Kati ya Mama mzazi na mke/mume nani utakaemjali?

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Aug 1, 2014
2,517
2,945
Habari wanazengo!

Natumai nyote ni wazima wa afya naomba leo tuweze kujadili hii mada ndogo ambayo tuliweza kujibizana na watu lakin bado hatujapata majibu kamili labda hapa huwenda ikawa sehem sahihi.

Ila mada hii tuiangazie kwa upande wa upendo lakin si peiority kwa mzazi I I mean labda mfano imetokea ajali ambapo kwenye ajali hiyo yupo mzazi wako ambae ni Mama pamoja na mke wako au Mume wako je yupi wa kwanza kumuokoa na option ni moja ya kuchagua?

Narudia tena pindi utakapo jibu utoe jibu la msingi labda una muokoa mama kwanini mama? Then unamuokoa mke /mume why.

Shukrani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mama yangu ameshapumzika kwa amani, hii Hainihusu. Nitamkumbuka Daima
IMG-20181125-WA0002.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kitu kizuri cha kuzingatia ni kwamba wachangiaji wa humu hatufanani historia zetu, wewe ambae umelelewa vyema na mama yako, usijilinganishe na yule aliyetupwa mtaroni na mama yake mara tu alipozaliwa, au yule ambae aliona kabisa kati yake na ndugu zake aliozaliwa nao tumbo moja, mama yake alichagua kuwapenda zaidi hao wengine kuliko yeye, na hata michango yake ndani ya nyumba haithaminiki, mfano atawanunulia sofa set ndani ya nyumba lakini hakuna appreciation, ila ndugu yake akinunua saa ya ukutani, kila mgeni atakae ingia hapo ndani ataambiwa ile saa kanunua fulani, ni bora asingekuwa mama huyo anasema kabisa, lakin kitendo cha namna hiyo kinapunguza upendo wa mtoto kwa mzazi. Kwahiyo linapokuja eneo la nani wa kumsaidia kwanza, tusishangaane, kwakuwa ulivyotendewa na mama yako sivyo nilivyotendewa na mama yangu.

Unaposikia kuna matukio ya ukatili dhidi ya wanawake, asilimia kubwa ya wanaume wanaofanya matukio hayo ukifuatilia historia zao utagundua hawakupata upendo wa mwanamke wakiwa wadogo, iwe alilelewa na bibi, mama, shangazi au dada, so matokeo ya ukatili wowote anaofanyiwa mwanamke na mwanaume ni zao la chuki kutoka kwa mwanamke mwenzake.
 
Back
Top Bottom