Kati ya matofali ya kuchoma na ya saruji unachagua yapi?

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
52,885
2,000
Nilibishana na rafiki yangu, yeye ameamua kujengea matofali ya kuchoma. Anasema ubora wa tofali la kuchoma liliokwa sawa sawa unazidi matofali ya saruji. Yeye pesa anayo ila ameamua kutumia matofali ya kuchoma katika ujenzi wake. Hivi ni kweli kuwa matofali ya kuchoma ni bora kuliko ya saruji?

Nilichomwambia ni kuwa, matofali ya kuchoma unauhakika ni udongo 100% kuliko upate ya saruji yawe 1/3 ni mchanga na 1/4 ni saruji. Lakini kuhusu uboara hui sina uhakika.

1627922057340.png

Matofali ya kuchoma

1627922242801.png

Matofali ya saruji

Kokolo

JF-Expert Member
Mar 20, 2008
1,211
2,000
Tofari choma ni bora zaidi ya saruji, strength yake iko juu, nyumba inaweza kudumu miaka zaidi ya 200, kama zimechomwa kwa standard nzuri, ndo maana wenzetu uko majuu USA, Europe wanatumia sana tofari choma pia zinahifadhi joto kwa muda mrefu, uimara wa tofari choma ni sawa na tofari za zege.

Tanzanian hatuna kiwanda Cha tofari choma kipo Uganda, wengi wenye pesa uchukuwa Uganda maana standard zake ni nzuri siyo hizi za kutumia kuni, pumba za mpunga etc. Nzuri wanatumia makaa ya mawe, gas etc.
 
Wang Shu

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
2,529
2,000
Kwa life expectancy ya Tz na kipato cha kududuliza usihangaike kujengea tofali za kuchoma ni imara zaidi lakini inaitaji ukamilishe kila kitu unapoanza kujengea.

Tunaishi miaka isiyozidi 90 ukibahatika ujenzi wa wengi leo msingi mwakani boma mwaka kesho kutwa kupaua za saruji ni rafiki kwa hilo utaishi utakufa mwanao atarithi nae atakufa atarithi mjuu wako pia.
 
Mtafiti77

JF-Expert Member
Oct 31, 2011
1,527
2,000
Nilibishana na rafiki yangu, yeye ameamua kujengea matofali ya kuchoma. Anasema ubora wa tofali la kuchoma liliokwa sawasawa unazidi matofali ya saruji. Yeye pesa anayo ila ameamua kutumia matofali ya kuchoma katika ujenzi wake. Hivi ni kweli kuwa matofali ya kuchoma ni bora kuliko ya saruji?

Nilichomwambia ni kuwa, matofali ya kuchoma unauhakika ni udongo 100% kuliko upate ya saruji yawe 1/3 ni mchanga na 1/4 ni saruji. Lakini kuhusu uboara hui sina uhakika.
Kwa ujumla, tofali za kuchoma ni imara zaidi kuliko zile za saruji. Hata hivyo, kwa hapa kwetu ni vigumu kulitambua hili mpaka uwe mtafiti ama mtaalamu wa masuala haya ya ujenzi. Mazingira ya ujenzi wetu hayana viwango. Kwahiyo, ni vigumu wewe kuona ubora wa tofali maana si saruji wala la kuchoma linalotengenezwa kwa kufuata viwango. Tena bora wazee wetu miaka ya 90 mwanzoni kurudi nyuma walifuata viwango, sisi wa miaka hii tuwe wakweli, hakuna kitu. Mradi tumehamia.

Tukifuata viwango, la kuchoma ni funika bovu. Linaweza kudumu hata miaka 300. Tazama waliotutangulia kule Ulaya. Miji yote mikongwe imejengwa kwa matofali ya kuchoma. Kuna majengo yapo kwa zaidi ya karne na hadi leo unayapenda. Aidha, usione tofali kwa macho tu, huwa zinatofautiana wapi zinatumika.

Mfano, ukijenga daraja kuna tofali zake, jengo la kuishi kuna tofali zake n.k. So, ukitaka uthibitisho, hakikisha matofali yako yanafuata viwango vyote, kuanzia aina ya udongo, vipimo, tanuru, moto unaotumika n.k. Sasa niambie, ni nani anafuata masharti haya? Akina sisi kuna tofali ya kuchoma unajenga, mvua ikipiga inamomonyoka. Mkeo akiwa mjamzito anayamaliza kwa kuyabwia.

Ukiona hivi, huna tofali hapo. Tofali la kuchoma sawia ukiligonga kwa sarafu linalia kama chuma. Kama kimalkia kinapanda soma makala haya hapa chini kuongeza maarifa:

Amina
 
Mtafiti77

JF-Expert Member
Oct 31, 2011
1,527
2,000
Mtindo huu wa tofali ndio ninao ukubali zaidi View attachment 1866032 View attachment 1866034
Hawa watu wana nidhamu mkuu. Sisi wazee wa mradi liende. Wanafuata viwango. Mfano hizo zimelazwa hapo ardhini uimara wake ni mkubwa zaidi kuliko zile zinajenga nyumba.

