Kati ya Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi kipi kianze?

SOPINTO

Senior Member
Oct 19, 2020
155
385
Vyama vya upinzani nchini Tanzania kwa kipindi kirefu vimekuwa na madai mbalimbali yanayousiana na suala zima la chaguzi za kisiasa , madai haya yamekuwa yakibadilika badilika kulingana na serikali iliyopo madarakani.

Hapo awali kulikuwa na vuguvugu kubwa la kudai tume huru ya uchaguzi, vuguvugu hili limedumu kwa kipindi kirefu bila mafanikio.

Hivi karibuni kumeibuka tena harakati za madai ya Katiba Mpya, kwasasa kila kona ya jamii yenye kufuatilia mambo ya kisiasa inadai katiba mpya sasa niulize kati ya Tume Huru au Katiba Mpya kipi kianze?
 
Katiba Mpya yenye Tume huru na vingine vyote ndani yake, hili swali la kimtego litasababisha kuwaondoa watu kwenye reli kwa kila mmoja kusema kianze atakachotaka yeye.
 
Ile iliyopitishwa ilikuwa na mapungifu GANI? Kwanini waliisusia? Maana kazi ingekuwa ndogo kuweka MABADILIKO kidogokidogo.
 
Vyama vya upinzani nchini Tanzania kwa kipindi kirefu vimekuwa na madai mbalimbali yanayousiana na swala zima la chaguzi za kisiasa , madai haya yamekuwa yakibadilika badilika kulingana na serikali iliyopo madarakani...
Vyote huenda pamoja!Katiba mpya inabeba ndani Tume Huru.
 
Vyama vya upinzani nchini Tanzania kwa kipindi kirefu vimekuwa na madai mbalimbali yanayousiana na suala zima la chaguzi za kisiasa , madai haya yamekuwa yakibadilika badilika kulingana na serikali iliyopo madarakani...
Muundo wa Tume ya Uchaguzi ni sehemu ya katiba ya nchi. Siyo vitu viwili tofauti. "it is only a naive person that separates the two".
 
Back
Top Bottom