Kati ya hawa wawili ni nani husababisha mmojawapo kufa mapema?

Yuyo Ahumile Shamalendi

JF-Expert Member
Mar 10, 2018
993
782
Habari kwa ujumla, niruke moja kwa moja kwenye mada.

Naombeni kuuliza katika maisha ya ndoa ni nani kati ya mume na mke ambae kwa ujumla husababisha mwenza wake atangulie mapema mbele ya haki?
Karibu wachangiaji ili tujue kua ni akina nani wasababishi na tukishajua tuwashauri wahanga waweze kuepukana na hili janga au nini kifanyike kuepusha haya?

Nawasilisha, karibuni.
 
Wacha niseme, katika kuhangaikia familia nyumbani baba hutoka kwenda kutafuta ili mke amlidhishe (amflahishe),huenda machimboni, mapolini, mijini, na nk huko kote hukumbana na mikasa hatimaye mauti.
Mwanamke baba nanilii njoo utusaidie kuna nyoka, baba anakuja anaokota fimbo kuanza kupambana nanyoka masikini anakosea kidogo nyoka anamgonga (Black mamba) anakufa.
Mume anamfuma mke wake akiwa na lijamaa, wanaanza kupambana bahati mbaya anazidiwa anapigwa pabaya anakufa.
Wanaume huongoza kufa zaidi ya wanawake.
Hapa sijui husababisha nani!
 
Wacha niseme, katika kuhangaikia familia nyumbani baba hutoka kwenda kutafuta ili mke amlidhishe (amflahishe),huenda machimboni, mapolini, mijini, na nk huko kote hukumbana na mikasa hatimaye mauti.
Mwanamke baba nanilii njoo utusaidie kuna nyoka, baba anakuja anaokota fimbo kuanza kupambana nanyoka masikini anakosea kidogo nyoka anamgonga (Black mamba) anakufa.
Mume anamfuma mke wake akiwa na lijamaa, wanaanza kupambana bahati mbaya anazidiwa anapigwa pabaya anakufa.
Wanaume huongoza kufa zaidi ya wanawake.
Hapa sijui husababisha nani!
Ndiyo pamoja na hayo kwani mengine ni majukumu yaliyopangwa na muumba kua huyu atafanya hili na yule atafanya lile, hapa kinachotafutwa ni wahusika wa kusababisha wenza wao kutangulia, mfano ugomvi, magonjwa, stres na mengineyo mengi tupe uzoefu wako.
 
Sitaki kutoa hukumu, ila ngoja nisimulie kisa kimoja,
Marehemu baba yangu mdogo alifariki mwaka 1997 kwa kupararaizi, ilikua hivi, kiujumla mama yangu mdogo ni muongeaji sana mno, kiasi kwamba akianza kuongea hua haishiwi chaji zaidi zaidi wasikilizaji ndo mtaishiwa chaji na kukimbia, nadhani mnajua nikiongea hivo namaanisha nini kiufupi ni wale akina mama ambao akianza kuongea utatamani ardhi ipasuke ujichimbie, sasa kulingana na mfumo huo ilibidi baba mdogo atafute njia mbadala ili aweze kupata faraja, sasa kutokana na kuhangaika huku na kule akijikuta amejibanza kwa mama mmoja ambae alikua ni single mother.

Kama kawaida wakawa wanaendelea na maisha baba mdogo anaishi nyumbani kwake kule kwenye nyumba ndogo akawa anaenda zake na kurudi wakati huo mama mdogo hajajua kua mweza wake anachepuka, wameendelea hivo kwa muda mrefu ikafika siku baba mdogo alikua ametoka huko kwenye nyumba yake ndogo akafika nyumbani kwake akaenda chooni akatoka akawa anaingia ndani ile kunyanyua mguu wa kwanza ili aingie ndani akaanguka hapo hapo mlangoni wakati huo mguu mmoja uko ndani tayari na mwingine uko nje, pale pale akawa anaomba msaada wakati huo mdomo umeenda upande mkono na mguu wa kulia haufanyi kazi, ikabidi akimbizwe hospitali, amekaa hospitali miezi mitatu akafariki dunia r i p baba mdogo.

Baada ya kumalizika msiba ikaja kugundulika kua alirogwa na mzee mwingjne ambae walikua wakigombea kwenye hilo jimbo, iligundulika hivo baada ya huyo mzee kuongea hadharani kua amemkomesha yeye hua hachezewi hayo tuyaache.
Twende kwenye hoja ni kwamba mzee alikua akitafuta faraja baada ya nyumbani kumkondesha kila uchao lakini akaja kuangukia pabaya na kupoteza maisha.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom