Kati ya Mama na Mke nani anastahili zaidi ya 50% ya mapenzi

2019

JF-Expert Member
Dec 31, 2018
2,982
4,457
Kwanza kabisa tuelewe majukumu ya hawa watu katika sekta zao. Heshima ya Mama haipungui kijana unapooa.

Tunajua umuhimu wa Mama toka amekubeba miezi 9 umezaliwa umekuwa na umejitambua hilo ni jukumu lake na lazima apate heahima kama Mungu alivyoagiza.

Umejitambua unataka sasa kujitegemea,umeanzisha Familia yani umeoa tunajua umuhimu wa Mke. Mke anaendeleza majukumu ya Mama alipoishia tena yakiongezeka mengine mengi zaidi. Kumbuka Mke ni ubavu wako,tukifuata kile Mungu alituambia hatuwezi kulelewa na Mama mpaka kufa kwetu.

Kulingana na migogoro ya kifamilia ya kileo ni nani anastahili upendo zaidi baada ya kujana kuoa?

Ukimpenda sana Mke wako Mama anaona umemtenga baada ya kuoa na huenda akahisi Mke ndio anafanya usimthamini kama mwanzo. Ukimpenda sana Mama Mke anaona ameporwa madaraka na Mama na anaona Mama anataka kumharibia ndoa.

Leo la mada hii ni kila muhusika kujua mipaka yake na kuepuka migogoro isiyo ya lazima.

Binafsi ukishaoa lazima mapenzi yapungue kwa Mama sababu ya majukumu ambayo Mama hawezi kukutimizia tena kwa hiyo

Mama 40% Mke 60%

Karibuni wajumbe
 
Mkuu ...mapenzi ya mama na mapenzi ya mke,,
Tofauti kama mbingu na ardhi.

Tusidanganyane humu..
Umeoa mtoto mbichi unampenda sana,,
Tena ndoa bado changa.
hizo nguvu za kuhimili hayo utazitoa wapi?
  • wanaume waliogombana na mama zao kisa mke ni wengi sana.
  • kuliko wanaume waliogombana na wake zao sababu ya mama...
 
Kwanza kabisa swali lako si sahihi sababu halikai kati ya wawili hao. Nini namaanisha kila mmoja ana nafasi yake na umuhimu wake na haki zake kutoka kwa sisi watoto na sisi waume.

Majibu ya swali lako hili kwa usahihi wake japo swali lako si stahiki, ni kuonyesha unachotakiwa kumfanyia mzazi wako katika wema na mke wako kadhalika katika wema, na majibu ya maswali haya hupatikana katikana katika dini.

Ngoja niendelee.

1.Nafasi ya mama kwa mtoto wake.
2. Nafasi ya mume kwa mke wake.

Narudi kuendelea....
 
wapende kulingana na nafasi zao.. vinginevyo utaharibu mambo hususan ukizidisha upendo kokote.. mwisho kama hujaoa, oa mwanamke atakaekua anapatana vizuri na mamaako.
 
Mama si ana Mme wake ambaye ni baba? Akapate mapenzi huko, kama ni single maza atajiju! Kila mtu apate mapenzi kwa mpenziwe!
Uko sahihi kabisa ila mama atapata mapenzi kiasi ila hayatalingana na mke
 
Mkuu ...mapenzi ya mama na mapenzi ya mke,,
Tofauti kama mbingu na ardhi.

Tusidanganyane humu..
Umeoa mtoto mbichi unampenda sana,,
Tena ndoa bado changa.
hizo nguvu za kuhimili hayo utazitoa wapi?
  • wanaume waliogombana na mama zao kisa mke ni wengi sana.
  • kuliko wanaume waliogombana na wake zao sababu ya mama...
Viwe vichache au vingi lengo ni kujua mipaka tu
 
ukitaka kupata jibu nenda kamuulize bibi ako, kati ya baba ako na babu yako nani anampenda sana . ukishapata jibu ndio ujue nani umpende zaidi
 
Mke siyo ndugu yako mkuu.. ukiumwa tu aamue kubaki au kusonga lakin mama ako atakupgania hadi mwisho
Huyo mke utakuwa umemwokota ila hujafunga nae ndoa na kuamua kuungana...mke sahihi hawez kukuacha.
Mamako anaweza kukuogesha?
 
Nataka mawazo/msimamo wako siyo ya mtu
ukitaka kupata jibu nenda kamuulize bibi ako, kati ya baba ako na babu yako nani anampenda sana . ukishapata jibu ndio ujue nani umpende zaidi
 
Back
Top Bottom