Kati ya matofali ya kuchoma na ya saruji unachagua yapi?

in Mara ya kwanza naona watu wanalinganisha choma na saruji. Tofali la kuchoma lina heshima yake. Sema tuu basi waswahili tumekuwa experts wa slope na magumashi. Lakini tofali lililochomwa kitalaam halina mpinzani.
 
Tofali ya kuchoma ina nguvu kuliko ya cement? Aisee!

Hivi ushawahi kuona ghorofa linajengwa kwa tofali ya kuchoma?

Ukijibu hilo pia jibu hili..

Kwanini kwenye structures kama matenki ya maji wanatumia tofali za cement na sio tofali udongo??
Ndio tena yako mengi tuu
 
Sasa kwanini magorofa na matenki ya maji wanatumia tofali za cement? Au hao wajenzi wa magorofa na matenki hawataki uimara?
Shida ni kasumba na pia haya ya saruji uandaaji wake hadi yapelekwe maabara kuyapima strength ni WA haraka kuliko tofari za kuchoma zenyewe zina process ndefu kuanzia uchaguaji wa udongo hadi kuichoma.

Sasa huwezi kutumia hizi za kubumba unless ujiridhishe na size,uimara na strength yake maana hizo ni Kazi za serikali mkuu.
 
Nakuambia hivi; hapa Bongo hakuna matofali ya kuchoma yanayoweza kuzidi matofali ya Saruji, labda matofali ya kuchoma kutoka nje ya Bongo, mfano sisi tulikuwa tunaagiza tractors kutoka Pakistani (Massey Ferguson), zilikuwa zikiletwa ndani ya kontena 40 feet, humo ndani ya kontena wapakistani walikuwa wanaweka vitofali vya kuchoma kama vigingi kuzuia hayo matreka yasiseleleke wakati wa usafirishaji, hayo matofali yalikuwa ni magumu ajabu kuliko matofali ya Saruji, kumbuka muulizaji alikuwa anataka kujua ubora kati ya matofali ya kuchoma na ya saruji yanayopatika HAPA HAPA Bongo ambako huyo nduguye ndipo anapojenga.

Hapa Bongo historia inaonyesha kwamba watu wenye kipato kidogo ndio hujengea kwa matofali ya kuchoma isitoshe mimi mwenyewe nimewahi kushuhudia nyumba nyingi zikijengwa kwa matofali ya kuchoma na si mara moja nimewahi kujaribu ugumu wa hayo matofali ukilinganisha na matofali ya Saruji (1 bag for 25 bricks).
Na wewe una shida zako binafsi pia,kwa taarifa yako wenye pesa wanaagiza tofari choma maalumu kutoka maeneo zinakopatikana za uhakika wanajengea nyumba kali Sana 👇👇

IMG_20210424_081329_602.jpg
 
Mmesahau matofali mabichi yanayotumika uku Mbeya nayo ni standard sana🤓🤓🤓
Inategemeana na udongo,kuna udongo mwingine ukichoma unahatibu ubora,huo wa Mbeya unafaa kujengea wenyewe ila Ili yawe imara zaidi inafaa yaongezewe saruji kiasi afu fyatua kausha utaona mziki wake.
 
Mkuu haya mambo usichanganye. Naona unaniambia hapa kinachoongelewa ni nyumba za kawaida na "sio structure zangu" lakini cha kushangaza na wewe badala ya kuongelea hizo nyumba ukarudi kwenye structure zangu!!

Kama uko kwenye sekta ya ujenzi utakubaliana na mimi kwamba hata nyumba huwezi kuta mtu anaye jiweza anajenga kwa tofali za kuchoma! Ukija kwenye majengo makubwa nako huwezi kuta tofali ya kuchoma.

Swali ni kwamba kama tofali za kuchoma ni imara na zinakubalika kuliko za kuchoma kwann nyumba nyingi zinajengwa kwa kutumia matofali ya cement? Je hawa watu hawapendi uimara wa tofali za kuchoma mpaka watumie za cement??

Turudi kwenye hii statement yako..

===

Choma in terms of tension force iko poa zaidi ya sementi.
Ila la sementi liko poa in terms of compressive strength Ila sio tension.

=====

Mkuu uko serious kweli??
Nadhani anaejiweza atajengea tofari choma zile za viwango sio blocks wa choma kawaida.

Mimi niwe na pesa zangu naachaje kujenga kwa tofari kama hizi hapa chini?👇👇

IMG_20210424_081329_602.jpg


IMG_20210620_113722_495.jpg


IMG_20210613_114204_082.jpg
 
Tofari choma ni bora zaidi ya saruji, strength yake iko juu, nyumba inaweza kudumu miaka zaidi ya 200, kama zimechomwa kwa standard nzuri, ndo maana wenzetu uko majuu USA, Europe wanatumia sana tofari choma pia zinahifadhi joto kwa muda mrefu, uimara wa tofari choma ni sawa na tofari za zege.