Wanazitofautisha kwa nyuzi joto kule kiwandani. Sasa tazama hivi vyetu vya saruji (maarufu pavement blocks), eti vinawekwa leo, mwakani vinamomonyoka.

Vinaisha kama pipi. Nashangazwa eti wanaviparaza layer fulani ya rangi kwa juu, wala haikai. Sisi utani mwingi sana! Hiyo mijengo hapo pichani ukute walijenga baba wa babu yake Trump! Kudaaadenye!
 
Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
52,885
2,000
Kwa ujumla, tofali za kuchoma ni imara zaidi kuliko zile za saruji. Hata hivyo, kwa hapa kwetu ni vigumu kulitambua hili mpaka uwe mtafiti ama mtaalamu wa masuala haya ya ujenzi...
Ni kwasababu hatuna utaalamu mzuri wa kuoka matofali. Ulaya wanatumia matanuri ya gas na wanaoka kwa wingi kibiashara.

Kuna Mwarabu mmoja hapa kwetu ni mshika dini sana, yeye anafuata ratio ya 30:1 bag katika matofali ya saruji. Kwa kununua huyu anaaminika na matofali yake yananunuliwa sana.
 
Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
23,487
2,000
Nilibishana na rafiki yangu, yeye ameamua kujengea matofali ya kuchoma. Anasema ubora wa tofali la kuchoma liliokwa sawasawa unazidi matofali ya saruji. Yeye pesa anayo ila ameamua kutumia matofali ya kuchoma katika ujenzi wake. Hivi ni kweli kuwa matofali ya kuchoma ni bora kuliko ya saruji?

Nilichomwambia ni kuwa, matofali ya kuchoma unauhakika ni udongo 100% kuliko upate ya saruji yawe 1/3 ni mchanga na 1/4 ni saruji. Lakini kuhusu uboara hui sina uhakika.
Kumaliza ubishi yapelekeni maabara yakakandamizwe ijulikane yanavunjikia kwenye NEWTON'S ngapi
 
Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
23,487
2,000
Changamoto ni kuwa haya ya saruji unanunua matofali, mchanga na mashine. Fundi na amepata pa kuponea anakupiga humohumo anatoa matofali 45 kwa mfuko wa saruji na anakuambia mfuko mmoja ametoa 25
Ndo hapo sasa... Ila kuna wauzaji, matofali yao yanaaminika na maabara za pale DIT.. Kwa Dar, nawafahamu jamaa wapo pale kabla ya daraja la mto mzinga kushoto kama utakwenda Vikindu
 
King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
43,083
2,000
Ukijenga kwa satandard zote ni imara ila zikitengenezwa kwa kubumba lazima zitakuwa za hovyo! sasa mtu tofali za saruji unatoa tofali 45 hadi 50 unategemea kweli zitakuwa nzuri? Jaribu kutoa 30 au 25 uone zitakavyotoka kama chuma!!
 
Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
17,430
2,000
Tofari choma ni bora zaidi ya saruji, strength yake iko juu, nyumba inaweza kudumu miaka zaidi ya 200, kama zimechomwa kwa standard nzuri, ndo maana wenzetu uko majuu USA, Europe wanatumia sana tofari choma pia zinahifadhi joto kwa muda mrefu, uimara wa tofari choma ni sawa na tofari za zege.

Tanzanian hatuna kiwanda Cha tofari choma kipo Uganda, wengi wenye pesa uchukuwa Uganda maana standard zake ni nzuri siyo hizi za kutumia kuni, pumba za mpunga etc. Nzuri wanatumia makaa ya mawe, gas etc.
Tofali ya kuchoma ina nguvu kuliko ya cement? Aisee!

Hivi ushawahi kuona ghorofa linajengwa kwa tofali ya kuchoma?

Ukijibu hilo pia jibu hili..

Kwanini kwenye structures kama matenki ya maji wanatumia tofali za cement na sio tofali udongo??
 
COMOTANG

JF-Expert Member
Jan 6, 2021
1,743

Mkuu tofali ya block Ni imara kuliko ya kuchoma lakini sio Kama ndo HAKUNA MAGHOROFA YA TOFALI ZA KUCHOMA !
Yapo AREA C DODOMA MAGHOROFA ya tofali za kuchoma
 
COMOTANG

JF-Expert Member
Jan 6, 2021
1,743
2,000
Tofali ya kuchoma ina nguvu kuliko ya cement? Aisee!

Hivi ushawahi kuona ghorofa linajengwa kwa tofali ya kuchoma?

Ukijibu hilo pia jibu hili..

Kwanini kwenye structures kama matenki ya maji wanatumia tofali za cement na sio tofali udongo??
Kwasababu tofali za kuchoma hunyonya maji au unyevu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom