Kati ya Mzee Mwinyi aka Mzee Ruksa na Che Mkapa aka Mambo nani baba wa ufisadi Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kati ya Mzee Mwinyi aka Mzee Ruksa na Che Mkapa aka Mambo nani baba wa ufisadi Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mpayukaji, Apr 4, 2012.

 1. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #1
  Apr 4, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mwinyi alianzisha mtindo wa hovyo wa Ruksa ambapo wezi wachache waliutumia kuuibia umma. Rejea kashfa ya Loliondo.Mkapa alianzisha mtindo wa kuutetea ufisadi wazi wazi kwa kuuliza nani si fisadi huku akiasisi na kufanikisha wizi wa EPA ambapo mabilioni ya shilingi yaliibiwa na kutumbukizwa kwenye uchaguzi uliomnufaisha Jakaya Kikwete. Je kati ya wawili hawa nani baba wa ufisadi Tanzania? Kikwete anajulikana alivyofaidika na pesa ya EPA. Hii ni kutokana na kushutumiwa kule Mwembe Yanga asikanushe.
   
 2. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Hakuna shetani nafuu. Awe mdogo,mkubwa mzee wote ni shetani tu. Nina maana wote ni mafisadi tu.
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Apr 4, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Wote waliondoa vizingiti vya mafisadi kukomba mali za watanzania

  1. Mwinyi kwa kuanzisha azimio la zanzibar aliondoa JKT kwahiyo mafisadi wengi hawakwenda Jeshini baadhi yao waliingia serikalini na wengine waligombea Ubunge na wengine walinunua viwanda vya serikali na kuviua kabisa

  2. Mkapa yeye baada ya kuleta hao wawekezaji hakuwauliza ushuru, kodi wala ajira za wananchi; hao wawekezaji wa madini mfano GOLD wakala, kakatapika na bado wanakula

  WOTE NI SAWA SAWA; Wameiua nchi kwa manufaa yao wenyewe na marafiki zao
   
 4. monongo

  monongo JF-Expert Member

  #4
  Apr 4, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 370
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Hakuna Shetani mkubwa wala mdogo!! Shetani ni nguvu ya uharibifu kwa Taifa, Familia, na Jamii kwa ujumla.wote ni wabaya Tu!! Mkapa aliwachukia wapinzani,aliwaona ni maadui wake.Aliwadharau sana, aliwaita wana siasa uchwara,
   
Loading...