Kati ya hivi ni kipi kinafanya uchumi wa nchi na uchumi wa mtu mmoja kukua

EllySkyWilly

JF-Expert Member
Aug 28, 2020
2,204
2,083
Kati ya hivi ni kipi kinafanya uchumi wa nchi na uchumi wa mtu mmoja kukua

1. Je kutoza kodi kubwa kunafanya uchumi kukukua?

2. Je kutoza kodi kidogo kunafanya uchumi Kukukua?

3. Je kufanya kazi za udhalishaji mali kwa bidii kwa, masaa mengi kunafanya uchumi kukua?

Lete jibu hapa na utupe maelezo ni kwanini?
 
Namba mbili ikiboreshwa itasaidia sana hayo makusanyo ya kodi kukua. Kodi iwe ndogo halafu serikali ibuni vyanzo vingi zaidi huku ikichochea ukuaji wa uchumi kwa mtu mmoja mmoja kwa kuboresha miundombinu ya barabara, kilimo, biashara, viwanda na upatikanaji wa masoko ya bidhaa ndani na nje ya nchi, kuzalisha ajira za kutosha kwenye Sekta binafsi na Serikalini, nk.
 
100/100 Excellent
 
Namba mbili,kutoza kodi stahiki kwa eneo husika.
Yaani kiwepo kitengo maalum cha wahasibu ambacho kitahusika na kuhakiki biashara za watu na kutoza kodi kuendana na mfumo uliowekwa,ambao hautaathiri wafanyabiashara wala government.
Pia kuwe na majukwaa elekezi kwa wafanyabiashara na watendaji,ikitokea kuna mapungufu mahali wanakaa chini kujadili na kupata ufumbuzi.
Kodi ni muhimu kwa maendeleo ya taifa lolote,ila inakuwa na tija na manufaa kama itaendana na uhalisia wa biashara za walipaji.
 
Back
Top Bottom