Kati ya matofali ya kuchoma na ya saruji unachagua yapi?

Umeongea kwa emotions na sio kwa facts ama rational mind mkuu.
Hebu Kama vipi tuingie maabara.
Inategemeana ni wapi.jamaa ameongelea nyumba na sio hizo structures zako.
Choma in terms of tension force iko poa zaidi ya sementi.
Ila la sementi liko poa in terms of compressive strength Ila sio tension.

Ila pia ghorofa ukiweka hata vioo ni sawa Ile ni weather protection.
Choma ghorofani yanakubali Mana kazi ya Wall katika ghorofa sio load bearing wall Bali ni weather protection.
Kumbuka ghorofa ni beam ,column,slabs , foundation na stairs ndo Zina kazi ya kulishikilia jengo Ila wall Haina kazi kiusalama.
Sawa kabisa. Aisee, kuna watu wanashangaza sana. Eti anahoji kabisa uliona wapi ghorofa likijengwa kwa tofali la kuchoma. Unajua hata kama wewe si fundi ama hujui lolote kuhusu ujenzi/matofali, huwezi kuuliza swali kama hili. Hii inaashiria huyu mtu uelewa wake una shida sana. Yani yeye kutoona hayo majengo basi matofali ya kuchoma hayafai? dah! Yaani anadhani maisha na mazingira aliyokulia ndiyo dunia hiyo pekee.Asijue kuna maeneo tofali za kuchoma ndo maisha.

Hivi, watu hivi wanafanya makusudi ama wamelogwa?
 
Mmesahau matofali mabichi yanayotumika uku Mbeya nayo ni standard sana🤓🤓🤓
Kuna akina sisi mkuu, tofali zetu za saruji haziingii kwa hizo tofali mbichi. Tofali zetu hiz za mfuko mmoja tofali 40? Sasa hapa nimcheka wa matofali mabichi kweli, nitakuwa mzima?
 
Hakuna unachoongeza hapa. Usemacho ndicho tusemacho wenzako. Swali halikuwa tofali la wapi bali tofali lipi kati ya la kuchomwa na la saruji. Nilikuepeleka Iringa baada ya kuona unaropoka tu ,eti, kisa huoni watu wakijengea basi ni ya masikini. Hii hoja ya kindezi sana ndugu yangu. Kha! Rejea post ndugu. Unachokifanya ni redundunt. Sisi tulishasema kuwa kama factors zote zikiwa constant, la kuchomwa ni bora zaidi. Hii hata Engineering inakiri. Hii ndo hoja hapa. Sasa unarudia kitu ambacho wenzako ndicho tunakisema.

Ukija hapa kwetu , bado huwezi kusema tu "through armchair thinking", eti tofali za saruji ni bora kuliko za kuchomwa. Kwa ujenzi wa kibongo chochote kinawezekana. Watu wengi tunajenga kwa materials yaliyo chini ya kiwango. Kwa hizi tofali itategemea tu ufyatuaji ulivyofanyika. Tupo maelfu ambao matofali yetu ni ya saruji lakini yanamomonyoka kama biskuti zile digestive kwa kutokufuata kanuni. Huyu akilinganishwa na aliyechoma tofali vema, tayari tutasema ya saruji si bora.Na kinyume chake ni hivyohivyo. Sasa hiki si kigezo cha kisayansi maana tunazungumzia matofali ambayo tayari kuna tatizo.

So, hoja ya msingi ni hiyo hapo juu, tukitumia standards , za kuchomwa ni madhubuti zaidi. Suala la uduni wa bidhaa kwa watanzania ni kesi nyingine.

Haya, nisijekuharibu biashara yako ya tofali za kuchoma. 🤣
 
Changamoto ni kuwa haya ya saruji unanunua matofali, mchanga nae mashine. Fundi na amepata pa kuponea anakupiga humohumo anatoa matofali 45 kwa mfuko wa saruji na anakuambia mfuko mmoja ametoa 25
Kwa tanzania yalikua yakizalishwa na wakatoliki wamishenari wabenediktini wa peramiho,ila bei zao sasa ni kama za ulaya vile,hizo walikua wanauziana wao kwa wao tuu waafrika walichemsha
 
Tofali ya kuchoma ina nguvu kuliko ya cement? Aisee!

