Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 34,671
- 40,912
Chama Cha Demokrasia na Mandeleo kipo kwenye wakati mgumu sana wa kumpata mgombea wa kiti cha urais kwa uchaguzi wa mwaka 2020.
Ugumu wa upatikanaji wa mgombea unakuja kutokana na sifa mbali mbali walizonazo makada wake.
Ingawa mgombea wa nafasi hiyo bwana Lowasa bado ana nafasi hiyo ila ushindani umeongezeka kwake.
Mwenyekiti wa chama hicho Bwn. Freeman Mbowe ambaye kwa sasa anafahamika kama mfungwa wa kisiasa anazidi kuchanja mbuga katika kupaliilia nafasi hiyo adimu kabisa na ya kihistoria.
Mwanasheria mkuu wa Chama Bwn. Lisu naye hayuko nyuma kwani ameongeza umaarufu maradufu baada ya kuvamiwa na kupata shambulizi la risasi, jambo ambalo limemfanya afanye matibabu nje ya nchi , ambako kwa hivi sasa anafanya ziara ulaya na marekani akinadi tukio lake la kupigwa risasi.
Kwa kuangalia sifa hizo kemkem ambazo kwa macho ya wanachama na wafurukutwa na chadema ni uzalendo wa kutukuka, nakosa majibu ni nani kati yao atakayebeba mikoba ya kukiwakilisha chama.