Kati ya mabanga ya matangazo na magari yaliyotelekezwa barabarani, kipi hatari zaidi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kati ya mabanga ya matangazo na magari yaliyotelekezwa barabarani, kipi hatari zaidi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jatropha, Feb 23, 2011.

 1. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #1
  Feb 23, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Kanuni za Sheria ya barabara namba 13 ya 2007, zilizopitishwa kupitia Tangazo la Serikali namba 21 la Tar 23 Januari 2009 katika Ibara ya 9 (1-10) inaipa TANROAD mamlaka ya kuondosha magari yaliyoharibika au kutelekezwa barabarani kwa zaidi ya masaa 6 kwa maeneo ya mijini na masaa 24 katika maeno ya vijijini.
  Kutokana na TANROAD kushindwa kutekelza jukumu hilo kwa mujibu wa Kanuni zake yenyewe, idadi ya vifo vinavyotokana na ajali za barabarani hususan zile zinazosababishwa na magari yaliyoharibika na kutelekezwa zinazidi mkuongezeka kila mwaka kiasi cha kukimbizana na idadi ya vifo visababishwavyo na Malaria na Ukimwi.
  Hali inashangaza kwa sababu Waziri wa Wizara ya Miundo Mbinu Mhe John Magufuli na TANROAD kila siku wanajigamba kuwa wanahakikisha kuwa sheria za barabara na Kanuni zake zinatekelezwa kwa 100% hata kama ni kwa kuwabomolea wananchi wasio na hatia.
  Kwani kununua magari ya breakdown yenye uwezo wa kuvuta magari makubwa na madogo yaliyoharibika barabarani kwa kila mkoa hapa nchini ni shilingi ngapi ikilinganishwa na idadi ya vifo vinavyosababishwa na magari yanaharibika na kutelekezwa barabarani? TANROAD si inapata fedha kutoka mfuko wa barabara ambao kila mwananachi anaponunua mafuta ya magari huchangia.
  Ina maana kauli za Mhe John Magufuli kuwa "nimeapa kutii na kulinda sheria", "sitaki sheria za barabara kuchezewa" ni kiini macho tu na anazitumia ili kujitafutia umaarufu kwa kuwabomolea wananchi wanyonge na maskini nyumba zao bila ya kuwalipa fidia kama walivyofanya mradi wa mabasi yaendayo kasi (DART) 2008, ili atimize malengo yake ya kugombea urais 2015 tu?
   
 2. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Koote umepatia hapo tu ndio unaleta walakin labda utoe uthibitisho, maana wewe unaweza kuwa unataka kumchafua Magufuri kwa lengo la kujiwekea mazingira 2055.
   
 3. d

  darnessta Member

  #3
  Feb 23, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo ndugu yangu umesema kweli, mimi ni dereva wa magari makubwa, kutokana na kusafiri mara kwa mara nafahamu ukubwa watatizo hili na magari yaliyoharibika na kutelekezwa barabarani linavyosababisha ajali na vifo karibu kila siku. Cha kushangaza hakuna mamlaka yoyote inayoonekana kuchukua hatua zozozte kunusuru maisha ya wanachi wanaokufa bure kila siku kutokana na magari yanayoharibika na kuwekewa majani na matawi ya miti na kukaa barabarani kwa muda kati ya wiki hata mwezi mzima.

  Nchi za jirani, asasi kama TANROAD zinz mabreakdown yake ambayo huondoa magari ya aina hiyo mara moja ili kuepusha ajali. Na mmiliki wa gari husika kutakiw akulipa gharama za kuondosha gari hilo lilipokuwa na utunzanji wake. Gharama hizo huwa ni kubwa kiasi cha mmagari mengine kunadiwa na yanayoonekana mabuvu kutoruhusiwa kurudi barabarani.


  Kulingana na ukubwa wa taizo lenyewe, yaani idadi ya ajali zinzosababishwa na magari ya aina hii na vifo, napendekeza Mhe John Magufuli ahahirishe kila kitu ikiwemo mabango ya matangazo na hao wanaoishi pembeni mwa barabara na aanze kwanza na tatizo hili kuwa kuwa hayo hayamaliz watu katika barabara zake.
   
Loading...