Hivi ushawahi kuona ghorofa linajengwa kwa tofali ya kuchoma?

Ukijibu hilo pia jibu hili..

Kwanini kwenye structures kama matenki ya maji wanatumia tofali za cement na sio tofali udongo??
Mzee ghorofa zipo kibao,tatizo kwa dar,udongo wake hauivi wala kushikana kutengeneza tofali hivyo wanalazimika kutumia la saruji,la kuchoma kwa ghorofa ni recommended kwa kuww pia linapunguza uzito kwenye jengo hivyo kufanya lidumu zaidi
 
Kwasababu tofali za kuchoma hunyonya maji au unyevu
Basi itakua haijachomwa mzee,kuna udongo kama wa mbozi mbeya na huko songea tofali unaona mpaka chuma kimeyeyukia kwenye tofari linapochomwa kwa kuwa udongo wao una chuma kingi,hilo halivunjiki asilani,tena hata usipolichoma ukijengea hata mvua inyeshe utalikuta limesimama vile vile,tofauti na maeneo mengine utakuta tofali ikinyeshewa inabomoka au kupukutika kama zile za bloku
 
Sasa kwanini magorofa na matenki ya maji wanatumia tofali za cement? Au hao wajenzi wa magorofa na matenki hawataki uimara?
Kutokana na sehemu bwana na upatikanaji wake si kila sehemu wanajengea,pili wajrnzi wengi wanapenda bei mtelemko ili kufidia faida wanalazimika kutumia za bloku maana za kuchoma gharama kwa kuwa zina maumbo madogo
 
Kipindi najenga..nilichukua udongo nkachanganya Na cement nikafyatua halafu nikachoma.....Saivi hata kuweka picha ukutani siwezi...
Ulichoma tofali yenye simenti?! Kivipi mkuu hebu fafanua maana kwa uelewa wangu mdogo simenti inafeli strength just around 300C, which means ukienda above that temperature utaambulia biscuits badala ya tofali. Lakini pia moto na simenti ni binder na huwezi kuzitumia zote kwa wakati mmoja maana utakua unaongeza gharama za ujenzi pasipo sababu za msingi
 
Wacha nichangie kidogo kwenye huu mjadala. Tofali ya kuchoma ni imara; bora na inadumu zaidi ya tofali ya simenti. Tofali ya kuchoma inatokana na natural materials na binder ya hizo materials ni moto. Kitu chochote kikichomwa close to it's melting point hua particles zake zinayeyuka na kushikamanisha particles zingine lakini pia ule uji uji huziba mashimo na nyufa zote. Kwa jinsi hii tofali ya kuchoma itakua imara na kwakua imetokana na natural materials hasa mfinyanzi; majivu ya volcano ambavyo kuungua kwake kunaunda kitu kama kauri (marumaru ilivyo); tofali hili ni ngumu kushambuliwa na chumvi; kutu; unyevu; fungus, na kemikali nyingine (hii ni sifa ya fired ceramic product including tiles; firebrick, vyombo vya nyumbani; masinki).
Cha kukufrahisha ni kwamba vinu vya kuyeyushia mawe/ madini ujenzi/ limestone wakati wa kuandaa cement vimeundwa kwa tofali maalum za kuchoma zitokanazo na mchanganyiko ww udongo wa mfinyanzi na madini mengine especially Bauxite; ukizingatia kwamba ili cement hutengenezwa kwa kuyeyusha hizi materials at temperature above 1600C. Point hapa ni processing techniques tu; tofali za kuchoma tunazotengeneza sisi hapa nyumbani hatuzingatii viwango vya uzalishaji na narudi palepale kwenye processing techniques & selection of materials.
Mtu anachoma tofali bila temperature regulation maana anatumia pumba na kuni ni ngumu kujua unachoma hilo tofali kwenye temperature ipi kifikia sintering temperature ya materials ulizotumia lakini pia mfinyanzi wa eneo A hauwezi kua na chemical contents sawa so lazima ufanye chemical analysis kujua udongo wako una chemical contents zipi na je zinafanana na zile zinazotakiwa kwenye uzalishaji wa tofali lako according to recognized world standards; maana yake hapo kuna additives lazima uongeze kufikia viwango vinavyotakiwa.
Sisi hatufanyi ivyo ndo maana ni ngumu kumshawishi mtu kama tofali la kuchoma ni imara kuliko la simenti; lakini ukweli tofali za kuchoma hata gharama zake za uzalishaji ziko juu na hivyo tofali hii haiwezi kua cheap kama watu wengi wanavyofikiria; ukitaka kuamini agiza leo tofali kutoka India; China au Pakistan uone gharama zake na zinaendana na ubora wake pia; sie tunachoma matope hata shape tu ni mbovu matu atakuelewa vipi?!
 
Umeongea kwa emotions na sio kwa facts ama rational mind mkuu.
Hebu Kama vipi tuingie maabara.
Inategemeana ni wapi.jamaa ameongelea nyumba na sio hizo structures zako.
Choma in terms of tension force iko poa zaidi ya sementi.
Ila la sementi liko poa in terms of compressive strength Ila sio tension.

Ila pia ghorofa ukiweka hata vioo ni sawa Ile ni weather protection.
Choma ghorofani yanakubali Mana kazi ya Wall katika ghorofa sio load bearing wall Bali ni weather protection.
Kumbuka ghorofa ni beam ,column,slabs , foundation na stairs ndo Zina kazi ya kulishikilia jengo Ila wall Haina kazi kiusalama.
Huyo jamaa hajui kitu. Ni taburalasa.

Anafikiri ghorofa linashikiliwa na ukuta!! Duuh!
 
Sawa kabisa. Aisee, kuna watu wanashangaza sana. Eti anahoji kabisa uliona wapi ghorofa likijengwa kwa tofali la kuchoma. Unajua hata kama wewe si fundi ama hujui lolote kuhusu ujenzi/matofali, huwezi kuuliza swali kama hili. Hii inaashiria huyu mtu uelewa wake una shida sana. Yani yeye kutoona hayo majengo basi matofali ya kuchoma hayafai? dah! Yaani anadhani maisha na mazingira aliyokulia ndiyo dunia hiyo pekee.Asijue kuna maeneo tofali za kuchoma ndo maisha.

Hivi, watu hivi wanafanya makusudi ama wamelogwa?
 
Wacha nichangie kidogo kwenye huu mjadala. Tofali ya kuchoma ni imara; bora na inadumu zaidi ya tofali ya simenti. Tofali ya kuchoma inatokana na natural materials na binder ya hizo materials ni moto. Kitu chochote kikichomwa close to it's melting point hua particles zake zinayeyuka na kushikamanisha particles zingine lakini pia ule uji uji huziba mashimo na nyufa zote. Kwa jinsi hii tofali ya kuchoma itakua imara na kwakua imetokana na natural materials hasa mfinyanzi; majivu ya volcano ambavyo kuungua kwake kunaunda kitu kama kauri (marumaru ilivyo); tofali hili ni ngumu kushambuliwa na chumvi; kutu; unyevu; fungus, na kemikali nyingine (hii ni sifa ya fired ceramic product including tiles; firebrick, vyombo vya nyumbani; masinki).
Cha kukufrahisha ni kwamba vinu vya kuyeyushia mawe/ madini ujenzi/ limestone wakati wa kuandaa cement vimeundwa kwa tofali maalum za kuchoma zitokanazo na mchanganyiko ww udongo wa mfinyanzi na madini mengine especially Bauxite; ukizingatia kwamba ili cement hutengenezwa kwa kuyeyusha hizi materials at temperature above 1600C. Point hapa ni processing techniques tu; tofali za kuchoma tunazotengeneza sisi hapa nyumbani hatuzingatii viwango vya uzalishaji na narudi palepale kwenye processing techniques & selection of materials.
Mtu anachoma tofali bila temperature regulation maana anatumia pumba na kuni ni ngumu kujua unachoma hilo tofali kwenye temperature ipi kifikia sintering temperature ya materials ulizotumia lakini pia mfinyanzi wa eneo A hauwezi kua na chemical contents sawa so lazima ufanye chemical analysis kujua udongo wako una chemical contents zipi na je zinafanana na zile zinazotakiwa kwenye uzalishaji wa tofali lako according to recognized world standards; maana yake hapo kuna additives lazima uongeze kufikia viwango vinavyotakiwa.
Sisi hatufanyi ivyo ndo maana ni ngumu kumshawishi mtu kama tofali la kuchoma ni imara kuliko la simenti; lakini ukweli tofali za kuchoma hata gharama zake za uzalishaji ziko juu na hivyo tofali hii haiwezi kua cheap kama watu wengi wanavyofikiria; ukitaka kuamini agiza leo tofali kutoka India; China au Pakistan uone gharama zake na zinaendana na ubora wake pia; sie tunachoma matope hata shape tu ni mbovu matu atakuelewa vipi?!
Hallelujah!
 
