Kati ya kura anazozitarajia kikwete asihesabie na ya baba ................. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kati ya kura anazozitarajia kikwete asihesabie na ya baba .................

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ng'wanangwa, Oct 5, 2010.

 1. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Jana nilipata "network". Nikazungumza na baba yangu mzazi anayeishi kata ambako msafara wa kikwete uliwahi kupigwa mawe.

  Nikamuambia mwaka huu tunataka mabadiliko. Aachane na mambo yake ya zamani ya "chama kimetulea". Nikamsisitizia kuwa Nyerere alisha kufa. CCM siyo ile ya Nyerere iliyokuwa inawajali wananchi. CCM ya leo ni ya matajiri, mabepari, wanyonyaji, mafisadi.

  Akaniuliza: "Sasa unataka nini we mtoto?"

  Nikamjibu: Chagua Dr. Slaa.

  Akauliza swali jingine (lililoniacha hoi): "Eti huku kijijini tunaambiwa Kikwete anaweza kupambana na Obama?".

  Nilicheka nusura nipaliwe na Valeur.

  Kucheka kwangu tu kulitosha kumpa ujumbe kuwa jibu la swali lake ni HAPANA!

  (maana ya swali lake ni kuwa, kama JK anaweza kupambana na Obama, itakuwa Slaa. huo ndiyo uzushi ulioko kijijini kwa baba. na ndiyo sera za CCM hizo")

  Mwisho nikamwambia: Vaa fulana zao, vaa kofia zao, kunywa pombe zao, kula pesa yao. Siku ya kura kamchague Dr. Slaa. Waambie na wazee wenzio unaokunywa nao pombe. Kiulaiini faza akakubali.

  Jamani tutafute network. Tuwatangazie ndugu zetu vijijini habari njema ya mabadiliko. Wakati ni huu. Muda uliobaki ni mwingi sana.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Only one vote makes a difference!
  Nakusifu sana kwa kuokoa hiyo kura moja ya Mzazi wetu iliyokuwa inapotea bure kwa kulishwa habari za siasa nyepesi(kama babayetu Kakobe) anavyosema!
  Kila mtu na ajaribu kuwasiliana na wazazi wake!
  Mimi sofar nishawabadili majirani wasiopungua 8 waliokuwa na msimamo mkali wa ccemu!
   
Loading...