Kati ya CCM na CHADEMA nani tayari anamwaga damu za watanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kati ya CCM na CHADEMA nani tayari anamwaga damu za watanzania?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Jatropha, Oct 5, 2010.

 1. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  katika siku za hivi karibuni ccm imeanzisha siasa za maji taka kwa kuwatisha watanzania kuhusu umwagaji damu, ikiwa ni pamoja na kulitumia jeshi.
  lengo la ccm ni kuwafanya watanzania wavihofie vyama vya upinzani kama walivyofanya mwaka 1995 wakati kituo pekee cha runinga cha itv kiliporusha picha za mauaji ya rwanda katika kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu kama hiki, na hivyo kuwafanya mafisadi kupata ushindi wa kishindo katika chagzui zilizofuatia
  hebu tujiulize kati ya vyama vya ccm na chadema au cuf ni chama kipi kinahusika moja kwa moja na umwagaji wa damu na watanzania kupoteza maisha? Ni viongozi wa chama kipi ambao mpaka sasa wameshahusika na umwagaji wa damu za watanzania na watanzania kupoteza maisha kwa sababu mbali mbali?
  haki ya kuishi ni moja ya haki za msingi katika katiba ya jamhuri ya muungano, hivyo ni jukumu la serikali iliyoko madarakani kutumia raslimali za nchi hii kuwapatia wananchi uhifadhi ya maisha yao.
  kwa mujibu wa katiba hiyo serikali za tanzania ni lazima zitokane na vyama vya siasa. Hivyo chama cha siasa hakiwezi kukwepa lawama za mapungufu yoyote yanayotokana na utendaji duni wa serkikali yake. Kwa takribani miaka 49 sasa chama cha ccm kimekuwa madarakani kwa mujibu wa katiba hiyo.
  kutokana na viongozi wa serikali za ccm zilizokuwa madarakani kushindwa kushindwa kutimiza wajibu wao ipasavyo katika mutumizi ya raslimali za taifa, hali hiyo ya upungufu au kukosekana kwa raslimali katika sekata m,bali mbali kumepelekea baadhi ya watanzania kufikwa na umahuti kwa sababu mbali mbali ikwemo maradhi yanayoepukika, ajali za barabarani zinazoepukika, kulia na kutumia vyakula na bidhaa vibovu na vsizokidhi viwango vinavyoingizwa hapa nchini na kusababisha watanzania kupata kansa na hatimaye vifo n.k.
  tujiulize ni watanzania wangapi wanapoteza maisha kila mwaka kwa kukosa madawa, kukosekana kwa madakatari, manesi, wauguzi, vifaa vya tiba n.k katika kile kwa muda mrefu serikali za ccm zinachokiita ukosefu wa fedha za kutosha kuwapatia wananchi huduma hizo?
  ni akina mama na watoto wachanga na wale wa kufikia umri wa miaka mitano wangapi wanapoteza maisha kila mwaka kutokana na kukosekana kwa huduma za kujifungua salama. Madawa, vifaa vya kujifungulia, madakatari, manesi, wauguzi n.k. Katika kile kwa muda mrefu serikali za ccm zinachokiita ukosefu wa fedha za kutosha kuwapatia wananchi huduma hizo?
  ni wagonjwa wagapi wanapoteza maisha kwa kukosa huduma ya kufikishwa hospitali kwa kukosekana usafiri? Katika kile kwa muda mrefu serikali za ccm zinachokiita ukosefu wa fedha za kutosha kuwapatia wananchi huduma hizo?
  ni watanzania wanagapi wanakufa kila mwaka kutokana na magonjwa yanyosababishwa na matumizi ya maji machafu kama vile kipindipindu, kuhara n.k? Katika kile kwa muda mrefu serikali za ccm zinachokiita ukosefu wa fedha za kutosha kuwapatia wananchi huduma hizo?
  ni wazee wangapi wanakufa kutokana na kukosa matunzo, na vilema kukosa misaada?katika kile kwa muda mrefu serikali za ccm zinachokiita ukosefu wa fedha za kutosha kuwapatia wananchi huduma hizo?
  ilihali tanzania imejaaliwa utajiri lukuki ikiwemo madini kama vile dhahabu, almasi, tanzanite, gesi, uranium, ruby, saphire n.k; ardhi safi inafaa kwa kilimo; mito, maziwa na vyanzo mbali mbali vya maji vinavyofaa kuwapatia wananchi maji safi ya kunywa, kilimo cha umwagaliaji, kuzalisha umeme ili kuondoa umaskini n.k; vivutio vya watalii ikwemo mbuga za wanyama, fukwe n.k
  ambavyo vyote vinatumiwa kunufaisha kikundi kidogo cha viongozi wa ccm na serikali zake na washirika wao kutoka nje ya nchi kwa jina la wawekazaji ilihali watanzania wakiachwa wakipoteza maisha kwa visingizio vya ukosefu wa fedha.

