Katazo la kutokula nyama ya Nguruwe linaathiri Wafugaji Wilayani Kilolo! Kwanini kuna katazo hili?

Hakuna kitu kama hicho .

Nimeuliza najua kuwa wilaya ya kilolo yote kitimoto hakitakiwi.

Swali langu ni why&how.
Ha haaa haaaa hujui unachat na mtu wa wapi ndio maana!

Unasema pomerini nakwambia njoo hapa kilabuni kati kuna nyama we unasema eti hakuna kitu kama hicho!
Haya njoo majuzi mimi nilikua luganga kuna nyama kibao!

Narudia tena acha kuokoteza story mara ooooooh nmesikia kwa fulani!
 
Tangu lini huyo mdudu akawa halali kuliwa? China,korea n.k wamechomwa moto kutokana na maradhi. Mmepewa kila aina ya wanyama kama vile ng'ombe, mbuzi,kondoo,kuku na bata mle lakini hamridhiki
Walichomwa Moto kutokana na maradhi yaliyowapata hao viumbe kipindi hicho, baada ya hapo waliendelea kula. Hata ukiingia ugonjwa wa mafua ya ndege huwa tunapewa tahadhari kuhusu ulaji wa kuku
 
Hata mkoani Mbeya Shwain marufuku fuga kuku mkuu achana na mifugo haramu

Kule mbeya tangy homa ya bonde la Ufa ilivyotikisa hata Mabucha hamna wauuzia kwenye vidoo kwa kuibia

Kitu haramu effect yake inaonekana hapahapa ulimwenguni

Shwain Marufuku kwa ustawi wa Afya yako #slogan

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa ila fanyia Kaz ujumbe niliokupa, Isaya 66 kasome yote taratibu ,neno kwa neno

Na imani utaachana na Hayo manguruwe

Sent using Jamii Forums mobile app
Asome na Isaya 65

3 watu wanikasirishao mbele za uso wangu daima, wakitoa dhabihu katika bustani zao, na kufukiza uvumba juu ya matofali;
4 waketio kati ya makaburi, na kulala katika mahali pao pa siri; walao nyama ya nguruwe, na mchuzi wa vitu vinichukizavyo u katika vyombo vyao;
 
Tii maagizo ya Mungu Mambo ya Walawi 11
Hayo maandiko huyajui. Hakuna katazo. Kasome maandiko yanayohusiana na katazo hilo kwenye biblia, utaona kuwa kimsingi hakuna katazo. Bali kuna maagizo yaliyoelekezwa kwa kundi fulani la watu. Usitake kulazimisha mfanano wa maandiko ya Biblia na maandiko ya vitabu vingine
 
SUBIRI JEHANUM MAANA SISI BINADAMU NI WABISHI SANA ,SUBIRI MUNGU ATAKAVYOKUSANYA MATAIFA YOTE ATAKAPOTOA KICHAPO KWA WALA NGURUWE,PANYA ,KENGE NA MACHUKIZO MENGINE

ISAYA 66

15 Maana Bwana atakuja na moto, na magari yake ya vita kama upepo wa kisulisuli; ili atoe malipo ya ghadhabu yake kwa moto uwakao, na maonyo yake kwa miali ya moto.

16 Kwa maana Bwana atateta na wote wenye mwili, kwa moto na kwa upanga wake; nao watakaouawa na Bwana watakuwa wengi.

17 Watu wale wajitakasao, na kujisafisha katika bustani, nyuma yake aliye katikati; wakila nyama ya nguruwe, na machukizo, na panya; watakoma pamoja, asema Bwana.

18 Nami nayajua matendo yao na mawazo yao; wakati unakuja nitakapokusanya mataifa yote na lugha zote; nao watakuja, nao watauona utukufu wangu.

SIO MIMI NI BWANA KASEMA HIVO, SITAKI POVU

Sent using Jamii Forums mobile app
Wanafunzi wa Yesu wakauliza, tukibaribishwa chakula .......kuleni vyote wala msiulize ulize; ....akaambiwa ...... kula usikiite najisi. Ningepata muda ningekupa mstari. Kuleni vyote wala msiulize ulize;panya, nguruwe, nyoka mjusi etc. mradi hudhuriki. Nyakati hizi hatujafungwa kwa chakula. Ukisusa sisi twala
 
Asome na Isaya 65

3 watu wanikasirishao mbele za uso wangu daima, wakitoa dhabihu katika bustani zao, na kufukiza uvumba juu ya matofali;
4 waketio kati ya makaburi, na kulala katika mahali pao pa siri; walao nyama ya nguruwe, na mchuzi wa vitu vinichukizavyo u katika vyombo vyao;
Amri za Mungu ni zaidi ya kumi;nyingi sana
 
mbona mi nakula


Samahani sana mkuu, mimi sikukatazi kula kitimoto lakini huenda hichi nitakacho kueleza kikakushangaza lakini ndiyo ukweli.

Katika Wanyama "wanaoliwa" na binadamu ni Nguruwe pekee anayefanya Ushoga (sodomy), ukiweka madume ya nguruwe pamoja hata kama majike wapo aghlabu kuyaona yakifanyana wao kwa wao, wataalamu wa lishe na chakula wanasema "you are what you eat", yaani mtu yupo (kitabia na mienendo) kulingana na chakula alacho, sasa kwa watu wanaokula sana kitimoto kuna uwezekano mkubwa wao kuwa mashoga sababu ya kula hiyo nyama.

Nguruwe ni miongoni mwa wanyama waliokuwa karibu sana kimfumo ( utendaji wa mifumo mwilini) na binadamu kuliko wanyama wote, hivyo basi ukila nyama yake unakuwa karibu mno na kula NYAMA ya mtu-- kwa maneno mengine ladha ya nyama ya nguruwe inafanana na ladha ya nyama ya mtu, ndiyo maana madaktari leo duniani wanafanyia utafiti wa viungo vya nguruwe kama Maini, macho, mapafu, kongosho nk, viwe viungo mbadala kwa ajili ya binadamu, na hiyo ndiyo faida ya nguruwe kwa binadamu na siyo kula nyama yake.

Ndiyo maana vitabu vitakatifu vyote, vya waislamu, wakristo ,wayahudi vimeharamisha kitimoto kwa sababu ni nyama yenye madhara mengi katika mwili wa binadamu inapoliwa.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom