Kati ya Jasusi na Commando, yupi ni mtu hatari sana anayepaswa kuogopwa?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa Jamiiforums. Mimi mdogo wenu Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to the Almighty. Leo swali langu ni kama hivi;

Kati ya Jasusi na Commando, yupi ni mtu hatari sana anayepaswa kuogopwa?

Nimeuliza hivyo kwa maana kwamba inasemekana hawa wote wawili wanakuwa ni watu waliopitia mafunzo magumu sana ya uvumilivu (endurance), matumizi ya silaha pamoja na kujilinda (self-defense).

Kuna baadhi ya watu wanadai Jasusi anatumia akili nyingi na nguvu kidogo wakati Commando anatumia nguvu nyingi na akili kidogo.

Ni nani mtu hatari sana kumzidi mwenzake?

OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Jasusi unaweza kua hata ww kama nchi husika au idara ya ujasusi itakuona unaweza kupenya vizuri na kufanya kazi (kukusanya taarifa etc) flan ambayo mtu mwingine itamuia vigum. Kwamfano, ni rahisi Kardinali Pengo kutumwa kama Jasusi Vatican kuliko umtume mtu wa Kawaida

Lakini Komando ni mtu hatari, mwenye mafunzo na anatumika kwenye mission zinazohitaji kuapply skills na force

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Majasusi wapo wa aina mbili....tuanza na aina ya kwanza...Jasusi huyu wa aina hii ni yule kazi za ujajasusi anazifanyia katika war zone au kwa maslai ya kijeshi huyu anaweza kuwa katika ngazi ya ukomandoo kwa maana amepitia mafunzo hayo ya ukomandoo.
Jasusi wa pili niyule anayefanya ujasusi kwa sabau za kitaifa kwa maslahi au kwa sabubu ya uchumi,au kwasababu ya ulinzi wa nchi yake au pia kwa ajili yakupata taarifa fulani zinazo hitajika katika nchi husika.

Sasa Komandoo yeye ni mtu wa vita katika medani za vita vigumu makomando ndiyo kazi yao kuhakikisha kwanza wanajua ramani ya vita ya mwenzake katika uwanja wa mapambano lakini si jasusi.....kidogo ni kdadafulia nikijuacho mengine tutaendelea kujuzana kadri ya mahitaji.
 
Jasusi unaweza kua hata ww kama nchi husika au idara ya ujasusi itakuona unaweza kupenya vizuri na kufanya kazi (kukusanya taarifa etc) flan ambayo mtu mwingine itamuia vigum. Kwamfano, ni rahisi Kardinali Pengo kutumwa kama Jasusi Vatican kuliko umtume mtu wa Kawaida

Lakini Komando ni mtu hatari, mwenye mafunzo na anatumika kwenye mission zinazohitaji kuapply skills na force

Sent using Jamii Forums mobile app
Umeongea kweli kabisa

Sent from my itel A32F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom