Kati ya Haji na Barbara nani hapa kazichanga vyema karata zake na yupi kajimaliza na atajutia milele?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,548
108,858
Je, ni Haji Manara ambaye baada ya Kuuamisha Umma kuwa anaonewa hivyo alitamani Simba SC ifungwe majuzi ili aje Kummaliza vyema Adui yake Kisha akaendelee zake Kupiga Pesa ASAS Diary, Azam Products na GSM au ni CEO Barbara Gonzalez ambaye pamoja na Shutuma zote alizopewa ila alichagua Kunyamaza mpaka Simba SC iibuke Mshindi katika Fainali ya ASFC kisho ndipo aje Kummaliza vizuri Adui yake na awe sehemu salama Kuiendesha Simba SC Kiuweledi zaidi akiwa na Wasaidizi wanaojitambua kuanzia kiakili na kimaadili?

Nasubiri Majibu yenu japo nimeshangazwa kutaarifiwa hivi punde kuwa Yule Yule aliyeomba Mwenyewe kuachana na Simba SC tena kwa Jeuri na Nyodo zote ndiyo huyo huyo baada ya Kuona Klabu ya Simba imetoa Tangazo la Mbadala wake ghafla akaangua Kilio Kikubwa Kwake Mikocheni jirani na Ofisi za Kampuni ya Simu ya Halotel.

Simba SC ni Kubwa kuliko yoyote Yule!
 
Simba sports club , ni taasisi, na ina utaratibu wake wa kujiendesha, binafsi kitendo walichokifanya ni cha weledi kabisa.

Haji amekua mlopokaji sana na kufanya mambo ambayo mara nyingine hayana ulazima katika klabu, na klabu imekua ikikaa kimya.

Binafsi napongeza uongozi wa simba kwa walichokifanya, watu wote watapita ila itasimama, na hili litakua kama angalizo kwa watumishi wenye mambo na tabia kama za Haji.

Respect......
 
Tatizo manara hajui maadili ya kazi na kila taasisi ina maadili yanayopaswa kufatwa. Huwezi kumshambulia mkubwa wako vile mtandaoni.. alistahili kuondolewa tena simba imemvumilia saana. Ethics &code of conduct ziheshimiwe
 
Siwezi nikapata kibarua kikubwa vile halafu nikakichezea kama alivyofanya haji
Nasikia anaenda kuwa mkurugenzi wa halmashauri moja hapa nchini...nasikia kule ata kama mshahara mdogo ila kuna posho nyingi na kule kuna uwakika wa maisha.
 
Nasikia anaenda kuwa mkurugenzi wa halmashauri moja hapa nchini...nasikia kule ata kama mshahara mdogo ila kuna posho nyingi na kule kuna uwakika wa maisha.
Acheni Uzushi na Kudanganya Watu na ni vyema kama hamjui Mambo muwe mnanyamaza tu.

Kwa Rekodi Chafu aliyoiweka Haji Manara alipokuwa Mwenezi CCM Mkoa na 'dossiers' zake ndani ya CCM kuonyesha kuwa hafai nitamdharau Mtu yoyote atakayemteua huko Serikalini.

Hata Kimaadili tu Haji Manara ameshapoteza Sifa ya kuwa Kiongozi wa Serikali. Kama ameshaonyesha kuwa ni Msaliti ndani ya Klabu Kubwa kama ya Simba na hana Kifua cha Kutunza Siri je, huko Serikalini ndiyo ataweza?

Watanzania mnaposikia au kuambiwa Habari za Umbea na Uzushi kama ulivyoambiwa Wewe na Kuziamini mkimaliza nanyi muwe mnajikita katika kutafuta 'Facts' za Mhusika ili mjue kama ataweza au hawezi.

Serikali ya Tanzania ikimteua Haji Manara kwa Cheo chochote kile ( hasa DED au DAS au DC ) nitaidharau na hata Mteuwaji nae nitamdharau mno.

Haji Manara ni Mswahili aliyeshindikana.
 
Kwenye serikali ya CCM amna kitu kina choshindikana boss mfano mzuri n aliyekuwa mkuu wa mkoa wa arusha ndugu mrisho gambo na mchungaji gwajima...
 
Nasikia anaenda kuwa mkurugenzi wa halmashauri moja hapa nchini...nasikia kule ata kama mshahara mdogo ila kuna posho nyingi na kule kuna uwakika wa maisha.
Akiwa mkurugenzi wa familia yako inatosha,wapumbavu dizaini ya Haji na wewe hamna hadhi ya kuongoza taasisi zenye weledi labda hizo uchwara zenu
 
Kwenye serikali ya CCM amna kitu kina choshindikana boss mfano mzuri n aliyekuwa mkuu wa mkoa wa arusha ndugu mrisho gambo na mchungaji gwajima...
Hivi Mapungufu ya Kimaadili ya Mrisho Gambo au Mapungufu ya Askofu Gwajima ukiwa na Akili timamu kabisa unaweza Kuyafananisha na ya ( aliyonayo ) Haji Manara?

Nina Mashaka na Uelewa wako hasa Kiuchambuzi na kwa Ufuatiliaji pia wa Masuala Mtambuka yanayoendelea nchini Tanzania na hata duniani.
 
Back
Top Bottom