Kati ya Mkuu wa Majeshi na Waziri nani ni Mkuu kiprotokali?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,870
155,829
Tukio linaloendelea Mererani Ni la Bwana Leizer kukabidhi jiwe la kilo sita la Tanzanite.

Naona Mkuu wa Majeshi amehutubia mwanzoni kabisa, Kisha wakafuata wakuu wa mikoa ya Kilimanjaro, Manyara kisha akafuata Naibu Waziri na Waziri.

Hii kiprotokali imekaaje? Yaani Mkuu wa Majeshi Ni mdogo hata kwa Mkuu wa Mkoa?
 
Ukiona kuna cheo cha kisiasa, kiprotocally huyo ni mkubwa ni mkubwa kiungozi kuliko cheo cha kiutendaji. Polititiacians ni leaders watendaji ni operating machines controlled by politicians. Hapo hata angekuwa diwani still angekuwa mkuu kuliko mabeyo.
 
Mfumo wetu umekaa kisiasa zaid Yan wanasiasa wanakua na kauli kubwa mbele ya majeshi
Mtu akiwa mkuu wa mkoa huyo anakua na uwezo wa kuyapa amri majeshi yaliyo ndani ya mkoa wake na yakatii,, nafkir hii imewekwa hivi ili kumlinda aliepo madarakan
 
Mfumo wetu umekaa kisiasa zaid Yan wanasiasa wanakua na kauli kubwa mbele ya majeshi
Mtu akiwa mkuu wa mkoa huyo anakua na uwezo wa kuyapa amri majeshi yaliyo ndani ya mkoa wake na yakatii,, nafkir hii imewekwa hivi ili kumlinda aliepo madarakan
Majeshi ya polisi sio jw, Kama unataka uamini, mkuu wa mkoa anaweza kwenda kituo cha polisi gafla hata bila taarifa yoyote akatoa amri hata kumfukuza kazı, ila sio kwenda kambi ya jeshi hovyo hovyo
 
Majeshi ya polisi sio jw, Kama unataka uamini, mkuu wa mkoa anaweza kwenda kituo cha polisi gafla hata bila taarifa yoyote akatoa amri hata kumfukuza kazı, ila sio kwenda kambi ya jeshi hovyo hovyo
Mkuu wa wilaya/mkoa hana mamlaka ya kumfukuza polis kaz mkuu, polis had afkuzwe kaz Kuna taratibu zao za kijesh znafatwa kwanza,,,, kwenye mkoa Kuna kitu kinaitwa kamati ya ulinzi na usalama kwenye hiyo kamati majeshi yote yapo Jw, polis, magreza na mwenyekit wao ni mkuu wa mkoa Yan yeye ndo anawapa order wote hao Hadi hao JW unaowasema wewe
 
Kwa nchi zilizoendelea hua wanawafungia siku nne bila maji wala chakula humo ndani ni kuchapana makonde atakayetoka baada ya siku nne ndiyo anakua mkubwa kiprotokali.

Nchi zinazofuata huu utaratibu ni Andorra, Kazakhstan, Estonia, Jimbo la Apuhlachia Marekani na Uganda ya Obote.
 
Sisi Tanzania tunafuata mfumo wa nchi za madola

Malkia mwakilishi wake Gavana anakuwa ananguvu za kimalikia

Hivyo hivyo kwa Mkuu wa mkoa anakuwa ananguvu kama Raisi
 
Mkuu wa majeshi si mdogo tu kwa RC mpaka kwa DC Ni mdogo pia
Aisee.
Screenshot_2020-08-03-12-32-20-1.jpg
 
Mkuu wa wilaya hana mamlaka ya kumfukuza polis kaz mkuu, polis had afkuzwe kaz Kuna taratibu zao za kijesh znafatwa kwanza,,,, kwenye mkoa Kuna kitu kinaitwa kamati ya ulinzi na usalama kwenye hiyo kamati majeshi yote yapo Jw, polis, magreza na mwenyekit wao ni mkuu wa mkoa Yan yeye ndo anawapa order wote hao Hadi hao JW unaowasema wewe

Kwa JW iko tofauti kidogo mkuu. Kwakua utawala wa JW hauko kimkoa bali unaenda kwa Brigedi ambazo ziko kwenye kanda.

Kamati ya Ulinzi na usalama inakua na Kamanda wa TAKUKURU( ni kiongoz wa mkoa), Wa uhamiaji, wa magereza, wa polisi hawa wote wanakua ni wakuu wa hizo idara katika mkoa na kwenye wilaya

Ila Mshauri wa mgambo wa mkoa/ wilaya wanaoingia kwenye hii kamati wanakua mara nyingi ni attacheès tu ila sio wakuu wa JW eneo hilo husika.

Ila tukirudi kwenye mada DC na RC wanatoa amri kwa mamlaka waliyokasimishwa na Amir Jeshi. So wako juu kiprotokali
 
Back
Top Bottom