Kati ya mabango yaliyopita kwenye Mei Mosi, ni kwanini hakuna hata bango, lililokemea ufisadi mkubwa uliofanywa Serikalini wa mabilioni ya shilingi?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,477
30,137
Nimeyaangalia mabango yote, yaliyobebwa na wafanyakazi, yaliyopita mbele ya mgeni wa heshima, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, sikuona hata bango moja, lililokemea vikali ufisadi mkubwa uliofichuliwa na CAG, Charles Kicheere, wa ufujaji wa mabilioni ya shilingi za pesa za walipa kodi wa nchi hii.

Nimeona mabango Karibu yote, yakihimiza maslahi bora kwa wafanyakazi, ikiwemo kuongeza kima cha chini cha mshahara.

Ni jambo la kushangaza, kuona Katika wafanyakazi wote wa nchi hii, hakuna mfanyakazi yeyote aliyekerwa na ufisadi mkubwa uliofanywa na baadhi ya watumishi wachache wa Umma!

Hivi wafanyakazi, wanajua kweli madhara yaliyofanywa na watendaji hao wachache kuiba mabilioni ya shilingi ya walipa kodi wa nchi hii?

Hivi wafanyakazi wanajua kuwa kama siyo ubadhiifu mkubwa unaoendelea kufanywa huko Serikalini, wangweza kulipwa maslahi bora, hata kwa kima kilichopendekezwa na TUCTA cha shilingi milioni moja kwa mwezi??

Hata kauli mbiu ya mwaka huu, MISHAHARA NA MASLAHi BORA YA WAFANYAKAZI NDIYO KILIO CHETU, haikuweza kutumizwa na Rais kwa sababu ya ubadhirifu mkubwa uliotokea Serikalini.

Swali tunalojiuliza wananchi wa nchi hii, je ufisadi mkubwa unaofanywa huko Serikalini, una baraka ya uongozi wa juu wa hapa nchini?
 
Kila mtu anapambania kibuyu chake cha asali.
Lakini ni jambo linaloshangaza kuona wafanyakazi mamilioni wa nchi hii, hakuna hata mfanyakazi mmoja, aliyeona umuhimu wa kukemea ufisadi mkubwa unaofanywa huko Serikalini!
 
hii ndo nchi ya WADANGANYIKA!!!

mpaka siku damu zitoke masiikioni ndo wataamua kuchoka na hii FISIEMU
Swali tunalojiuliza, je TUCTA ina ubia na watawala wa CCM?

Tunapata ushahidi kwa kauli iliyotolewa na Rais wa TUCTA, Nyamuhokya, kuwa wafanyakazi wa nchi hii, watahakikisha kuwa Rais Samia anaendelea kuliongoza Taifa hili baada ya kipindi chake hiki kuisha mwaka 2025!
 
CCM Ikiondoka mabango ya kukemea Ufisadi yataonekana.

Ni ilani za Kidikteta za CCM na vibaraka wake ndizo zinafinya mawazo halisi juu ya Ufisadi.

CCM isiyo na Demokrasia ndani ya chama inawezaje kuachia mabango ya kulaani Ufisadi unaofanywa na wanachama wake wanaohodhi madaraka katika kila kona za dola? Inawezaje kuacha Demokrasia ishamiri wakati miongoni mwao hilo halitelekezeki?
 
Kuna kujipendekeza ambako kunagharimu maisha ya watu wengi. Ishu ya mabango ni kama iliratibiwa na serikali.
Absolutely true

Hata ukiaangalia namna ya uandishi wa hayo mabango yenyewe ni kama yaliratibiwa na kuwa "edited" na mtu mmoja, na huyo si mwingine, bali mkuu wa Mkoa wa Dom!
 
Back
Top Bottom