Kati ya elimu na tiba kipi kingekua bure?

abdallahjumbe

Member
Jul 1, 2016
48
46
Pongezi kwa mtukufu rais Magufuli kuja na hii kitu sijui tuseme ni sera ya chama ama ni matakwa yako juu ya elimu kua bure

Katika mwaka wa kwanza tu tumeshuhudia wimbi kubwa la uandikishwaji wanafunzi darasa la kwanza

Hii maana yake ni kua walala hoi wengi tulikua tukikosa elimu hata ya msingi tu

Lakini nyuma ya elimu kuna jambo muhimu la tiba

Mtukufu rais kama ungekusanya maoni kati ya elimu na tiba kipi kiwe bure walala hoi wote tungechagua tiba

Ila kwa kuwa wewe umetuchagulia elimu kwanza sio mbaya tumelipokea

Ila tunakuomba basi katika awamu yako ya pili na tiba iwe bure

Mwaweja baba
 
Back
Top Bottom