Kati ya Mkapa, Kikwete, na Magufuli nani amejenga miundombinu mingi?

Wajumbe

Senior Member
Jul 26, 2020
136
379
Wadau, ili kuweka rekodi sawa, hebu tujikumbushe nani kati ya Mkapa, Kikwete, na Magufuli aliyejenga miundo mbinu mingi. Miundo mbinu hii ni kama barabara, shule, hospitali, vyuo, viwanja vya ndege, madaraja, ndege, meli, miundo mbinu ya umeme, vivuko, majengo ya taasisi mbalimbali za umma na kadhalika.

Je, tunaweza kuorodhesha miundo mbinu iliyojengwa na kila mmoja wao? Hii itasaidia kuondoa siasa za ghiliba na uongo kuwa kila kitu tangu uhuru kafanya rais x . Tuwe wakweli ndugu zangu, tusipotoshe, tusipotoshane.

Wajumbe oyee
 
Kila mtu amefanya kulingana na wakati wake na uhitaji wa nchi kwa wakati ule na wote wako sawa hakuna aliyemzidi mwenzake.

Mwingine alijenga msingi kwa kuwa kipindi chake kilikuwa ni cha kujenga msingi, mwingine akajenga ukuta kwa kuwa msingi ulikuwa umejengwa na mtangulizi wake,na mwingine anaendeleza pale wenzake walipoishia.

Nawengine wanao kuja wataendeleza hivyohivyo kulingana na wakati na mahitaji ya wakati huo kwa kuwa ni safari isiyokuwa na mwisho mpaka dunia itakapokunjwakunjwa kama karatasi na kutupwa motoni hapo ndipo utakuwa mwisho wa safari.
 
Tusimeze maneno
1.jk
Udom
Songwe airport (airports)
Quality roads (iringa-dodoma,tabora-nzega,nk)
Mlonganzila na Bw Moapa hospitals
2.big Ben
Moapa brigade
Roads (dom-singida mwanza)
Bunga
Na bwmkapa stadium

3.magufuli
Sgr
Stiglitz
Flyover zilizopita kamili kaka
Mzee wa uzinduzi
 
Wadau, ili kuweka rekodi sawa, hebu tujikumbushe nani kati ya Mkapa, Kikwete, na Magufuli aliyejenga miundo mbinu mingi. Miundo mbinu hii ni kama barabara, shule, hospitali, vyuo, viwanja vya ndege, madaraja, ndege, meli, miundo mbinu ya umeme, vivuko, majengo ya taasisi mbalimbali za umma na kadhalika.

Je, tunaweza kuorodhesha miundo mbinu iliyojengwa na kila mmoja wao? Hii itasaidia kuondoa siasa za ghiliba na uongo kuwa kila kitu tangu uhuru kafanya rais x . Tuwe wakweli ndugu zangu, tusipotoshe, tusipotoshane.

Wajumbe oyee
MKAPA:
SITAMWONGELEA HUYU KWANI KATUTOKA TAYARI

JK:
1. UDOM
2. DART
3. JNIA III
4. TAZARA FLYOVER (JPM KAMALIZIA MPANGO ULIOKUWA MEZANI TAYARI)
5. UBUNGO FLYOVER (JPM KAMALIZIA MPANGO ULIOKUWA MEZANI TAYARI)
6. KURASINI FLYOVER
7. DARAJA LA KIGAMBONI
8. JKCI
9. MLOGANZILA
10. BARABARA ZINAZOUNGANISHA MIKOA NA WILAYA NCHI NZIMA PAMOJA NA KWENDA NCHI JIRANI

JPM:
1. SGR (INASEMEKANA ITAISHA IN 10 YEARS TIME????)
2. STIEGLER'S GORGE (INASEMEKANA ITAISHA IN 15 YEARS TIME???)
3. ENDELEZENI WENYE KUJUA VINGINE MAANA MIMI SIKUMBUKI!!
 
Wadau, ili kuweka rekodi sawa, hebu tujikumbushe nani kati ya Mkapa, Kikwete, na Magufuli aliyejenga miundo mbinu mingi. Miundo mbinu hii ni kama barabara, shule, hospitali, vyuo, viwanja vya ndege, madaraja, ndege, meli, miundo mbinu ya umeme, vivuko, majengo ya taasisi mbalimbali za umma na kadhalika.

Je, tunaweza kuorodhesha miundo mbinu iliyojengwa na kila mmoja wao? Hii itasaidia kuondoa siasa za ghiliba na uongo kuwa kila kitu tangu uhuru kafanya rais x . Tuwe wakweli ndugu zangu, tusipotoshe, tusipotoshane.

Wajumbe oyee
Serikali inakusanya kodi inatekeleza mipango kama kujenga barabara. Ni jukumu lake na hivo haihita kusifiwa.
Miaka hii imegeuka sijui kwa nini.
Kitu cha muhimu ni kodi. Ili kodi ipatikane ya kutosha ni lazima watu wawe na uwezo wa kiuchumi maana ndio hulipa kodi ambo hujenga miundo mbinu na kutoa huduma.
Kwa hiyo watu ndo wanastahili kusifiwa kwanza kwamba wametoa kodi na kuwezesha maendeleo.
Anayejenga tunamlipa kwa kazi ya kukusanya na kujenga wenye pesa ni sisi. Sijui tukoje!

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Mimi naona wote wamejitahidi kulingana na wakati wao na hali ya uchumi na mahitaji ya wananchi.
Sisi wananchi ndo wazalishaji na tunahitaji watu wachache i.e. serkali tuwakabidhi hela yetu i.e. kodi zetu ili wasimamie miradi yetu kama ujenzi. Tunawalipa kwa kazi hiyo. Hivi wakimaliza kujenga tunapaswa kuwasifu kwamba wametuletea hivyo vitu wakati pesa ni zetu? Sifa pekee wanazostahi ni namna walivofanya vizuri lakini sisi ndo tunastahili kujipongeza kwa kupiga hatua.
Kwa hiyo miundombinu mingi au michache inategemea na jinsi tulivozalisha mali na uhitaji wetu kwa waka husika.

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom