Katavi: Wahudumu watatu wa afya Wachunguzwa kwa wizi wa Dawa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,801
11,961
DESEMBA 19, 2020

WAHUDUMU watatu wa afya katika kituo cha Ilembo Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wanachunguzwa kwa makosa ya wizi wa dawa za serikali pamoja na kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa wagonjwa wanaolazwa kwenye kituo hicho.

Christopher Nakua, ambaye ni Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Katavi amebainisha kuwa wahudumu wa afya ambao ni Hussein Hassan Kimaro, Charles Daniel na Isack Muhigi wanachunguzwa na taasisi hiyo na pindi uchuguzi huo utakapokamilika na tuhuma hizo kuthibitika watuhumiwa watafikishwa mahakamani.
 
Ila KANGE LUGULA hadi leo anapeta mtaani Mh Rais alisema kuna kulikuwa na harufu ya upigaji!Wangekuwa na kipato cha kutosha sidhani kama wangeiba😭😭
 
Back
Top Bottom