denooJ
JF-Expert Member
- Mar 31, 2020
- 18,512
- 68,141
Hapo naona badala ya kusema "nadhani" jibu la haya yote lipo kwa wananchi kuondoa the entire political system waweke mfumo wao, ungetakiwa kuandika "naamini"Now, this is certainly a calm response from you that can be discussed rationaly.
Siwezi kamwe kuwatetea wapinzani kwamba hawafanyi/hawajawahi kufanya makosa, kuna sehemu mbalimbali wamefanya makosa, pengine hata mengine yanayotokana na kukosa uzoefu.
Lakini kuwalaumu kwa kushindwa kwao kwa mfano kutetea viti vyao vya ubunge katika uchaguzi mkuu kama ule uliofanyika 2020, hapo ni kuwaonea kuliko wazi kabisa.
Wapinzani wamefanyiwa bugdha, nyingi tu, hata za kuwanyima haki ya kufanya siasa, haya nayo walaumiwe wao kutoweza kutumia wale wabunge wachache waliokuwa nao bungeni kuongeza wingi wao? Huko bungeni kwenyewe, chini ya uongozi wa Ndugai na huyu binti sasa anayekalia kiti cha spika, hukuwahi kuona jinsi walivyokuwa wakitendewa humo ndani?
Hao wabunge waliokuwa wakinunuliwa kutoka upinzani, nako tuseme ni upinzani ulioshindwa kuwasimamia wabunge wake?
All in all, haya yote tunayoyasema hapa ni mfano mzuri unaoonyesha kwamba hata hiyo "Tume Huru" kwa muujiza ingetokea kuwepo, mfumo unaoendeshwa na CCM usingeruhusu hiyo tume ifanye kazi inavyotakiwa.
Kwa hiyo, jibu si kuwepo kwa "Tume Huru" kutakakoongeza wabunge upande wa upinzani, halafu wabunge hao ndio wasimamie kutengeneza Katiba Mpya.
Na kwa kweli nasita hata kusema kuwa uwepo wa Katiba Mpya 'per se' ndiko kutakakoondoa mfumo mbovu unaoilinda CCM kuendelea kuvuruga nchi.
Nadhani jibu la haya yote lipo kwa wananchi kuamua ku-overhaul the entire system. Kuung'oa kabisa mfumo huu mbovu na miziz yake yote, halafu tutengeneze Katiba Mpya, na matokeo yake yawe kupatikana kwa Tume Huru ya uchaguzi.
Ni wananchi pekee, ndio wenye uwezo huo, lakini wawe na elimu ya kutosha katika eneo hili, na pawepo na uongozi thabiti wa kuwaongoza kuikamilisha shughuli hii muhimu sana kwa taifa letu wakati huu.
CCM hataki kabisa mabadiliko haya, na katika kukataa huko, tunaona wanavyohangaika na hizi mbinu mpya za kuwalaghai watu, ikiwa ni pamoja na baadhi ya viongozi wa upinzani.
Hiyo ndio solution itakayoondoa kutoaminiana kulikojaa kwenye vichwa vya wanasiasa, wakiachwa peke yao waitafute Katiba Mpya kwa kuteua wajumbe wa bunge la Katiba tutakuwa tunadanganyana.
Hiyo move itakufa kama ilivyokufa ile ya mwanzo, political interest zitawateka matokeo yake wasahau mahitaji ya wananchi waangalie mahitaji ya vyama vyao hasa kushika madaraka (Urais, ubunge nk)
Hivyo kwa maoni yangu, suala la Katiba Mpya ni lazima waachiwe wananchi, wateuliwe viongozi wengine (wajumbe) na wananchi kutoka makundi mbalimbali ambao hawatakuwa na vinasaba na chama chochote cha siasa ili kuondoa dhana ya kutoaminiana.
Lakini tukianza tena CCM walete wajumbe wao, upinzani nao wapeleke wajumbe wao, halafu ipigwe kura ya kumchagua spika mwanasiasa ambae wajumbe wengi wa chama chake watampa kura, hapo tutakuwa tunafeli kila siku, hiyo Katiba Mpya haitakaa ipatikane.