Tanzanian hatuna kiwanda Cha tofari choma kipo Uganda, wengi wenye pesa uchukuwa Uganda maana standard zake ni nzuri siyo hizi za kutumia kuni, pumba za mpunga etc. Nzuri wanatumia makaa ya mawe, gas etc.
Hahahah eti standard za kuni
 
  1. matofali ya blocks yana high compressive strength than choma, sababu strength ya bloko iko prpotion to cotent ya cement where by sand,water quality ni costant sasa kadri uongezapo cement kwenye mchanga na maji strengh inaongezekaa toafuti na choma, ukiongeza poda ya vumbi kwenye paste ya tofali unaongeza plascity index ya paste then unapunguza bearing capacity ya tofali.
  2. kama hakuna magunzo ya zege kwenye structure, bloko ndo nzuri
  3. water raiser ndio hata government wanatumia bloko lakini ratio ni kali kidogo 1:3 hadi 1:4(hapo mfuko mmoja utapata tofali 9 au 10 za nch 6)
 
mimi nyumba yangu sipendi kutumia tofali za choma au blocks napenda sana mahekalu kama ya mjerumani napenda nyumba iwe kama chuma
  1. hatua ya msingi , napenda raft foundation haijalishi eneo likoje, option ya pili napenda nichimbe msingi kwenda chini 70cm -100cm , upana 60cm, then nacast chini ya msingi kwanza blinding concrete grade 15, 6cm thickness baada ya hapo najenga ukuta wa msingi kwa kutumia matofali ya zege(1:2.5:5 mix hapa unapata strength ya 17.5MPA Ambayo ni class 15 kali kidogo) hadi usawa wa juu ya ardhi, then ukuta unaenda 1M high above original ground level ili nipate ngazi 5 za veranda hata mvua ikinyesha nakuwa niko juu then naweka moramu ndani ya msingi,then mawe na fill pores za mawe kwa sand baada ya hapo nanyunyuzia dawa ya kuua wadudu altmeticn baadae naweka DPM (damp proof membrane) hilo ni kapeti laini baadae nasuka nondo y12 kuzunguka misingi mama(bearing) au yote kama na fund baadae nafunga box namwaga zege la jamvi ratio ileile 1:2:4.5 hadi hapo nakuwa na msingi imala
  2. hatua ya boma, najenga kwa tofali za zege inch 6 hadi juu ,lenta natumia zege la ratio 1:1.75:3.5 ambayo ni class 20 itakayokupa 22.5MPA Stength
  3. naezeka na araf steel truss pamoja na branderring, kwenye bati natumia roman tiles gauge 28, bodi gypsum kwa ajili ya dari
  4. skimming natumia wall putty
  5. rangi natumia weather na silk paint
  6. milango natumia mbao za mninga na vitasa natumia 3 levers au vile vya kisasa vya pasword
  7. sakafu, napenda 3d expoxy.
  8. madirisha upv slinding windows
nazani nyumba imeisha
 
Ninadhani unasababisha ubishani usio na sababu. Mtoa post aliuliza kiujumla. Na baadhi ya wachangiaji tumemjibu kuwa kama mambo yatafanyika kikanuni, kwa tofali zote, kuchoma ni namba moja. Wewe post hii ndo umeonesha kuwa kumbe unakiri la kuchoma ni kiboko mradi tu viwango viwepo. Ile hoja yako ya mwanzo hadi nikakujibu vile ni kwa vile uliongea kiujumla tu. Yani kama unafundisha basi mwanafunzi anaelewa la kuchoma halifai, na sababu ni vile huoni watu wakijengea. Hii ni dhambi aisee!

Halafu bado hoja zako si madhubuti sana. Eti za kuchoma hutumiwa na masikini. Umeipata wapi hii? wabongo baadhi kwa kutojua ama sababu za kimazingira ndo huchagua saruji. Na wanatumia matofali ya kiwango cha chini mno. tofali unakuta 1:40. ndo majengo yaliyojaa miji yetu hasa Dar na maeneo jirani. Sababu kubwa kwa hapa kwetu watu kutumia ya kuchomwa ama saruji ni mazingira. Mpaka mkazi wa Dar pale magomeni apate tofali la kuchomwa litamfikia kwa kiasi gani? Hali hii ni tofauti ukiwa Iringa. Yale majumba ya wazee vibopa wa Kikinga kule Kihesa na Gangilonga yote ni tofali za kuchomwa. Kuna nyumba zimejengwa Dar mwaka jana, lakini haziingii kwa nyumba zile aisee zenye miongo kadhaa. Kakague chuo kama Mkwawa, sekondari kama Ifunda n.k. kisha njoo utuambie ule ni umasikini ama la.

