi kati ya ndugu zako wa damu? Kwanini huyo?

 
Hiyo brother kaka ndio maana yake nini
Hahahahha ndomana imewekewa quotation marks (' '). Hiyo ni lugha ya kiuandishi mkuu...siku zote mwandishi anapotaka kuonesha kuwa hajamaanisha serious kitu alichokiandika lazima aweke hizo alama..ni alama fulani zinazotumika kwenye lugha zisizo rasmi.

Mfano...nikisema recycle Bin amuwashia 'moto' Extrovert...hiyo moto nakuwa namaanisha maana nyingine tofauti na moto ambao watu wataufikiria.

Tukija kwa 'brother kaka'........hii ni lugha fulani ya kiutani..ndio maana nimeiwekea hizo alama kuonesha u seriousless fulani kwenye hiyo lugha. I hope umenielewa mzee​
 
Fohadi Mie ndugu yangu nayempenda zaidi ni sister yangu ambaye tumefuatana we share a lot in common!

My bro first borne tumeenda astray kwa itikadi na mambo mengi tho we still brothers. We have social connection ila sio kama na sisteri wangu!
 
Back
Top Bottom