Kati ya hawa watu wawili (D na H) ni nani kwako wewe hasa ni Eistein (Mwerevu) kiuchumi kuliko mwenzake?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,544
108,869
Mtu D

Huyu ni Mtu Tajiri sana hivyo kwa Kutumia Pesa zake na ili asijichoshe na asipoteze muda aliamua Kuingia Jukwaani na Ndege ya Helicopter. Na hata alivyoingia Ukumbini bado aliweza Kuonyesha kuwa Yeye si tu kwamba ni Tajiri lakini pia ni Mtu Mwerevu (Einstein) mno na ambaye Mambo yake mengi tu yamepangiliwa na kupangika vizuri Kiratiba. Na kuonyesha kuwa anajithamini hata hakukaa muda mrefu baada ya 'Kutumbuiza' na Helicopter 'Kumbeba' na Kuondoka wakati Mwenzake aliondoka na Bajaji baadae.

Mtu H

Hili nalo ni Litajiri mno ila kwa Ubahili wake wa Pesa huku likijua kabisa litajichosha na hata kuhatarisha Maisha yake likaamua Kuingia Ukumbuni kwa 'Kuwaiga' Askari 'Komandoo' na matokeo yake likatua vibaya na kupatwa na 'Kizunguzungu' kama cha dakika Mbili hivi ndiyo likaanza Kujitambua na 'Kutumbuiza' huku likimshukuru Mwenyezi Mungu kwamba kaepuka 'Kifo' alichokuwa akikiona kabisa kinakuja hadi kuanza 'Kulia' na Kutia 'Huruma' akiwa 'Angani' na Kudondosha 'Bendera' yake na 'akijamba' vile vile.

Nayasubiri majibu yangu kutoka Kwenu tafadhali!
 
Sasa mkuu unataka watu wajadili nini wakati ushaonesha chuki nzito sana kwa mtu wa pili ?

Huyo Mtu wa Pili hapo ni nani Mkuu? Mbona hata Wewe pia nimeambiwa kuwa 'Unamkubali' sana huyo Mtu wa Kwanza hapo kwani ni Fundi hasa?
 
Back
Top Bottom