Katavi: Tundu Lissu apinga Muswada wa Sheria ya Usalama wa Taifa kuwasilishwa bungeni, adai utaleta Ukiritimba

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
116,495
215,349
Akizungumza kwenye Oparesheni ya chama chake inayoitwa 255 ambayo sasa iko Mkoa wa Katavi Tundu Lissu, amedai kwamba amepewa Taarifa ya kupelekwa Muswada wa marekebisho ya sheria ya Usalama wa Taifa Bungeni, kwenye vikao vinavyoendelea huku akidai kwamba Muswada huo una nia ovu.

Mbele ya Maelfu ya Wananchi Lissu amedai kwamba lengo la Muswada huo ni kumpatia Rais Mamlaka ya moja kwa moja ya kuendesha shughuli za Usalama wa Taifa na kuondoa mamlaka hayo kwa Waziri wa Utawala Bora kama ilivyo sheria ya sasa ambayo ilitungwa wakati wa uongozi wa Benjamin Mkapa, ambako Mawaziri waliowahi kuhudumu walikuwa Mkuchika na Masilingi.

Lissu amesema kifungu cha 5:2(b) cha sheria hiyo ya mwaka 1996 kinakataza maofisa wa Usalama wa Taifa kufanya kazi za Polisi, jambo ambalo kwenye muswada huu wa sasa linaenda kuondolewa.

Anasema ndani ya Muswada huo hata wale walinzi wa Wagombea wa Urais wakati wa Uchaguzi, wale waliokuwa Polisi na waliratibiwa na IGP sasa wanatakiwa waondolewe na Wawekwe maofisa wa Usalama wa Taifa ambao wataripoti moja kwa moja kwa Rais ambaye naye atakuwa Mgombea, maana usalama wa Taifa ni kitengo kitakachokuwa chini yake moja kwa moja.

Toa Maoni yako.

Pia soma: Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa unaoifanya iwe chini ya Usimamizi wa Rais watua Bungeni
 
Mungu aibariki sana Chadema kwa kuwaamsha na kuwapigania watanzania

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
CHADEMA au Tundu Lissu? Mimi naona Lissu (mnyika, heche na wengine wenye mtizamo kama wao) wanaenda kuwa watu pekee relevant ndani ya chama chenu, wengine wameridhika na kuwa 'chama kikuu cha upinzani', wanawaza majimbo watakayopewa na mwenyekiti wa CCM hiyo 2025.

BTW, naungana na Lissu, badala ya kumpunguzia madara Rais wanataka kumwongezea? Hapo kweli kuna nia ovu. Taasisi zinazofanya kazi kwa siri bila uwajibikaji ziko kwenye hatari kubwa zaid ya kutumiwa vibaya ma wenye madaraka kukandamiza wengine.

Intelligence service should never be turned into a president's personal tool.
 
Anasema ndani ya Muswada huo hata wale walinzi wa Wagombea wa Urais wakati wa Uchaguzi , wale waliokuwa Polisi na waliratibiwa na IGP , sasa wanatakiwa waondolewe na Wawekwe maofisa wa Usalama wa Taifa ambao wataripoti moja kwa moja kwa Rais , ambaye naye atakuwa Mgombea , maana usalama wa Taifa ni kitengo kitakachokuwa chini yake moja kwa moja.
Huyu Mwamba kwa akili hizi kila siku anakuwa Ahead of Time
 
Hayo marekebisho ndio sahihi na yanaleta uhalisia. Utawala bora ilikuwa kivuli tu bora ijulikane direct Rais yuko responsible.

Hofu ya kuondolewa Polisi kwa wagombea itabadili nini wakiwa usalama? Bado Rais ni amri jeshi mkuu akitaka taarifa atazipata tu.

Issue ya Usalama kukatazwa kufanya kazi za Polisi nafikiri iliwafunga mikono Usalama na wakati mwingine kuhatarisha kuharibu operation zao. Ijulikane tu aina ya makosa watayo deal nayo direct bila kupitia Polisi.
 
L
CHADEMA au Tundu Lissu? Mimi naona Lissu (mnyika, heche na wengine wenye mtizamo kama wao) wanaenda kuwa watu pekee relevant ndani ya chama chenu, wengine wameridhika na kuwa 'chama kikuu cha upinzani', wanawaza majimbo watakayopewa na mwenyekiti wa CCM hiyo 2025.

BTW, naungana na Lissu, badala ya kumpunguzia madara Rais wanataka kumwongezea? Hapo kweli kuna nia ovu. Taasisi zinazofanya kazi kwa siri bila uwajibikaji ziko kwenye hatari kubwa zaid ya kutumiwa vibaya ma wenye madaraka kukandamiza wengine.

Intelligence service should never be used a president's personal tool of intimidation and expression.
Lissu yuko vizuri sana
 
Kwa maslahi ya Ccm ni sahihikwa maslahi ya Taifa Rais ni binadamu tu kama wewe Responsibility ibaki kwenye Taasis na sio kwenye mtu.
Hayo marekebisho ndio sahihi na yanaleta uhalisia. Utawala bora ilikuwa kivuli tu bora ijulikane direct Rais yuko responsible.

Hofu ya kuondolewa Polisi itabadili nini wakiwa usalama? Bado Rais ni amri jeshi akitaka taarifa atazipata tu.

Issue ya Usalama kukatazwa kufanya kazi za Polisi nafikiri iliwafunga mikono Usalama na wakati mwingine kuhatarisha kuharibu operation zao. Ijulikane tu aina ya makosa watayo deal nayo direct bila kupitia Polisi.
 
Hayo marekebisho ndio sahihi na yanaleta uhalisia. Utawala bora ilikuwa kivuli tu bora ijulikane direct Rais yuko responsible.

Hofu ya kuondolewa Polisi kwa wagombea itabadili nini wakiwa usalama? Bado Rais ni amri jeshi mkuu akitaka taarifa atazipata tu.

Issue ya Usalama kukatazwa kufanya kazi za Polisi nafikiri iliwafunga mikono Usalama na wakati mwingine kuhatarisha kuharibu operation zao. Ijulikane tu aina ya makosa watayo deal nayo direct bila kupitia Polisi.
Ngoja apate mamlaka zaidi awashushulikie vizuri Sukuma Gang😀
 
Hayo marekebisho ndio sahihi na yanaleta uhalisia. Utawala bora ilikuwa kivuli tu bora ijulikane direct Rais yuko responsible.

Hofu ya kuondolewa Polisi kwa wagombea itabadili nini wakiwa usalama? Bado Rais ni amri jeshi mkuu akitaka taarifa atazipata tu.

Issue ya Usalama kukatazwa kufanya kazi za Polisi nafikiri iliwafunga mikono Usalama na wakati mwingine kuhatarisha kuharibu operation zao. Ijulikane tu aina ya makosa watayo deal nayo direct bila kupitia Polisi.
Kitengo cha madawa nacho walikua hivyo hivyo ila sheria ikabadilishwa wakawa na uwezo wa kubeba silaha.

Hapo awali Operesheni zao iliwalazimu kuzifanya na polisi.

Polisi nao kwa kweli ndio vile tena.
 
Hayo marekebisho ndio sahihi na yanaleta uhalisia. Utawala bora ilikuwa kivuli tu bora ijulikane direct Rais yuko responsible.

Hofu ya kuondolewa Polisi kwa wagombea itabadili nini wakiwa usalama? Bado Rais ni amri jeshi mkuu akitaka taarifa atazipata tu.

Issue ya Usalama kukatazwa kufanya kazi za Polisi nafikiri iliwafunga mikono Usalama na wakati mwingine kuhatarisha kuharibu operation zao. Ijulikane tu aina ya makosa watayo deal nayo direct bila kupitia Polisi.
Unataka wafunguliwe mikono na wao waanze kukimbizana na wezi na kazi zingine za ulinzi wa raia na Mali zao?
 
Kati ya maswala mtambuka nchi hii ni pamoja na hii idara.
Pengine nadhan ingekuwa jambo la maana ikawa huru chini ya rais, badala chini ya utawala bora ambapo hata sifa za kuchaguliwa hazijulikani.
Lakini zaid wajibu wao kwa umma uwe mkubwa na wa kizalendo kweli kama ilivyo mashirika mengine ya ujasusi duniani.

Lazima kuwe na namna ya kudhibiti hawa vishoka wanaotembea na bastola baa na kuvunja sheria za usalama barabarani bila sababu za msingi.

Kazi ya usalama wa taifa iwe kwel ya weledi.

Hofu ya Lissu kuhusu askari wa mgombea urais ni unjustified kwa sababu, wanaweza amua Afisa usalama akavalishwa nguo za polisi na bado akaripot moja kwa moja magogoni... yote yanawezekana.
 
CHADEMA au Tundu Lissu? Mimi naona Lissu (mnyika, heche na wengine wenye mtizamo kama wao) wanaenda kuwa watu pekee relevant ndani ya chama chenu, wengine wameridhika na kuwa 'chama kikuu cha upinzani', wanawaza majimbo watakayopewa na mwenyekiti wa CCM hiyo 2025.

BTW, naungana na Lissu, badala ya kumpunguzia madara Rais wanataka kumwongezea? Hapo kweli kuna nia ovu. Taasisi zinazofanya kazi kwa siri bila uwajibikaji ziko kwenye hatari kubwa zaid ya kutumiwa vibaya ma wenye madaraka kukandamiza wengine.

Intelligence service should never be turned into a president's personal tool.
A tiger watching a chicken pen. Tafsiri: Kicheche kupewa kazi ya kulinda banda la kuku. Total conflict of interest.
 
24 Reactions
Reply
Back
Top Bottom