Kati ya JWTZ na JKT, jeshi lipi bora zaidi?

michael western

JF-Expert Member
May 7, 2014
545
0
Haya majeshi makubwa nchini Tanzania ni jeshi lipi linamzidi mwenzake kiujuzi,mazoezi,kuwa na wasomi wengi,mishahara,na mengineyo!

Je vyeo vyao vinafanana?

Je kwa maswala ya mafunzo wanaingiliana kama wataalam wa JWTZ kufundisha kwenye JKT na wa JKT kufundisha JWTZ?

Ni jeshi gani hapo lina silaha za maana zaidi kuliko mwenzake na kupewa kipaumbele?

Wenye ufahamu kuhusu hili naomba tujadili!
 
Elly B

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
1,194
1,195
Hawa majamaa nani anamzidi mwenzake kiujuzi,mazoezi,kuwa na wasomi wengi,mishahara,na mengineyo!

Je vyeo vyao vinafanana?Je kwa maswala ya mafunzo wanaingiliana kama wataalam wa JWTz kufundisha kwenye JKT na wa JKT kufundisha JWTz.

Ni jeshi gani hapo lina silaha za maana zaidi kuliko mwenzake na kupewa kipaombele??

Wenye ufahamu kuhusu hili naomba tujadili!

**JWTZ ndiyo walioanzisha mafunzo ya JKT na ndiyo wanaofundisha mpaka leo.(Directly and indirectly)

**JKT imegawanyika katika makundi mawili. 1. Viongozi, walimu na wakufunzi, 2. Wanafunzi (servicemen)

**Viongozi wote wa JKT lazima wapitie mafunzo ya depo za kawaida za JWTZ

**JKT (servicemen) hawapewi mafunzo ya kijeshi kwa undani. Mpaka mara ya mwisho nilipofuatilia, walikuwa wanapewa mafunzo ya kijeshi kwa karibu 35% huku zilizobakia ni ujasiriamali na uzalendo!

**Vyeo vinafanana. Ukiacha wale servicemen wale viongozi wao ni wanajeshi halisi na vita ikiwaka wanasongesha kama wanajeshi wengine.

**Kama umenielewa vizuri mpaka hapo, ni wazi kuwa JKT haihitaji silaha za maana, zaidi ya bunduki za kulinda, mali zao ambazo ni karakana, mifugo, ofisi, bustani na maghala yao ya bunduki.
 
michael western

JF-Expert Member
May 7, 2014
545
0
**JWTZ ndiyo walioanzisha mafunzo ya JKT na ndiyo wanaofundisha mpaka leo.

**Viongozi wote wa JKT lazima wapitie mafunzo ya depo za kawaida za JWTZ

**JKT hawapewi (servicemen) hawapewi mafunzo ya kijeshi kwa undani. Mpaka mara ya mwisho nilipofuatilia, walikuwa wanapewa mafunzo ya kijeshi kwa karibu 35% huku zilizobakia ni ujasiriamali na uzalendo!

**Vyeo vinafanana. Ukiacha wale servicemen wale viongozi wao ni wanajeshi halisi na vita ikiwaka wanasongesha kama wanajeshi wengine.

**Kama umenielewa vizuri mpaka hapo, ni wazi kuwa JKT haihitaji silaha za maana, zaidi ya bunduki za kulinda, mali zao ambazo ni karakana, mifugo, ofisi, bustani na maghala yao ya bunduki.

Nashukuru mkuu sikuwa nafahamu hilo,kwahiyo ina maana vita inapotokea hawa JKT wao watakuwa hawatoki nje ya mipaka au wanaweza pia kuchuliwa kwenda kupigana huko nje!
 
PAPA OBAMA

JF-Expert Member
Dec 27, 2013
204
225
Kwa kuongezea, kimsingi
WANAJESHI walioajiriwa JKT wote ni JWTZ, ile ni kama Kamandi kuu ihusuyo
na malezi ya vijana na Uzalishaji mali. Kamand zingine ni Landforce,
Airforce na Navy nk nk. So JKT na JWTZ ni kitu kile kile,ila JWTZ ndiyo
mkuu wa yote!
kweli mkuu JKT ni tawi tu la JWTZ huwezi zilinganisha tawi na shina
 
Elly B

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
1,194
1,195
Nashukuru mkuu sikuwa nafahamu hilo,kwahiyo ina maana vita inapotokea hawa JKT wao watakuwa hawatoki nje ya mipaka au wanaweza pia kuchuliwa kwenda kupigana huko nje!