Cha ajabu, ukizungumza kuhusu saruji, unataja standard hiyo ya 1:25, na hzi za kuchomwa pia zina viwango vyake, vikifikiwa ni bora zaid ya saruji. Na wangapi bongo wanajengea tofali za 1:25? Tumuogope Mungu aisee!
Natamani unielewesha zaidi, natamani sana nyumba ya tofali za kichina, Uganda wanjengea tofali za kuchoma na ni nzuri mno,
 
  1. matofali ya blocks yana high compressive strength than choma, sababu strength ya bloko iko prpotion to cotent ya cement where by sand,water quality ni costant sasa kadri uongezapo cement kwenye mchanga na maji strengh inaongezekaa toafuti na choma, ukiongeza poda ya vumbi kwenye paste ya tofali unaongeza plascity index ya paste then unapunguza bearing capacity ya tofali.
  2. kama hakuna magunzo ya zege kwenye structure, bloko ndo nzuri
  3. water raiser ndio hata government wanatumia bloko lakini ratio ni kali kidogo 1:3 hadi 1:4(hapo mfuko mmoja utapata tofali 9 au 10 za nch 6)

Mzee 1M kwa 5steps za ngazi!? Hiyo riser na tread zitakuwa na sizes gani?
 
Tofali za kuchoma zinaleta joto kali kwenye nyumba. Zinafaa mikoa yenye ubaridi. Kwa uimara za kuchoma ni imara zaidi sema zinakula cement nyingi wakati wa kuzijenga!
Naomba kuuliza mkuu, unavyosema zinakula cement nyingi unamaanisha nini maana hata za cement pia si zinakengwa kwa kutumia cement, naomba unieleweshe napenda sana nyumba za ma tofali ya kichina hua zina vitia, na inawezekana kupiga plasta na rangi au lazima matofali yaonekane tu
 
Wacha nichangie kidogo kwenye huu mjadala. Tofali ya kuchoma ni imara; bora na inadumu zaidi ya tofali ya simenti. Tofali ya kuchoma inatokana na natural materials na binder ya hizo materials ni moto. Kitu chochote kikichomwa close to it's melting point hua particles zake zinayeyuka na kushikamanisha particles zingine lakini pia ule uji uji huziba mashimo na nyufa zote. Kwa jinsi hii tofali ya kuchoma itakua imara na kwakua imetokana na natural materials hasa mfinyanzi; majivu ya volcano ambavyo kuungua kwake kunaunda kitu kama kauri (marumaru ilivyo); tofali hili ni ngumu kushambuliwa na chumvi; kutu; unyevu; fungus, na kemikali nyingine (hii ni sifa ya fired ceramic product including tiles; firebrick, vyombo vya nyumbani; masinki).
Cha kukufrahisha ni kwamba vinu vya kuyeyushia mawe/ madini ujenzi/ limestone wakati wa kuandaa cement vimeundwa kwa tofali maalum za kuchoma zitokanazo na mchanganyiko ww udongo wa mfinyanzi na madini mengine especially Bauxite; ukizingatia kwamba ili cement hutengenezwa kwa kuyeyusha hizi materials at temperature above 1600C. Point hapa ni processing techniques tu; tofali za kuchoma tunazotengeneza sisi hapa nyumbani hatuzingatii viwango vya uzalishaji na narudi palepale kwenye processing techniques & selection of materials.
Mtu anachoma tofali bila temperature regulation maana anatumia pumba na kuni ni ngumu kujua unachoma hilo tofali kwenye temperature ipi kifikia sintering temperature ya materials ulizotumia lakini pia mfinyanzi wa eneo A hauwezi kua na chemical contents sawa so lazima ufanye chemical analysis kujua udongo wako una chemical contents zipi na je zinafanana na zile zinazotakiwa kwenye uzalishaji wa tofali lako according to recognized world standards; maana yake hapo kuna additives lazima uongeze kufikia viwango vinavyotakiwa.
Sisi hatufanyi ivyo ndo maana ni ngumu kumshawishi mtu kama tofali la kuchoma ni imara kuliko la simenti; lakini ukweli tofali za kuchoma hata gharama zake za uzalishaji ziko juu na hivyo tofali hii haiwezi kua cheap kama watu wengi wanavyofikiria; ukitaka kuamini agiza leo tofali kutoka India; China au Pakistan uone gharama zake na zinaendana na ubora wake pia; sie tunachoma matope hata shape tu ni mbovu matu atakuelewa vipi?!
Hapa ndipo umuhimu wa shule huonekana. Bravo kiongozi.
 
Back
Top Bottom