Kati ya Jasusi na Commando, yupi ni mtu hatari sana anayepaswa kuogopwa?

Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa Jamiiforums. Mimi mdogo wenu Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to the Almighty. Leo swali langu ni kama hivi;

Kati ya Jasusi na Commando, yupi ni mtu hatari sana anayepaswa kuogopwa?

Nimeuliza hivyo kwa maana kwamba inasemekana hawa wote wawili wanakuwa ni watu waliopitia mafunzo magumu sana ya uvumilivu (endurance), matumizi ya silaha pamoja na kujilinda (self-defense).

Kuna baadhi ya watu wanadai Jasusi anatumia akili nyingi na nguvu kidogo wakati Commando anatumia nguvu nyingi na akili kidogo.

Ni nani mtu hatari sana kumzidi mwenzake?

OMBI LANGU: NSSF nipeni pesa zangu nyie jamaa. Mtaani maisha ni magumu sana. Mungu anawaona mjue?????
Hao jamaa(Komando Vs Jasusi) wanafanya kazi tofauti,ukizungumzia Bato komando yuko juu hata operation wanazopewa hua ni tofauti ukizingatia Komando anaweza kua jasusi ila jasusi hawezi kua komando
 
Unajua ulichokiandika mkuu?

Commando usimfananishe na chochote kile, Komando ndie anayefundishwa ujasusi, Jasusi hafundishwi ukomando.

Mpaka uwe jasusi ni jitihada zako tu kusoma, siku hizi na connection, Commando hata connection hakuna na ni kozi ambayo mtu haombi kizembe, ni unachaguliwa kwenda kutengenezwa.

Na ina umri wake maalumu kujifunza ukomando tofauti na ujasusi. Mkuu ukisikia mtu ni komando, ana bawa full, achana na hicho kiumbe.
Angalau nimeyaelewa maandishi uliyoyaandika.
 
Mkuu umepiga mojaa kaliii. Kula utawala kwanza kidogo
Wengi wanajibu tu ilimradi amejibu au anatumia uelewa wake tu kujibu, kwa ufupi Sana naomba nieleze kidogo,
Komando Ni mwanajeshi wa cheo chochote alifuzu mafunzo maalumu, komando Ni jeshi kamili( single army unity) pia Ni ukamilifu( full package) yeye lazima afuzu mafunzo ya military intelligence, martial& combat karate, air, infantry and navil( SEAL), anauwezo wa kupeleleza, kushambulia, kupigna, kuteka, kuokoa mateka n.k komando kutokana na uwezo huo huweza kutumika na taasisi mbalimbali za kijasusi

Jasusi Ni mtu anayejifunza kutafuta, kufatilia, kutathmini, kuandaa taarifa fulani au tukio fulani!! Ktk kazi ya ujasusi vyote hutumika nguvu na akili pia japo ndani ya ujasusi Kuna vitengo vingi Sana, vipo mahususi kwa kukusanya data, kufatilia data, kuua, kupoteza ushahidi n.k hivyo jasusi lazima apate basic ya physical training( martial arts and combat karate)
Ujasusi upo sehemu zote jeshini na uraiani,. Lakini komando Ni special force ndani ya jeshi !!
Upo wakati TISS huhitaji msaada was komando na pia huhitaji military intelligence lkn jeshi huwa halihitaji msaada wa TISS !!!! Kwa ufupi Sana naomba niishie hapa zaidi tunaweza vuka mipaka
 
Tunamuita ASSET
ha ha ha,kitu kingine jasusi sio lazima awe hatari,anaweza kuwa boya tu lakini ni jasusi,msitishwe na hilo jina jasusi,anaweza kuwa hata dame fulani mfano anatumwa na kundi fulani kwenda sehemu fulani akapata kazi,mfano kiwanda fulani akaanza kuiba informations,data etc kuzituma kwa walio mtuma,huyo tayari ni jasusi,
 
Tunamuita ASSET
Both commandos and intelligence officers at times their roles are intertwined,to say a commando primary role is in line in their training they are fighters however mostly in the military,commandos get a priority and some are appointed to carry out clandestine,overt and or covert Intel operations
 
Kwa upande mwingine naona komando anayo nafasi kubwa kuogopwa zaidi ya Jasusi, maana kuna aina nyingi za Majasusi. Kumbuka Jasusi hutokea kutegemeana na kazi husika na mahari husika, hivyo wapo Majasusi wasioweza hata kukwepa ngumi!!😎😎 Lakini wapo vyema katika upande wa utafutaji taarifa na mambo mengine mengi. Sasa basi nadhani mnafahamu vyema nini huwa wanapitia makomando, 😎😎 Wakuu huko kukaza roho tu muda wote.
 
Kwa upande mwingine naona komando anayo nafasi kubwa kuogopwa zaidi ya Jasusi, maana kuna aina nyingi za Majasusi. Kumbuka Jasusi hutokea kutegemeana na kazi husika na mahari husika, hivyo wapo Majasusi wasioweza hata kukwepa ngumi!!😎😎 Lakini wapo vyema katika upande wa utafutaji taarifa na mambo mengine mengi. Sasa basi nadhani mnafahamu vyema nini huwa wanapitia makomando, 😎😎 Wakuu huko kukaza roho tu muda wote.
 
Kutokana na ujuzi wa teknolojia na uvumbuzi wa silaa zenye uwezo mkubwa zimekuja kupoteza uhalisia wa hivi vitu,jasusi/komando.Kwa nyakati hizi hawa wanapimwa kwa uwezo wao wa kutumia teknolojia na silaa na namna wanavyoweza kukwepa risasi wanapolengwa....
 
Komando ana mafunzo ya kikomando na kidogo ya kijasusi na jinsi ya kumtambua jasusi,ila jasusi ana mafunzo yakijasusi,,
Swali langu ni jason bourne kwenye zile movies zake za kijasusi yeye kacheza kama komando au kama jasusi??
 
Usitishwe na jina jasusi (linatisha yani km huyu mtu hatari) kingereza spy huyu uwezi kumfananisha na komando. Komando ni mtu hatari ambaye anaweza kufanya tukio hatari sehemu ya tukio tofauti na spy ambaye yy anafanya upelelezi tu. Km kuna jasusi na komando sehemu ya moja na kuna kitu kinatakiwa kifanyike mara moja atapewa komando jukumu zima la utelekezaji wa order
 
Back
Top Bottom