  kwa muda mrefu sasa ccm imekuwa ikihusika moja kwa moja na umwagaji damu za maelfu ya watanzania wanapoteza maisha kila mwaka katika ajali za barabarani zinazosababishwa na madereva waliopatiwa leseni za udereva na serikali za ccm kwa njia za rushwa pasipo kupata mafunzo na kufaulu mitihani ya udereva wa magari, pikipiki, bajaj, malori na mabasi ya abiria n.k.

  kwa muda mrefu yamekuwepo madai kuwa serikali za ccm zilihusika moja kwa moja na umwagaji wa damua za watanzania waliofukiwa katika migodi, iliyokuwa mbioni kuuzwa kwa wawekazaji uchwara, na ccm kama chama cha siasa hakijawahi kutoa tamko au kuchukua hatua yoyote juu ya suala hilo.

  ccm na serikali zake zinahusika moja kwa moja na umwagaji wa damu za wakulima na wafugaji waliohusika katika mapigano katika sehemu mbali mbali za nchi yetu kama vile kilosa na kwingineko; kufuatia vitendo vya rushwa vya baadhi ya viongozi wake kuwamilikisha wawekezaji uchwara ardhi ya wafugaji ya loliondo, ngorongoro n.k na wafugaji kulazimika kuhamia na mifugo yao katika sehemu za wakulima.

  hata hivi sasa idadi kubwa ya watanzania wanaendelea kupoteza maisha (umwagaji damu za watanzania) katika kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu wa 2010 kwa sababu zilizotajwa hapo juu kwa madai kwamba serikali ya ccm haina fedha kuwapatia wananchi madawa, huduma za madakatari, manesi na wauguzi pamoja na na vifaa vya tiba ilhali ccm ikitumia bilioni 50 katika kampeni zake kugombea viti 237 tu ilihali chama cha conserrvative cha uingereza kilitumia bilioni 42 tu kugombea viti 639. Na nchi ni mmoja wa wafadhili wetu wakuu na bajeti ya 2010/11 imetupatia bilioni 240.
  iweje ccm iwe na matumizi makubwa ya fedha kuliko vyama vya siasa vinavyoongoza nchi wafadhili wetu? Na fedha hizo ccm inazipata wapi kama sio kutoka katika raslimali zilizopaswa kutumika kuokoa maisha watanzania? Kwa matumizi haya makubwa ya fedha wakati watanzania wanaendelea kupoteza maisha ccm inashirki moja kwa moja katika mauaji ya watanzania na umwagaji wa damu hapa nchini kwa kushindwa kuhakikisha kuwa serikali zake zinztumia raslkimali za taifa kulinda haki ya kuishi ya watanzania.
   
 2. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Sishangai kuna mwaka CCM one night kabala ya uchaguzi walilusha program ya vita ITV kuwatisha watu na upinzani
   
 3. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  CCM kwani ndio wenye vyombo vya dola na dalili za kuvitumia ni matamshi ya Lt. Gen. A. Amir Shimbo! Hivi TPDF wanatulizaje vurugu? Kwa kutumia AK - 47 au artillery?
   
 4. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  umesahau mwaka 2005 siku moja kabla ya uchaguzi generali mahita alionekana kwenye tv akiwa na visu vyenye rangi zinzofanana na benderea ya cuf na kudai eti wamekamata shehna hiyo, baada ya uchaguzi visu hivyo viliendelea kuuzwa mitaani kwa muda mrefu ujao ikiashiria kuwa zilikuwa ni njama za jeshi hilo kuwatisha wananchi wasiichague cuf.
   
Loading...