Kati Kijiji cha mwamalele kilichopo katikati kata ya Loya wilaya ya Uyui, mkoa wa Tabora, kuna tukio limetokea la kutisha

Butiyangu

Senior Member
May 19, 2018
123
167
Kati Kijiji cha mwamalele kilichopo katikati kata ya Loya wilaya ya Uyui, mkoa wa Tabora, kuna tukio limetokea la kutisha na kusisimua.Mnamo tarehe 10 mwezi wa 3 mwaka huu 2019 majira ya saa 12 asubuhi nilikuwa Bado nimelala alikuja kaka yangu kunigongea, maana ni mgeni kwenye Kijiji hiki cha Loya,

Alikuja kunipatia habari za tukio lilotokea kwenye Kijiji jirani kuwa kuna mtoto aitwae Bernard Simoni mwenye umri wa mwaka mmoja, wazazi walikuwa wamemlaza ndani chumbani wao wakiwa nje ilikuwa majira ya saa 10 jioni Jana trh 09 ilipofika saa 12 jioni yaani masaa mawili Toka mtoto alale, mzazi aliingia ndani kumwangalia mtoto wake kama amesema hapo ndipo aliposhituka alipo muona mtoto wake Amelia nyama za mkono wa kilo zote na kubakizwa mfupa tu na mtoto akiwa tayari kafariki, lkn cha ajabu zaidi hapa kuwa na damu hata chembe,

Ndugu wa marehemu waliamua kuripoti tukio hilo kwenye serikali ya Kijiji, baada ya hapo mtendaji na mwenyekiti walienda kushuhudia cha ajabu zaidi walikuja tena zaidi ya kule walichoelezwa, walikuta mtoto kaliwa nyama ya mkono na nyama kidogo ya kichwa sasa hapo watu ndipo waliposhangazwa zaidi. Uongozi wa Kijiji ulitoa taarifa kwenye kituo cha Police Loya, police nao walimpigia kaka yangu ambae ni doctor Kwa ajili ya kwenda nae kwenye eneo la tukio,

Kaka aliniambia nimsindikize, tuliondoka hadi police kisha Kwa haraka tuliondoka, tulipofika eneo la tukio tulikuta tukio limeongezeka zaidi mtoto Bernard alikuwa ameliwa vidole vyote vya miguu, na nusu ya ngozi ya kichwa kimeliwa, lakini hakuna hata chembe ya damu kwenye shuka. Tukio hilo limehusishwa na imani za kishirikina, pia ni mwendelezo wa matukio yanayotoke mara Kwa mara katika Kijiji.

Police wanaendelea na upelelezi na watu wawili tayari wameshakamatwa. R.I.P mtoto Bernard
 
Ninyi watu wa Mbokamanyema hamjaachs tu mambo yenu ya hovyohovyo? Dawa yenu warudishwe wale jeshi la sungusungu "wawasensyemye" hadi muimbe nyimbo za Waswezi.Hambadiliki hadi karne hii.Muwafichue hao watenda maovu.Muanze na kumhoji huyo mama wa mtoto.Kuna kitu hapo.
 
Sijawahi hata kushika karamu ya uandishi wa habari, tatizo la mwandiko limetokana nakwamba wakati naandika ujumbe huu nilikuwa sijatulia nilikuwa kwy gari ya police
Ulikua na haraka sana kwani? si ungetulia uandike kitu kinachoeleweka, yani nimekuja kuelewa mwishoni... Hapo kijijini kwenu kuna shida

Super hero daddy
 
Back
Top Bottom