Kati ya mkoa wa Dodoma na Kilimanjaro upi utakuwa wa kwanza kuwa jiji??

Mwasita Moja

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
2,903
2,580
Amani iwe kwenu.

Tukiendelea kusukuma gurudumu la maendeleo ni vyema tukamulika mkoa kwa mkoa.

Sasa kwa maoni yenu wadau mliowahi kufika Dodoma, Kilimanjaro na ambao hamjawahi kufika Hugo.
Je kati ya mikoa hii upi una vigezo vyote vya kuwa jiji kwanza??
 
Mkoa hauwezi kuwa jiji, bali manispaa ndio hupanda na kuwa jiji.
Kwa Dodoma ni Dodoma manispaa na kwa mkoa wa Kili basi Moshi itapanda kuwa jiji. Kwa sasa Dodoma ina vigezo karibu vyote vya kuwa jiji.
Moshi bado kidogo.
Nimeshakaa kwenye miji yote miwili.
 
Mkoa hauwezi kuwa jiji ila mji au manispa ndio hupanda hadhi na kuwa ni jiji,,, ila DODOMA MAANA MOSHI BADO SAANA.
 
Tatizo la moshi matajiri wamejifanya wajanja, badala ya kujenga mjini kwao wamejenga vijijini kwao.
 
Amani iwe kwenu.

Tukiendelea kusukuma gurudumu la maendeleo ni vyema tukamulika mkoa kwa mkoa.

Sasa kwa maoni yenu wadau mliowahi kufika Dodoma, Kilimanjaro na ambao hamjawahi kufika Hugo.
Je kati ya mikoa hii upi una vigezo vyote vya kuwa jiji kwanza??
Sahihisha kidogo, Kilimanjaro siyo Mji. Moshi ndiyo Mji,ktk Mkoa wa Kilimanjaro.
 
Dodoma na dar ndiyo miji pekee inayoendelezwa na kubebwa na serikali wakati mingine inaendelwa na wakazi wake wenyewe. Hivyo dodoma itabebwa soon kuwa jiji
 
Sio wewe ulileta mada siku zilizopita ukilinganisha tena Kilimanjaro na Dodoma?
Kwa taarifa yako kili na dodoma yako ni sawa na usingizi ba kifo kwa kilimanjaro. Mkoa pekee Tz wenye ustaarabu kuliko mingine yote .
 
Amani iwe kwenu.

Tukiendelea kusukuma gurudumu la maendeleo ni vyema tukamulika mkoa kwa mkoa.

Sasa kwa maoni yenu wadau mliowahi kufika Dodoma, Kilimanjaro na ambao hamjawahi kufika Hugo.
Je kati ya mikoa hii upi una vigezo vyote vya kuwa jiji kwanza??
sielewi unamaanisha nini?
 
Moshi hapana.vigezo vya kuteua majiji nadhani kiongezwe cha kuwa na proper urban plan.mji kama mbeya ni kayikati ya mji palipojengwa na wakoloni panaeleweka.kwingine ni ovyo na hilo lina apply mikoa
 
Back
Top Bottom