Wale viongozi wao, wanaweza lakini servicemen hapana. Ila kama itafikia mahali kuwe na upungufu wa askari, kulingana na mahitaji, basi hapo huwa kila mwananchi huwa anatakiwa kujitolea kupigania nchi yake, hata Servicemen!

cc michael western
 
Last edited by a moderator:

Master plan

JF-Expert Member
Dec 24, 2012
3,665
2,000
Kuna wakati huwa inafikia, hata raia wa kawaida anakwenda. Hardly utapelekwa kambini, utafundishwa kutumia bunduki, risasi zikielekea mbele inatosha. But that is not normal. Katika hali ya kawaida hatutegemei mgambo aende vitani.

Umesomeka vya kutosha.
 
MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
15,929
2,000
JKT ni kamandi moja wapo ya JWTZ. JKT ni kamandi ya askari wa ziada(Reserves)

Safi mkuu short and clear.......JKT ni sehemu ya JWTZ.....

SHERIA YA KUANZISHWA KWA JESHI LA KUJENGA TAIFA NA MAREKEBISHO YAKE

Jeshi la Kujenga Taifa lilianzishwa kwa sheria ya ‘Nationa Service Act No 16' ya mwaka 1964. Sheria hii inatoa uwezo wa Jeshi la Kujenga Taifa kuandikisha vijana wa kulitumikia taifa. Aidha, sheria hii imeendelea kufanyiwa marekebisho kutokana na mahitajio, baadhi ya marekebisho hayo ni:-

a. Marekebisho ya mwaka 1966

Tangu lilipoasisiwa JKT lilikuwa linaandikisha vijana wa kujitolea wenye elimu ya chini tu. Ilipofika mwaka 1966, ilionekana kuwa, kuna umuhimu wa vijana wasomi wenye elimu zaidi ya kidato cha nne kulitumikia JKT. Hivyo, sheria ilirekebishwa ili kulipa JKT nguvu za kisheria ili liweze kuandikisha vijana wenye taaluma zaidi ya kidato cha nne kwa mujibu wa sheria (Compulsory service).

b. Marekebisho mengine ni ya mwaka 1975 wakati JKT lilipounganishwa rasmi na JWTZ, hivyo kulifanya JKT kuwa moja ya Kamandi zilizo chini ya JWTZ. Sambamba na marekebisho hayo, shughuli za JKT ziliwekwa bayana kuwa ni:-

(1) Kuwafundisha vijana wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kulitumikia Taifa katika nyanja za
kijamii, maendeleo ya uchumi na ulinzi wa Taifa.

(2) Kutoa mafunzo ya msingi ya Jeshi kwa vijana kwa lengo la kuwawezesha vijana hao kufikia sifa

ya kujiunga katika vyombo vya Ulinzi na Usalama kama JWTZ, Polisi, Usalama wa Taifa na Magereza.
(3) Kushiriki kikamilifu katika ulinzi wa Taifa.
 
Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
8,308
2,000
Haya majeshi makubwa nchini Tanzania ni jeshi lipi linamzidi mwenzake kiujuzi,mazoezi,kuwa na wasomi wengi,mishahara,na mengineyo!

Je vyeo vyao vinafanana?

Je kwa maswala ya mafunzo wanaingiliana kama wataalam wa JWTZ kufundisha kwenye JKT na wa JKT kufundisha JWTZ?

Ni jeshi gani hapo lina silaha za maana zaidi kuliko mwenzake na kupewa kipaumbele?

Wenye ufahamu kuhusu hili naomba tujadili!

JKT ni kama kitengo tu kilichopo chini ya JWTZ na waajiriwa wote wa JKT wapo chini ya JWTZ n lazima waende mafunzo yao!!
 
beefinjector

JF-Expert Member
Jul 23, 2009
1,147
2,000
JKT ni kamandi moja wapo ya JWTZ. JKT ni kamandi ya askari wa ziada(Reserves)

Hata mimi ndio naelewa hivyo, na ndio maana tulioenda JKT miaka ile ya kwa mujibu wa sheria tulikuwa tunapewa mpaka Force number. Sijui hawa vijana walioanza kwenda juzi kama nao wanapewa.
 
HP1

JF-Expert Member
Feb 4, 2012
3,366
2,000
JWTZ bora zaidi kulinda mipaka ya nchi
JKT ni sehemu ya JWTZ ni bora zaidi kwenye uzalishaji mali na kujitegemea
Polisi ni bora zaidi kwenye kulinda raia na mali zao
 
Kennedy

JF-Expert Member
Dec 28, 2011
24,076
2,000
Kwenye thread ni kuwa hakuna majeshi mawili hapa ila kuna jeshi moja tu sasa huwezi kusema ipi bora na ipi sio bora
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom