Kati ya Marais watatu wastaafu wa Tanzania, nani ni Rais bora na kwanini?

MTV MBONGO

JF-Expert Member
Feb 18, 2016
1,262
1,220
WanaJF habari zenu! Mwl. Nyerere katawala nchi yetu kama miaka 23 hivi. Mtukufu Mwinyi, Mh. Mkapa na Mh. Kikwete wametawala miaka kumi kila mmoja. Ni rais gani kwako unamuona ni bora zaidi ya wengine? toa na sababu ktk hilo. tazama:
1. Ukuaji wa uchumi
2. Umoja wa Watz
3. Amani na usalama
4. Demokrasia
5. Haki na uhuru wa mahakama
6. uhuru wa kutoa maoni na kusikilizwa
7. upambanaji wa rushwa hasa kubwa
8. n.k
 
No more than JULIUS KAMBARAGE NYERERE. Kikwete ni number 2. Huyu wa sasa, tumuombee Mungu Kama anavyotuomba. Hali itakuwa mbaya sana huko tuendako. Nchi hutawaliwa kwa mujibu wa katiba. Maneno yake hayawezi kuwa ndiyo katiba ya Watanzania. Namuonea huruma coz, amepotea kabisa. Time will gonna answer.
 
Ukawa wanaisoma Namba .

Wanakalia kujiziba makaratasi hawapo bungeni wala jimboni ,huku ccm ikihudumia wananchi .

Uchaguzi ukifika wanaimba ule wimbo maarufu wa tumeibiwa kura .!!

Hapa Kazi Tu
 
Mwl Nyerere
Anaongoza kwny no.2 na 7
Mzee Mwinyi
3 na 4
Mkapa
1
Kikwete
5 na 6
 
Mpaka sasa naona kama Beni yuko juu...aliweka miundo mbini mingi sana ya kiuchumi
 
Mleta mada pia ungeweka na udhaifu wao sababu hakuna ubora pasipo na udhaifu , kwa muelekeo huo tungewachambua vilivyo kila mmoja udhaifu aliokuwa nao katika utawala wake na jinsi Rais mwingine alivyokuwa bora dhidi ya udhaifu wa mtawala aliyemtangulia , ni kanuni hakuna ubora pasipo na udhaifu" ukisema ubora pekee ni ngumu kila mmoja kamzidi mwenzie sehemu fulani katika utawala wake
 
Kila mmoja kwa nafasi yake.,.. lkn hakuna hata mmoja maana pamoja nakufanya makosa hakuna aliejitokeza kuomba ahukumiwe kutokana na makosa yake. Uungwana ni vitendo!
 
Ukawa wanaisoma Namba .

Wanakalia kujiziba makaratasi hawapo bungeni wala jimboni ,huku ccm ikihudumia wananchi .

Uchaguzi ukifika wanaimba ule wimbo maarufu wa tumeibiwa kura .!!

Hapa Kazi Tu
Spidi ya JPM ni shida, mpaka watu wazima wanavaa imoji za shut up!! Si mchezo.
 
Kwa kuzingatia mazingira ya wakati na siasa za ulimwengu kwa miaka hiyo, hakuna hata mmoja wa kumkaribia Mwalimu.

1. Mwalimu angetaka angeweza kuwa Rais mpaka kifo chake. Aliacha kwa hiari yake. Ndiye alisisitiza sana kufuata katiba na sheria. Ndiye alilazimisha kuwepo na mfumo wa vyama vingi na ukomo wa Urais hata kama watu bado wanakupenda

2. Kiuchumi tulikwenda vizuri mpaka mwaka 1978. Vita na Uganda ndiyo iliyoharibu uchumi. Vita naambiwa ilikuwa inakula dola 40m kwa siku.

3. Mwalimu alikuwa anajua kuwa hakuna maendeleo bila ya utafiti. Ndiye aliyeanzisha vituo vyote vya utafiti

4. Alijenga viwanda karibia vya bidha zote muhimu mpaka vya kuunganisha malori na matrekta

5. Vyuo vya certificates, diploma mpaka vyuo vikuu

6. Hospitali karibia zote kubwa zilijengwa wakati wa Mwalimu

Anayefuatia, naamini ni Kikwete

Ni ngumu sana kutoa nafasi ya Magufuli. Magufuli ana sifa mbili kubwa, ya ujasiri na uwezo wa kusimamia. Anahitaji sana umakini na ushauri wa kutambua njia zilizo bora za kufikia matamanio yake. Nasema matamanio na siyo mipango. Naona zaidi ana matamanio lakini njia sahihi za kufikia matamanio yake, nina mashaka sana kama anazitambua.
 
Kama Lowassa angekuwa PM kwa kipindi chote cha JK basi leo hii Kikwete angekuwa one of the best President kando ya JK Nyerere.
 
Jakaya
WanaJF habari zenu! Mwl. Nyerere katawala nchi yetu kama miaka 23 hivi. Mtukufu Mwinyi, Mh. Mkapa na Mh. Kikwete wametawala miaka kumi kila mmoja. Ni rais gani kwako unamuona ni bora zaidi ya wengine? toa na sababu ktk hilo. tazama:
1. Ukuaji wa uchumi
2. Umoja wa Watz
3. Amani na usalama
4. Demokrasia
5. Haki na uhuru wa mahakama
6. uhuru wa kutoa maoni na kusikilizwa
7. upambanaji wa rushwa hasa kubwa
8. n.k
Kikwete
 
Back
Top Bottom