Enny
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 962
- 130
Kuna topic nilileta hapa kwamba kuna dada, boyfriend wake alichukua kadi yake ya gari na kwenda kuchukulia mkopo wa riba huko mitaani. na alipogundua wanataka kuchukua gari aligombana sana na boyfriend wake huyo. Lakini ili kuepusha gari isichukuliwe ilibidi amwambie huyo bwana anatafute wateja kwa hali na mali ili auze kipande cha shamba nje kidogo ya jiji. kweli bwana alichakarika huku na huku akapata mteja na mteja huyo akatoa nusu ya hela ambayo ilitosha kukomboa gari. Sasa hela iliyobaki akaahidi kulipa mwezi wa kumi na moja. lakini cha kusikitisha yule bwana kaenda kuchukua hela na kaingiza kwenye biashara zake zingine bila kumwambia huyo dada. Dada baada ya kungundua kawaka sana mpaka kampeleka jamaa polisi. Na anaona uwezekano wa kuwa pamoja haupo tena kwani amemkosea mara mbili katika kipindi kifupi ila kwa jinsi ninavyomuaona bado roho yake inamuuma sana kuvunja uhusiano.
Mimi na dada yake tumejaribu kumsihi apige moyo konde amsahau kabisa, aanze ukurasa mpya. Lakini kuna rafiki yake mpenzi anamshauri amsamehe tu huyo bwana anaweza kujirekebisha kwani ameomba msamaha kupitia kwake.
Naomba mawazo yenu hapa katika kumfariji huyu dada.