Mtafiti77 soma hii hadi mwisho.
 
Hallelujah!

Mimi nimewahi kupata tofali za kuchoma pcs kadhaa kutoka pakistan ni ngumu ile mbaya, huwezi kulinganisha na hizi zetu tunazochoma kienyeji, ukitaka kujaribu chukua tofali yetu moja, chukua hiyo ya kutoka pakistan na chukua kipande cha tofali ya Cement weka hivyo vipande vyote kwenye barabara ya lami na magari yavisage, tofali letu la kuchoma litasagika na kuwa unga completely na lile la cement litakuwa vipande vipande kama changarawe (partially ground) na hilo la Pakistan almost litabaki intact.

Conclusion yangu ni kwamba, matofali ya saruji ni bora kulinganisha na matofali yetu ya kuchoma ambayo hata yanaweza kushambuliwa na mchwa wajengao kirahisi.
 
Na shida ya tofali ya cement ni kwamba imeundwa kwa materials ambazo ni rahisi sana for chemical attack,... we angalia tu tofali ya cement ilofyatuliwa na kuachwa nje ihesabie miezi 6 tu itakua ishaanza kupoteza strength yake.
Yani cement jua ni adui; mvua ni adui; chumvi ni adui ni rahisi sana kureact na external agents, tofauti na ya kuchoma ambayo ina sifa ya fired ceramic product (hizi ni resistive to chemical attack in nature), na ikichomwa vizuri ikaiva hua inatengeneza glass layer (glaze)kwa juu na kuifanya itereze (chukua mfano wa vyungu au ile layer ya udongo kwenye majiko ya mkaa), kwa lugha rahisi tu; ulishawahi kuona kigae cha chungu kinaoza kikizikwa ardhini?! That's the science/ chemistry behind. Kwahiyo hutakiwi kujiuliza maswali mengi juu ya kwanini nyumba za tofali za cement hazidumu na kwenye nchi za wenzetu hawazitumii sana.
Kuna mdau aligusia swala la matumizi ya tofali za kuchoma kwenye magorofa; inawezekana na tena ziko recommend sana maana ni imara na nyepesi kuliko concrete. Lakini pia nimeona concern ya kua tofali za kuchoma zina joto; hapa inategemea na aina ya materials ulizotumia km zina thermal conductivity kubwa ambapo sasa kwenye kipengele cha additives utatakiwa kuongeza materials zenye high thermal insulation capacity kulingana hali ya hewa ya eneo husika au according to customer's preferences
Nadhani shida ni reference tu ya tofali za kuchoma kwenye hii mada tumetumia hizi zetu ambazo tunavuruga matope tu ya kwenye vichuguu na majarubani; lakini pia hata aina ya mashine tunazotumia kwenye swala la crushing; grinding; sieving; moulding (hapa swala la pressure ni muhimu pia); ukaushaji; uchomaji (hapa kuna issue ya firing parameters), materials selection, analysis and preparations bila kusahau formulations (hapa kuna vitu utaongeza- additives); finally lazima utest physical- mechanical properties
Generally shida ni teknolojia tunayotumia inafanya watu wadharau tofali za kuchoma
 
Back
Top Bottom