Kati ya Dr. Mary Mwanjelwa na Dr. Tulia Ackson ni nani ana ubavu wa kumng'oa Sugu Mbeya mjini?

Ok,ndo maana huyu Tulia anahangaika sana japo anatafuta jimbo,anatamani mbeya lakini sugu kakaza na kule kwao lwangwa ndo hawamtaki kabisaa
Dr Tulia sio wa Lwangwa ni mtu wa Bulyaga(Tukuyu) Lwangwa alienda kuzindua ujenzi wa kituo kipya cha polis
 
Hakuna hata mmoja ,wote wamezoea kubebwa bebwa na kusukumizwa, maana kama tulia akijikuta tu kasukumiamo naye akaingiamo
 
Kwanza iko hv jimbo la mbeya kwa uwanja huru ccm hawawezi kupata kura hata nusu.
Tumeona mabadiliko chini ya sugu.

Hao waende tukuyu huko nako wasitegemee mteremko.
Kuwa mshindi jimbo la mbeya si lelemama hapa pana msafwa amebadilika si mchezo.
Just imagine shitambala ni msafwa mwenzao lakini walimnyima kura pamoja na kutumia ukabila kwenye kampeni.

Kwa sasa sugu anavyoteswa jela ndo wanambeya mzuka unazidi kupanda.
Ccm mbeya imejenga chuki kwa wananchi yenyewe kwa kuleta usumbufu usio wa lazima.
Nionavyo Sugu hagombei tena labda wakigawa majimbo bado naona wagombea ni wengine.

Tulia ataongea nini hasa hapa mbeya kumshawishi nani.Labda wawafunge mawakala vituoni kama walivyofanya arusha.
Mkuu wasafwa hawana ukabila kabisa..wanachotaka ni mtu muelewa,,imagine walimtema mpesya na shitambala pamoja ni wasafwa wenzao..
 
Ujinga mkubwa ambao Chama changu cha Mapinduzikitafanya ni kumteua mnyakyusa kugombea jimbo la Mbeya mjini..

Ikumbukwe wenyeji halisi wa mkoa wa Mbeya ni Wasafwa, lakini kutokana na kelele za wanyakyusa Wasafwa wanadharaulika, na ukisema tu 'natokea mbeya' unaonekana ni mnyakyusa..

Hili jambo linawauma sana Wasafwa ambao wanaona wanapolwa mkoa wao..

Jiulize mara ya mwisho Mbeya kuwa na mbunge mnyakyusa ni lini.?

CCM wasijiroge kupeleka mnyakyusa pale,.

Idadi ya wasafwa Mbeya mjini ni mara mbili ya wanyakyusa hapo hujahesabia WANYIA,WAMALILA na WANDALI ambao ni jamii ya Wasafwa na wanaongea lugha moja.
 
Hawa madaktari wawili ndio wanaotajwa sana jijini Mbeya kwamba mnamo mwaka 2020 watajitosa kupambania ubunge dhidi ya mbunge wa sasa Joseph Mbilinyi aka Sugu.

Je, yupi ana ubavu wa kumpiga chini " mnyamwezi" Sugu kati ya hizi PhD mbili?

Nawasilisha!
Wote wawili, kila mmoja ni maradufu ya sugu na hence lake
 
Hawa madaktari wawili ndio wanaotajwa sana jijini Mbeya kwamba mnamo mwaka 2020 watajitosa kupambania ubunge dhidi ya mbunge wa sasa Joseph Mbilinyi aka Sugu.

Je, yupi ana ubavu wa kumpiga chini " mnyamwezi" Sugu kati ya hizi PhD mbili?

Nawasilisha!
Hao wote hawana ubavu wakumtoa sugu .kwanza si wazaliwa wa mbeya wanatokea huko maporini .Sugu ni mzawa wa mbeya msafwa original
 
PhD siyo zinazoshinda uchaguzi au kuwa na PhD siyo kwamba ndiyo tiketi ya ushindi. The character is important and SUGU he is a man of character. Hao wote watapigwa chini.
 
Hao wote hawana ubavu wakumtoa sugu .kwanza si wazaliwa wa mbeya wanatokea huko maporini .Sugu ni mzawa wa mbeya msafwa original

Tuweke kumbukumbu Sawa mkuu sugu kaja mbeya akitokea Mtwara akiwa yuko shule ya msingi hivyo ali hamia shule ya msingi Sisimba na huko Mtwara ndiko aliko zaliwa toka lini Mbilinyi akawa msafwa ?
 
Back
Top Bottom